Friday, 5 October 2012

Aliyetorosha twiga hai mbaroni



MTUHUMIWA Mkuu wa kashfa kubwa iliyowahi kuitingisha nchi na Wizara ya Maliasili na Utalii ya kusafirisha wanyama hai wapatao 130 nje ya nchi, Kamran Ahmed (30), anashikiliwa na Polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za kukutwa na fedha bandia kiasi cha shilingi milioni 18.

Thursday, 4 October 2012

Ajali yaua 10 Mbeya, mbunge anusurika




MBUNGE wa viti maalum mkoani Mbeya kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Mary Mwanjelwa, amenusurika kufa katika ajali mbaya iliyogharimu maisha ya watu takriban 10.
Katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani hapa, gari la mbunge huyo liligongwa na kuteketea kwa moto papo hapo.
Ajali hiyo imehusisha magari manne likiwemo lori la mafuta la kampuni ya Lake Oil lenye namba za usajili T 814 BTC, gari ndogo ya abiria (Hiace) yenye namba za usajili T 299 BCE na gari ya Mbunge huyo Mary Mwanjelwa Toyota Hilux T 671 ABM.

Wednesday, 3 October 2012

EVERY CHILD IS BORN A STAR

As the T-shirt says "I can be president" this can real be.Such a boy can come to be our president.Such a dream can be met only if we as a society will be touched to help him.
  As no one is born a president unless good environment is prepared to him, by giving him better education and provide him with all the necessary basic needs such as food, clothes, shelter and love............

               "We Believe every child is born a star, Help us to help them"

Tuesday, 2 October 2012

NEW FORM OF KIDNAPPING



This is very scary and could happen to any of us. Seems like every
nice thing people do for one another can be perverted.  A new twist on
kidnapping from a very smart survivor:


About a week ago there was a woman standing by the mall entrance of
Garden City, this woman had finished shopping, went out to her car and
discovered that she had a flat tyre.

Monday, 1 October 2012

CANCER BADO TISHIO AFRIKA


UGONJWA wa saratani umekuwa tishio katika nchi za Afrika zilizo chini ya Jangwa la Sahara ikiwamo Tanzania ambapo kwa mwaka 2010, takwimu zinaonesha umeua watu milioni 9.9 duniani.
Hayo yalibainishwa na mratibu wa kampeni ya kupambana na ugonjwa huo nchini kutoka Taasisi ya Tanzania 50 Plus, Mchungaji Dk. Emmanuel Kandusi, alipozungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
Alisema saratani ni hatari sana ukilinganisha na takwimu za magonjwa mengine ambapo malaria uliua watu 500,000, kifua kikuu milioni 2.1, ukimwi milioni 1.8. Saratani inaongoza kwa kuua watu milioni 9.9.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors