Monday 2 February 2015

PICHA ZA PARTY YA MAMA ANNE KILANGO MALECELA ALIYOFANYIWA NA MUMEWE KUMPONGEZA KUWA NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI.

Na Steven Mruma [Dodoma]  

      ZIFUATAZO NI BAADHI YA PICHA CHACHE ZA PARTY YA MAMA ANNE KILANGO MALECELA ALIYOFANYIWA NA MUMEWE BAADA YA KUTEULIWA NA MH. RAIS DR. JAKAYA KIKWETE KUWA NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI AMBAPO KULIKUA NA BURUDANI MBALIMBALI IKIWEMO YA KWAYA YA UVUKE KUTOKA DODOMA. 

MAMA ANNE KILANGO MALECELA AKIPONGEZWA NA BAADHI YA AKINA MAMA KATIKA PARTY ALIYOFANYIWA NA MUMEWE YA KUMPONGEZA KUWA NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

MH VICKY KAMATA ALIKUA NI MIONGONI MWA WABUNGE WLIOKUWEPO KATIKA PARTY HIYO KAMA ANAVYO ONEKANA WA TANO KUTOKA KILIA

WAZIRI WA UCHUKUZI MH. SAWELI SITTA WA PILI KULIA NA MKWEWE MAMA MAGRETH SITTA  WA PILI KUSHOTO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MH. VICKY KAMATA MBUNGE VITI MAALUM GEITA  KUSHOTO NA MZEE JOHN MALECELA KULIA.

HUJAFA HUJAUMBIKA HUU NI MKASA UNAOWEZA KUKUKUTA WEWE AMA MIMI HATA LEO. SOMA KISA KIFUPI CHA KUSISIMUA CHA KIJANA AITWAYE BAHATI.

Imeandukwa na kuletwa na Steven Mruma kwa msada wa Betty Lucas Mwanza.

      Hiki ni kisa ambacho nilipenda kuwafikia wadau wengi wenye uwezo ili waweze kuwasaidia walemavu kwani ni kindi ambalo linaweza kuwa na uzalishaji na linashiriki kikamilifu katika kujenga nchi yetu..
     Bahati alipata msaada ambo umemfikisha hapa alipofika leo lakini shukrani za dhati zimfikie mwimbaji wa injili Dada Betty Lucas kwa msaada mkubwa sana aliompatia Kaka Bahati kama hapa alivyokua ananieleza kisa kizima na jinsi alivyomfahamu Bahati.
     "Bahati alikuja maeneo ya kanda ya ziwa akiwa na Baba yake mzazi wakitokea Dar es salam ambako waliwaacha Mama na ndugu zake. Baba yake alikua ni mganga wa jadi alizunguka huku na kule kutibu watu hatimae akafika kanda ya ziwa akiwa na mwanae yani Bahati. Miaka ilisonga baba wa Bahati akafariki kwa kuugua.
     Baada yakufariki yule mzee [Baba] Bahati amliiishi ktk familia za watu tofauti tofauti akifanya kazi kama kuchunga mifugo n.k lakini kuna usiku ambao ndio Usiku uliobadilisha historia yake akiwa amelala alishtuka usingizini baada yakung'atwa na kitu ambacho inahisiwa ni nyoka kwani hakikuonekana. Alipata maumivu makali lkn hakupata msaada wa matibabu kwa wakati hadi pale hali ilivyozidi kua mbaya ambapo alipelekwa hospitali ikaonekana tayari mguu umeoza. Bahati alikatwa Mguu kama anavyoonekana ktk picha.
  Nimeishi mtaani alikokua akiishi Bahati kwa mda wa miaka mitano Nilimfaham vizuri Baada yakukatwa Mguu wake alianza maisha mapya kabisa Kwani alikua hana furaha na hatimae akawa mlevi sana Hakua na uwezo wakufanya kazi zake tena Kila alipokua anakaa alifukuzwa kwani inasemekana alianza udokozi. 
      Mwaka huu mwezi wa pili [2014] Nilihama mtaa ule lakIni nilihama na Bahati mawazoni mwangu Nilitamani kumsaidia sikua na uwezo kabisaHatimae nikapiaita wazo la kuandaa tamasha nia ilikua nikupata pesa kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki pamoja na kumsaidia Bahati, Namshukuru Mungu tamasha lilifanyika nikapata pesa ambayo imeniwezesha kumsaidia Bahati ktk matibabu yake. 
     Kwasasa kazi ya Bahati ni kushona viatu nakubonda kokoto. Furaha ya Bahati ni kubwa mno Amekua na maswali mengi kama Nitaweza kuendesha baiskel? Inaonyesha ni namna gani alikosa vitu fulani katika maisha yake lakini pia anajiuliza kama anaweza kuinama nakufanya kazi. Tunashukuru sana pia kwa Dr Massawe wa Bugando ambaye ndio amefanya kazi yote ya kureebisha na kutibu mguu wa Bahati na  nimetumia sh milioni moja [1,000,000] kukamilisha matibabu yake. kwasasa Bahati anaishi mwanza wilaya ya Nyamagana kata ya Butimba mtaa wa Iseni anaishi ktk nyumba ya mtu ambayo inaendelea kujengwa" 

     Hayo nimaelezo niliyonukuu kutoka kwa Dada Betty Lucas ambaye pia ni mwnamuziki wa injili anayetamba na albam kadhaa ikiwemo KUNA NGUVU na UNAONA NINI. 


 ZIFUATAZO NI BAADHI YA PICHA ZA BAHATI WAKATI AKIWA BADO HAJAPATA MATIBABU NA BAADA YA KUPATA MATIBABU. 
Bahati kabla hajafanyiwa upasuaji na kuwekwa mguu wa bandia
Akiwa ametembelewa na Dactari aliyemfanyia mabibatu nyumbani kwake Iseni Nyamagana

Dr. Massawe kutoka Bungando akiendelea kutoa huduma kwa Bahati

Ijapokua alikata tamaa lakini sasa mwanga mpya wa maisha yake umeanza kuonekana na furaha iliyopotea sasa inarudi,.

Akiwa na team iliyohakikisha mguu wake unafanyiwa matibabu

hapa wakiangalia hali ya mguu wake ulivyo baada ya upasuaji wa kumuwekea mguu wa bandia kufanikiwa
sasa anaweza kutembea mwenyewe bila kutumia magongo

Maisha yamenza kuwa mapya na ya furaha.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors