Wednesday 14 August 2013

NECTA: MITIHANI KUSAHIHISHWA KWA COMPUTER, ITAONGEZA UBORA WA USAHIHISHWAJI.



Joyce Ndalichako

          Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Joyce Ndalichako amesema baraza lake linajiandaa kutumia teknolojia ya kompyuta wakati wa kusahihisha maswali ya mitihani ambayo wanafunzi wanajibu kwa kujieleza.
Kwa sasa teknolojia ya usahihishaji kwa kompyuta inayotumika nchini ni ile ya kujibu maswali ya kuchagua tu ya`Optical Mark Reader’ (OMR) iliyoanza kutumika mwaka jana kusahihisha mitihani ya darasa la saba.
     
Akizungumza na mwandishi wa habari jana wakati wa Mkutano wa Mabaraza ya Mitihani Afrika (AEAA), unaoendelea mjini hapa, Dk Ndalichako alisema: “Kwa kuanzia, Necta itafanya majaribio ya teknolojia hiyo mwakani na ninaamini itaongeza ubora katika usahihishaji.”
“Kwa kutumia hii teknolojia msahihishaji hawezi kuona namba ya mwanafunzi, anachoona ni sehemu ya swali anayotakiwa kusahihisha na jibu lake, akimaliza swali moja jingine linakuja moja kwa moja,” aliongeza.
   Alisema kwa kutumia teknolojia hiyo, mratibu wa usahihishaji anaweza kuona kazi inayofanywa na msahihishaji yeyote na hata kuwapima kama atakuwa na wasiwasi wowote.
    Alisema Zimbabwe imeanza kutumia teknolojia hiyo aliyosema itasaidia kuongeza ubora katika suala la usahihishaji.
     Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jana, alisema teknolojia ya OMR imeongeza ubora wa hali ya juu kwenye mtihani wa darasa la saba pamoja na usahihishaji wake.
“ Watu wanasema kuwa mtihani wa maswali ya kuchagua ni mrahisi, lakini hii siyo kweli, inatungwa na wataalamu na inalenga kumpima mtoto katika kila nyanja, ndiyo maana hata mtihani wa darasa la saba mwaka jana ilibidi Serikali ishushe alama za kwenda kidato cha kwanza zikawa 70 badala ya 100,” alisema Dk Ndalichako.
        Akizungumzia teknolojia hiyo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema wamebaini kuwa zaidi ya asilimia 80 ya nchi za Afrika zinatumia mfumo wa usahihishaji kwa OMR.
    Alisema baadhi ya nchi zimeanza kusahihisha kwa kutumia kompyuta hata katika maswali ya kujieleza na kuwataka Watanzania kuacha kujirudisha nyuma.

Sunday 11 August 2013

Mh. VICKY KAMATA NA VICTORIA FOUNDATION KWA UJUMLA WAWAPONGEZA WAISLAM DUNIANI KOTE

Mh. Vicky Kamata
 Familia ya Mh. Vicky Kamata
     Ikiwa ni siku moja baada ya sikukuu ya IDI el fitri Familia ya  Mh. Vicky Kamata ambaye pia ni mbunge wa viti maalum Geita pamoja na Mfuko wake wa VICTORIA FOUNDATION, wamewapongeza waislamu wote duniani kwa kusheherekea sikukuu ya IDI EL FITRI kwa amani na utulivu.  Akitoa pongezi hizo Mh. Vicky alisema "huu ni mfano wa kuigwa katika kila sikukuu ili kuweza kulinda amani ya taifa na Dunia kwa ujumla.."   
        Waislamu wote duniani siku ya Ijumaa na Jumamosi walisheherekea sikukuu hiyo baada ya kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.. sikukuu hiyo huadhimishwa na waislamu wote duniani kila mwaka na huendana na mwandamo wa mwezi...


MAMA TUNU PINDA ALIPOTEMBELEA WANAKIJIJI WA ZEGERO

Hivi karibuni mke wa Waziri mkuu Mama Tunu Pinda aliwatembelea wanakijiji wa kijiji cha Zegero ambapo alikutana na viongozi wa serikali ya kijiji akiwemo mwenyekiti, mtendaji wa kijiji na wajumbe...
   katika ziara hiyo aliambatana na Mh. Vicky Kamata Mbunge Viti Maalum Geita,, Officer Mohamedi Mapunda Wa Jeshi la Polisi Makao Makuu na Afisa Kilimo na Mifugo wa Mh. Vicky Kamata Dr. Steven Mruma.. 

                    YAFUATAYO NI MATUKIO MUHIMU YA ZIARA HIYO KATIKA PICHA..
Mama Tunu Pinda akiwa na baadhi ya viongozi wa kijiji cha zegero na mh. Vicky Kamata walipotembelea wanakijiji hao.
Mama Tunu Pinda akisisitiza jambo mbele ya baadhi ya viongozi wa kijiji
Mama Tunu Pinda akifuatilia jambo na Mh. Vicky Kamata Na moja kati ya maofisa wa polisi inspecta Mohamedi Mapunda kulia
Mh. Vicky Kamata akishauri jambo mbele ya Mama Tunu Pinda na Officer M. Mapunda
officer Mohamedi Mapunda akishauri jambo
Mama Tunu Pinda akisalimiana na mmoja ya wanakijiji bwana Susatule..
Mama Tunu Pinda katika Picha ya pamoja na Afisa Kilimo na Mifugo wa Mh. Vicky Kamata Dr. Steven Mruma katikati na kulia ni Mh. Vicky Kamata
Mama Tunu Pinda na Baadhi ya Wajumbe wa Serikali ya kijiji
Mama Tunu PInda akirejea katka ofisi ya kijiji baada ya kukagua miradi mbalimbali ya wanakijiji..
Hapa akiwa na moja ya familia inayoishi Zegero
Akiwa nje ya hema ambalo pia ni moja kati ya sehemu ya malazi ya moja ya wanakijiji
 


akikagua moja ya hifadhi ya misitu ya kijiji hicho..

GEITA DOCUMENTARY

Contributors