Wednesday, 21 August 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU WAKE..

RAIS J.M. KIKWETE
     RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi za juu za utendaji wa Serikalini kwenye nafasi za Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Wizara mbalimbali, ambapo  wapo waliohamishwa, wataopangiwa kazi nyingine na yumo anayestaafu.

Kauli hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Rais amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji wa kazi za Serikali katika ngazi hizo za juu,” alisema Balozi Sefue.

Mabadiliko yaliyofanywa kwa upande wa Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo:

Katibu mkuu kiongozzi Balozi OMBENI SEFUE
  • Dk Florens Turuka amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

  • Joyce Mapunjo amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara  ya Viwanda, Biashara na Masoko.

  • Jumanne Sagini amekuwa Katibu  Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) awali alikuwa Naibu Katibu  Ofisi wa Waziri Mkuu - TAMISEMI.

  • Dk Servacius Likwalile amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, awali alikuwa Naibu Katibu Wizara ya

Fedha.

  • Dk Patrick Makungu amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, awali alikuwa  Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo.

  • Alphayo Kitanda amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, awali alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.

  • Dk Shaaban Mwinjaka amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara  ya Viwanda, Biashara na Masoko.

  • Dk Uledi Mussa amekuwa Katibu Mkuu Wizara  ya Viwanda, Biashara na Masoko, awali alikuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

  • Profesa Sifuni Mchome amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya  Elimu na Mafunzo ya Ufundi, awali alikuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.

  • Charles Pallangyo amekuwa Katibu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri.

  • Anna Maembe amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, awali  alikuwa Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo.

  • Sihaba Nkinga amekuwa Katibu  Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo.

  • Sophia Kaduma amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Balozi Sefue aliongeza kwamba:

  • Katibu Mkuu aliyepewa uhamisho ni  Peniel  Lyimo ambaye anahamia Ofisi ya Rais - Ikulu  kwenye “Presidential’s Delivery Bureau” kama Naibu Mtendaji Mkuu mwenye jukumu la kuanzisha na kuongoza Idara ya Mageuzi ya Kilimo mwanzoni alikuwa  Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu.

Makatibu wakuu watakaopangiwa kazi nyingine ni:-

  • Sethi Kamuhanda aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo 

Sunday, 18 August 2013

VIONGOZI SADC WAMPIGIA SALUTI RAIS KIKWETE, "JOYCE BANDA NAE ANENA"ATAKA WANWAKE WAPEWE NAFASI"

Baadhi ya wakuu wa SADC

           RAIS wa Malawi, Joyce Banda amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuimarisha demokrasia, amani na usalama katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC).
           Banda alitoa pongezi hizo wakati akihutubia Mkutano wa 33 wa Wakuu wa SADC baada ya kukabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo kutoka kwa Rais wa Msumbiji, Dk Armando Guebuza.
        “Wananchi wa Malawi, mimi na SADC tunampongeza Kikwete kwa kuimarisha amani, demokrasia na usalama katika jumuiya katika kipindi chake cha uongozi (wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na usalama “Pia Rais wa Msumbiji, Armando Guebuza katika uongozi wake wa uenyekiti alishirikiana na Kikwete kushughulikia matatizo ya kisiasa na kuufanya ukanda wa nchi za SADC kuwa na amani,” alisema Rais Banda, ambaye nchi yake ina mgogoro na Tanzania upand wa ziwa Nyasa.
        
Rais Kikwete na Rais Joyce Banda wa Malawi
  Mgogoro huo uliibuka baada ya Serikali ya Malawi bila kushauriana na Tanzania, kutoa leseni kwa kampuni mbili za kigeni, kutafuta mafuta katika eneo la Ziwa upande wa Tanzania na kuibua mgogoro huo.
       Chanzo cha mgogoro huo unaoshughulikiwa na jopo la marais wastaafu wa Afrika; Thabo Mbeki (Afrika Kusini), Joachim Chisano (Msumbiji), Festus Mogae (Botswana) na wanasheria saba wa kimataifa, ni mikataba yenye utata iliyoachwa na wakoloni. Alisema ambao ndo waloigawa mipaka hiyo wakati wa ukoloni.
       Katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Rais Kikwete katika asasi hiyo ya siasa, ulinzi na usalama aliweza kufanikisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe, ambao Robert Mugabe ameshinda kuingoza nchi hiyo kwa muhula mwingine na kumbwaga mpinzani wake mkubwa na aliyekuwa waziri mkuu Morgan Tvshangirai.
      Amefanikisha pia kuanza kwa mchakato wa amani na kuatikana kwa muafaka wa kisiasa nchini Madagascar.
    Pia katika kipindi chake, alifanikisha kupelekwa kwa wanajeshi wa kulinda amani katika mji wa Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo waasi wa M23 wanapambana na wanajeshi wa serikali. Wanajeshi hao wa kulinda amani wametoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.

        Rais Kikwete amekabidhi madaraka hayo jana kwa Rais wa Namibia, Hifikepunye Pohamba. Rais huyo wa Malawi Bi. Joce  Banda ameahidi amani, Akizungumzia mkakati wake wakati wa uongozi wake wa mwaka mmoja kama Mwenyekiti wa SADC, Banda alisema ili ukanda wa SADC uwe na amani na usalama ni lazima nchi wanachama zipambane na umasikini.

       “Lazima tuimarishe siasa za ndani za nchi zetu, tuwe wavumilivu wa kisiasa na tusaidie wanawake wasiwe nyuma,” alisema. Aliahidi kuimarisha jumuiya za kikanda pamoja na kilimo kwa maelezo kuwa kilimo ndicho mwajiri mkuu wa wananchi wa nchi za SADC.
“Nitahamasisha kilimo kiboreshwe ili wananchi wa SADC waweze kuendesha kilimo cha biashara na pia sekta binafsi waingie kwenye kilimo na tupate masoko mapya ya bidhaa za kilimo nje ya mipaka ya ukanda wetu”.
      Alitaka katika ukanda wa jumuiya ya SADC kuboreshwe mwingiliano wa wananchi wa nchi za ukanda huo. Alisema haiwezekani kuboreshwa kwa jumuiya za kikanda bila kuruhusu mwingiliano huru wa wananchi wake.
     Rais Banda alitaka wanawake wapewe nafasi katika uongozi na kujengewa uwezo katika kuimarisha uchumi na kuondokana na umasikini na kusisitiza kuwa, “wanawake ndiyo wanaopambana na umasikini, wanabakwa, wanakabiliwa na unyanyasaji na wengi wamepoteza utu wao”.

      Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Dk Nkosazana Dlamini- Zuma alizitaka nchi za Afrika kuimarisha miundombinu ili mazao ya wakulima yaweze kusafirishwa pamoja na kuboreshwa kilimo, uwekezaji na kujengwa kwa viwanda.“Lazima tufanye kazi pamoja kuwahakikishia chakula watu wetu wa SADC na Afrika haiwezi kuendelea bila kuweka wanawake kila maeneo na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazotukabili za tatizo la ajira kwa vijana, umasikini, sekta duni ya viwanda na tatizo la kutokuwepo usawa wa kijinsia,” alisema Zuma.



GEITA DOCUMENTARY

Contributors