MSANII maarufu wa filamu nchini, Sadick Kilowoko ‘Sajuki’, kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya hadi kupelekwa nchini India kwa matibabu.
Baada ya matibabu ya muda mrefu, msanii huyo alirejea nchini akiwa amepata nafuu kubwa tofauti na wakati anakwenda hivyo akawashukuru wote waliofanikisha gharama za safari yake.
Lakini pamoja na kurejea nchini akiwa amepata nafuu kubwa, bado akatakiwa kurejea India kwa uchunguzi na matibabu zaidi, kitu ambacho pia kinahitaji gharama kubwa ya fedha.
Kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu (Dennis Sweya), Sajuki anahitaji kiasi cha shilingi mil. 28, ikiwa ni gharama za kwenda na matibabu nchini India.
Zimebaki shilingi mil. 21 kupata kiasi cha fedha kinachohitajika kwa ajili ya msanii huyo kwenda India kwa matibabu zaidi katika kupigania uhai wake.