Saturday 2 August 2014

PICHA: CHADEMA WATWANGANA KAVUKAVU GEITA BAADA YA KUTOKEA FUNUNU YA KUTUHUMIANA MAMBO YA "MLUNGULA"

Na Steven Mruma credit to  Victor Bariety via Malunde1 blog, Geita

       Katika tukio lisilo la kawaida baadhi ya Viongozi wa juu wa CHADEMA Geita walijikuta wakizichapa kavukavu baada ya kutuhumiana mambo ya rushwa nadani ya Chama hicho baada ya wenzao,wakiwemo viongozi wa matawi zaidi ya 50 kukamatwa na vijana wa ulinzi wa chama hicho (Red Brigade) wakiwa katika hoteli ya Wandela mjini Geita wakiwa kwenye kikao cha siri na kudaiwa walikuwa wanapokea rushwa kutoka kwa wagombea.
        Kundi hilo la siri linadaiwa kuandaliwa na katibu wa Jimbo la Geita aliyepo sasa hivi Rogers Ruhega ikiwa ni mkakati wa kumuwezesha kurudi madarakani katika uchaguzi unaokuja ambao inaonekana ameelemewa na mgombea mwenzake Mutta Robert.
       Ruhega ambaye hakuwepo katika kikao hicho, inadawa wajumbe waliokutwa Hotelini hapo ni kundi lina lohaha kila siku kutaka arudi madarakani kwa gharama yoyote na moja ya mbinu walizokuwa wanatumia ni kuchafua mgombea mwenzake na kutoa rushwa.

        Tukio hili linashangaza na linaashiria ni jinsi gani baadhi ya Viongozi walivyokua na uchu wa madaraka kiasi cha kutumia njia za mkato ili kuingia madarakani, na huku ni kukosa uzalendo na mfano wa viongozi hawa ni dhahiri wanataka kulinda maslahi yao bali si kutatua na kuwasadidia wanachi wa Geita, na Taita kwa ujumla.  

      KWA KUSOMA KISA HIKI KWA UNDANI BOFYA HAPA [ CLICK HERE]
  
Hapa likua ni mara baada ya Red Brigades wavamia hotel na kukuta wenzao wanajichana kwa soda na maji kabla ya timbwili
Wafuasi wa CHADEMA wakitaka kuzichapa nje ya Wandela hotel mjini Geita katika tukio la wanachama chama hicho kukutwa kwenye kikao cha siri katika hotel ya Wandela iliyopo Shilabela mjini Geita, ambapo kwenye kikao hicho ilidaiwa walikuwa wanagawiwa mlungula ili kupitisha kambi ya Katibu wa CHADEMA jimbo la Geita Rogers Luhega ambaye yuko taabani kisiasa dhidi ya mpinzani wake Mutta Robert aliyeomba kugombea nafasi hiyo.
Vurugu zikiendelea nje ya Hotel hiyo vijana wa CHADEMA wakitunishiana misuri
Timbwili la aina yake likiendelea.
Red Brigades wakiwa nje ya hotel wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini kabla ya kutoa sintofahamu ya kukunjana.

Thursday 31 July 2014

PICHA:HUKU WAASISI WA VICTORIA FOUNDATION WAKILA BATA VYA KUTOSHA SIKUKUU YA IDD, VICTORIA FOUNDATION YAWAPONGEZA WAISLAMU WOTE DUNIANI KWA KUSHEHEREKEA SIKUKUU YA IDD KWA AMANI,

Na Steven Mruma [Dar es salaam]
    Jana ilikua idd pili Victoria Foundation ilitumia muda huo kuwapongeza waislamu wote duniani kwa kusheherekea sikukuu hiyo kwa amani. lakini pia haikuishia hapo waliwasihi kuendeleza yale mazuri waliyojifunza katika kipindi chote cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. 
    Katika kumaliziamalizia sikukuu ya IDD kulifanyika part ya nguvu na Mwenyekiti wa victoria foundation akiwa na ndugu na marafiki zake walikula bata vya kutosha ya kusindikiza iddi pili.

Sehemu ya waislamu wakiswali sala ya Iddi

Bata zikiendelea siku ya Idd pili
Sifa kubwa siku ya sikukuu ni kula tu na hakika watu tulikula
Huo ulikua ni mtoko maalum wa siku ya Iddi pili

Bata zikiendelea na pia kuchat kuwatakia ndugu na jamaa na marafiki Idd Mubarak

Ilikua ni Kula na kunywa kwenda mbele

Bata zikiendelea

Kupendeza siku muhimu kama ya sikukuu lilikua na jambo la muhimu na huo ndio ulikua mtoko wa dada yetu

Monday 28 July 2014

ZIARA YA WANA CCM TAWI LA LUKILINI KATA YA KALANGALALA WALIPOTEMBELEA MAKUMBUSHO YA BABA WA TAIFA.

Na Steven Mruma [Butiama]
    Tawi la Lukilini kata ya Kalangalala mkoani Geita walitembelea makumbusho ya Baba wa Taifa na walipokelewa na tawi la wana CCM Butiama alikotokea Baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere.
    Hii ilikua ni ziara maalum ya kujionea makumbusho ya Baba wa Taifa na kujifunza mambo mbalimbali na kubadilishana mawazo na wana CCM wa tawi la Butiama.


Wana CCM waLukilini walipotembelea makumbusho ya Baba wa Taifa na kupokelewa na wana CCM wa Butiama
Haya ni makaburi ya wazazi wa Hayati Mwl J.k. Nyerere
Histroia ya eneo hilo ikitolewa na wenyeji
Sehemu aliyopendelea kukaa baba wa Taifa
Hichi ni kiti alichokua akipenda kukikalia baba wa Taifa
Mh. Vicky akiwasha mishumaa juu ya kaburi la Hayati Bbaba wa Taifa
Mh. Vicky Kamata akitambulishwa kwenye tawi la Wana CCM Butiama walipotembelea Makumbusho ya Baba wa Tiafa

BAADA YA KUKUTANA NA MH. VICKY KAMATA, WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU GEITA WALILIA KUPATA SEHEMU YA UHAKIKA YA KUCHIMBA MADINI GEITA

Na Steven Mruma [Geita]
      Hivi karibuni Mh. Vicky kamata mbunge wa viti maalum Geita akichangia hoja Bungeni aliiomba serikali isikilize kilio cha wachimbaji wadogo wa dhahabiu mkoani Geita kwani uchumi wa wachimbaji hao wadogo unategemea sana kazi ya uchimbaji wa Dhahabu.
     Baadha ya kutoa ombi hilo kwa serikali iwatengee eneo maalum lenye dhahabu ya kutosha, hakuishia hapo Mh. Vicky alikwenda na kukutana na wachimbaji wadogo wa dhahabu na kusikiliza zaidi kilio chao huku wengi wakilia ugumu wa maisha kutokana na kukosa sehemu ya uhakika ya kuchimba madini hayo, kilio cha wachimbaji hao wa madini kilifika mbali zaidi baada ya wachimbaji hao kutaka eneo la uhakika lenye uzalishaji baada ya kutakiwa kuhama eneo la Samina kupisha muwekezaji.
      Baada ya kusikiliza kilio hicho cha wachimbaji wadogo wa Samina Mh. Vicky kamata aliwasihi wachimbaji hao watulie na kwamba kilio chao hakijadharauliwa na serikali na kuwaahidi kuwa muda si mrefu serikali itatoa majibu baada ya mazungumzo kati ya GGM na serikali.


Mh. Vicky Kamata akibadilishana mawazo  na baadhi ya viongozi, 
Mh. Vicky Kamata akizungumza na wachimbaji wadogo wa Dhahabu Geita

Mh. Vicky Kamata akisisitiza jambo alipokutana na kuzungumza na wachimbaji wadogo wa dhahabu
      

GEITA DOCUMENTARY

Contributors