Tuesday, 22 March 2011

MAJINA YA WASANII WA 5 STAR WALIOFARIKI KATIKA AJALI

Majina ya mwanamuziki wa kundi la 5 Star waliofariki katika ajali ya gari Mikumi Mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo yatajwa.

Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barbarani mkoani Morogoro Ibrahimu Mwamakula, marehemu hao ni Issa Kijoti(aliyeimba wimbo wa mchumu chumu mwaa),Nassoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashimu, Tizo, Omary Tall, Ngeleza Hassan, Hamisa Omary, Maimuna, Haji Msaniwa na mcheza show wa kitu Tigo Ilala jijini Dar es Salaam.

Amesema majeruhi tisa ambao wote ni wasanii wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro ni Mwanahawa Ally(55) kutoka kundi la East Africa Melody, Susan Benedict(32), Zena Mohamed(27), Samila Rajabu(22) na Mwanahawa Hamisi(36) wamelazwa wodi namba tatu.

Wengine waliolazwa katika hospitali hiyo ni Ally Juma(25), Rajbu Kondo(25), Shabani Hamisi(41), Msafiri Musa(22) na Issa Hamisi. 

No comments:

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI