SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, amesema nchi yoyote haiwezi kuwa na maendeleo kama vijana hawatakuwa wabunifu wa kazi na kujiajiri.
Akipokea mitambo mitatu ya kutengenezea barabara kwa Mkoa wa Njombe jana, Makinda alisema licha ya halmashauri yake kupokea mitambo hiyo, aliomba boza la kunyunyizia maji wakati ujenzi wa barabara.
Mitambo hiyo yenye thamani ya Sh716 milioni, ilitolewa na Kampuni ya GF Truck and Equipments ya Dar es Salaam, inayojishughulisha na uuzaji mitambo mbalimbali.
“Nashukuru kampuni hii kwa kutoa mitambo mitatu ila ningeomba pia watuongezee boza ili kazi ya kutengeneza barabara iwe nzuri,” alisema Makinda na kuongeza: ”Hii mitambo mitatu itatufaa hasa tukiwa na boza, kwani eneo letu ni udongo tifutifu hivyo iwapo Kampuni ya FG itaongeza kifaa hicho, ujenzi wa miundombinu utakua haraka na kubadilisha mji wa Njombe.”
Awali, Ofisa masoko wa kampuni hiyo, Juma Hamsini, alisema wamefikia uamuzi wa kuikopesha kwa gharama nafuu Halmashauri ya Njombe baada ya kuwa ya kwanza nchini kuitikia wito uliotolewa na kampuni hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Njombe, George Mkindo, alisema hatua hiyo imefikiwa baada kuvutiwa na ubunifu wa hali ulionyeshwa na halmashauri yake katika upimaji viwanja na uboreshaji mji wa Njombe.
Kwa hisani ya Mwananchi comm
Wednesday, 30 May 2012
Tuesday, 29 May 2012
SAFARI YA KUTOKA GEITA KURUDI DAR ES SALAAM
Safari ilibidi kusimama kidogo baada ya kupata pancha maeneo ya Igunga
Team ya Victoria Foundation ikibadilisha tairi
Tukifunga tairi tayari kwa kuanza tena safari
Team ya Victoria Foundation ikibadilisha tairi
Tukifunga tairi tayari kwa kuanza tena safari
Monday, 28 May 2012
VICTORIA FOUNDATION YATOA MSAADA WA BAISKELI KWA WALEMAVU MKOANI GEITA WILAYA YA BUKOLI
Wamama wa wilaya ya Bukoli wakimkaribisha kwa furaha Mwenyekiti wa Victoria Foundation Vicky Kamata alipokuwa akiwasili wilayani kwa ajili ya kutoa msaada huo
Mama ambaye ni mlemavu(katikati) akisaidiwa na ndugu zake kuja eneo la tukio kwa ajili ya kupata msaada wa baiskeli
Walemavu wa wilayani Bukoli wakiwa wanasubiri kupokea msaada wa baiskeli zilizotelewa na Victoria Foundation
Baiskeli zilizogaiwa kwa walemavu hao
Wamama waliowasindikiza ndugu zao ambao ni walemavu kuja kupokea msaada wa baiskeli wakiwa wanafatilia kwa makini zoezi hilo
Mwenyekiti wa Victoria Foundation akiongea na wananchi wa Bukoli kabla ya kuanza zoezi la kugawa baiskeli kwa walemavu wilayani humo
Mwenyekiti wa Victoria Foundation akimsaidia mmoja wa walemavu kuvaa T-shirt iliyotolewa na Victoria Foundation
Mtoto ambaye ni mlemavu akiwa ameketi kwenye baiskeli yake mara baada ya kupokea msaada huo

Subscribe to:
Posts (Atom)