Monday, 14 January 2013

SUGU AISHUKURU COCA COLA


MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) maarufu kwa jina la ‘Sugu’, ameishukuru Kampuni ya Coca Cola kwa kuwachangia sh milioni tano kwa ajili ya kusomesha watoto 360 watakaotoka kila kata katika jimbo lake.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Sugu alisema katika jimbo hilo wameanzisha mfuko wa kusaidia watoto wasiojiweza unaoitwa Mbeya Education Fund ambao kila mdau anayeguswa na elimu ni muhimu kuuchangia bila kujali itikadi ya chama.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors