Friday, 25 March 2011
JESHI LA NATO SASA KUDHIBITI ANGA LIBYA
Majadiliano yanaendelea kuhusu nani aongoze harakati za kijeshi
Shirika la kujihami la NATO sasa limekbali kuchukua jukumu la kuthibiti anga ya Libya ili kuhakikisha marufuku ya ndege kutopaa inatekelezwa.Hatua hii imeafikiwa kwenye kikao cha waakilishi wa nchi wanachama wa shirika hilo mjini Brussels Ubeljiji.
Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema wanachama wote wa shirika hilo wameunga mkono uamuzi huo. Marekani ndio imekuwa ikisimamia utekelezaji huo lakini inataka kukabidhi wadhifa huo haraka iwezekanavyo.
Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema wanachama wote wa shirika hilo wameunga mkono uamuzi huo. Marekani ndio imekuwa ikisimamia utekelezaji huo lakini inataka kukabidhi wadhifa huo haraka iwezekanavyo.
UONGOZI WA VODACOM WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI
Mkurugenzi wa IPP media Joyce Mhavile akifafanua jambo kwa Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare , Mkurugenzi Mahusiano wa Vodacom Mwamvita Makamba mara walipotembelea IPP media group leo kwa ajili ya kujenga mahusiano ya kufanya kazi kwa pamoja.
Baadhi ya wageni wa Vodacom Tanzania na viongozi mbalimbali wa Africa Media group wakiangalia jinsi matangazo yanavyorushwa kwenye radio ya Magic FM.
Mtendaji Mkuu wa New habari Hussen Bashe akimuonyesha Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare wapili toka kushoto jinsi wanavyoaanda habari kwenye magazeti yao ,mara walipotembelea New habari kwa ajili yakuweka mahusiano mazuri ya kufanya kazi pamoja,kushoto Mkurugenzi wa mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,kulia Mtaalamu wa mambo ya habari wa Vodacom Matina Nkurlu.
SPIKA MAKINDA ATEMBELEA SIERRELEONE
Spika Makinda akizungumza na Watanzania waishio Freetown, SierraLeone walipomkaribisha chakula cha jioni. Kulia kwake ni Emmy Musokwa Bingwa wa Uangalizi na Ufuatiliaji wa PAGE , mwingine ni Omary Mjenga Mwakilishi Mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la UNOPS
Thursday, 24 March 2011
BALOZI WA NORWAY NCHINI ATEMBELEA OFISI ZA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU RAIS - MUUNGANO
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Samia Suhulu Hassan akiwa na balozi wa Norway nchini Tanzania Ingunn Klepsvik katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo yao ya changamoto za muungano na mabadiliko ya katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na serikali ya Umoja wa Kitaifa, ofisisni kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Samia Suhulu Hassan akizungumza Balozi wa Norway nchini Tanzania Ingunn Klepsvik kuhusu masuala ya serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. (picha na Ali Meja)
MASHAMBULIZI YAINGIA SIKU YA SITA LIBYA
Kiongozi mmoja wa muungano wa wanajeshi wa nchi za magaharibi amesema wamevunja ngome za kikosi cha wanajeshi wa anga wa Libya.Jemedari Greg Bagwell kutoka Uingereza amesema kikosi hicho hakina nguvu za kuwashambulia raia na hata ndege zao zinazopaa nchini humo.
Jemedari Bagwell akizungumza kwenye kituo chao cha kijeshi nchini Italy, ameongeza kuwa wanajeshi wa ardhini watalengwa wakati wowote watakapo shambulia raia.
TASWIRA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR
Msajili wa vyama vya siasa, John Tendwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais, Fatma Ferej nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi jana(Picha na Hamad Hija,MAELEZO Zanzibar)
Mawaziri wa SMZ, Kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha uchumi na mipango ya maendeleo,Omar Yussuf Mzee akiwa na Waziri wa Afya, Juma Duni Haji wakiwa nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi leo Mjini Zanzibar wakitazama ujumbe mfupi wa simu waliotumiwa.(Picha na Hamad Hija, MAELEZO Zanzibar)
RAIS KIKWETE ATEMBELEA WIZARA YA UCHUKUZI
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akisalimiana kwa furaha na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu( SUMATRA) Bw. Israel Sekirasa mara baada ya kuhitimisha ziara yake Wizara ya Uchukuzi leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoshuhudia ni Katibu mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Eng. Omari Chambo (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Watendaji wa Wizara, Idara, Mamlaka na Taasisi za Wizara ya Uchukuzi leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amewataka viongozi hao kuzifanyia kazi changamoto zinazoikabili wizara hiyo zikiwemo uboreshaji wa huduma za reli, usafiri mijini,uboreshaji wa huduma za bandari, matengenezo ya viwanja vya ndege nchini na migogoro ya wafanyakazi.
MAKAMU WA RAIS ZIARANI MKOANI MWANZA
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr.Mohammed Gharib Bilal katikati akiwapungia mkono wananchi wa kijiji cha Busisi alipokuwa akitembea kutoka kwenye kivuko cha MV. Misungwi, wakati wa ziara ya kukangua na kuzindua miradi ya maendeleo ya wananchi wa Wilaya ya Geita.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kalangalala Wilayani Geita baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa maabara ya Shule hiyo leo, ambapo ameahidi kuchangia shiliongi milioni tano kwa ajili ya kuanzisha kitengo cha mtandao wa intanet katika Shule hapo. Makamu wa Rais yopo Mkoani Mwanza kwa ziara ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo. Amour Nassor VPO.
Wednesday, 23 March 2011
MAANDALIZI YA KILI MUSIC AWARD YAKAMILIKA
Mkurugenzi wa masoko wa TBL David Minja(wa pili kushoto) akikabithi mfano wa tuzo zitakazotolewa kwa wanamuziki bora kwa Mratibu wa tuzo Angello Luhalla wakati wakuzitambulisha kwa waandishi wa habari, George Kavishe Meneja wa bia ya Kilimanjaro na Afisa uhusiano wa TBL Dorres Malulu.
MIILI YA WASANII WA 5 STAR YAWASILI DAR JANA
Mwili wa marehemu Issa Kijoti ukiwa tayari kwa mazishi katika makaburi ya Mtoni Sabasaba usiku wa jana mara baada ya kuwasili kutoka Morogoro.
Mwili wa marehemu Issa kijoti ukishushwa kwenye gari baada ya kuwasili.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Emmanuel Nchimbi akihojiwa na wanahabari kutoka vyombo mablimbali wakati wa kupokea miili hiyo.
Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka na nyuma ni yake ni mkurugenzi wa Screen Master wakipokea miili ya marehemu.
Miili ya wanamuziki wa five star ilipo wasili jana usiku.
JK ATEITEMBELEA OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na watendaji waandamizi wa ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake katika ofisi hiyo kwa ajiri ya kujionea utekelezaji wa malengo mbalimbali
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na watendaji wa ofisi hiyo, Rais aliwaagiza kuharakisha zoezi la kuhakikisha watumishi wa umma nchini koteili kuokoa fedha za umma zinazopotea kutokana na mishahara hewa na wahusika kuchukuliwa hatua. (picha zote naVicent Tiganya wa Maelezo
Tuesday, 22 March 2011
MAJINA YA WASANII WA 5 STAR WALIOFARIKI KATIKA AJALI
Majina ya mwanamuziki wa kundi la 5 Star waliofariki katika ajali ya gari Mikumi Mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo yatajwa.
Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barbarani mkoani Morogoro Ibrahimu Mwamakula, marehemu hao ni Issa Kijoti(aliyeimba wimbo wa mchumu chumu mwaa),Nassoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashimu, Tizo, Omary Tall, Ngeleza Hassan, Hamisa Omary, Maimuna, Haji Msaniwa na mcheza show wa kitu Tigo Ilala jijini Dar es Salaam.
Amesema majeruhi tisa ambao wote ni wasanii wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro ni Mwanahawa Ally(55) kutoka kundi la East Africa Melody, Susan Benedict(32), Zena Mohamed(27), Samila Rajabu(22) na Mwanahawa Hamisi(36) wamelazwa wodi namba tatu.
Wengine waliolazwa katika hospitali hiyo ni Ally Juma(25), Rajbu Kondo(25), Shabani Hamisi(41), Msafiri Musa(22) na Issa Hamisi.
KUNDI LA TAARABU LA 5 STAR LAPATA AJALI
BAADHI YA WANAMUZIKI WA 5 STAR TAARABU
WANAMUZIKI WA BENDI YA FIVE STAR MODERN TAARABU ZAID YA 10, WAMEPOTEZA MAISHA KWA AJALI YA GARI HUKO MOROGORO ENEO LA MIKUMI NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA SANA NA HALI ZAO NI MBAYA. GARI HILO LILIKUWA NA WATU 22, LAKINI WAMENUSURIKA 5, HUKU WATATU WAKIWA WAMEUMIA KIDOGO. KWA MUJIBU WA VYANZO VYA HABARI INADAIWA GARI HILO LILIKUWA KWENYE MWENDO MKALI NA KUPELEKEA KUGONGA LORI LILILOKUWA LIMEPAKIA MBAO PEMBENI YA BARABARA, KUGONGA HUKO ILIPELEKEA VIFO VYA WATU 8, HAPO HAPO NA KISH AKAENDA UPANDE WA PILI AMBAPO LORI LINGINE LILIKUWA LINATEMBEA NDIPO ILIPOISHIA NA KUSABABISHA VIFO HIVYO ZAIDI YA 10, NA MAJERUHI WENGI.MAITI ZIMEHAARIBIKA VIBAYA SANA HALI AMBAYO HAZITAMBULIKI KUTOKANA KUWA VIWILI WILI. habari kwa hisani ya Andrew Chale(Tanzania Daima)
ANNA MAKINDA ATEMBELEA LIBERIA
Wanawake waishio Liberia wakiwa katika picha ya pamoja na Spika Anna Makinda
Watanzania waishio Liberia wakiwa katika picha ya pamoja na spika Anna Makinda walipomkaribisha chakula cha jioni.
Subscribe to:
Posts (Atom)