Saturday, 24 May 2014

PICHA: MH. VICKY KAMATA AKIWA AMELAZWA HOSPITALI BAADA YA KUUGUA SAA CHACHE KABLA YA NDOA YAKE... HALI YAKE YAZIDI KUIMARIKA PIA SOMA ALICHOKIZUNGUMZA NILIPOMTEMBELEA KUJUA HALI YAKE.

Na Steven Mruma

      Ni tukio nadra sana kutokea na mara linapotokea lazima ukubali ukweli na hali halisi, zilibaki saa 36 tu kabla ya kufungwa kwa  ndoa ya Mh. Vicky Kamata mbunge wa viti maalum Geita na msanii wa muziki ambaye pia amejizolea umaarufu  kwa kutetea haki za wanawake.
       Ilikua ni jioni ya alhamisi Mh. Vicky alianza kujiskia vibaya na kila muda uliposonga hali yake ilizidi kuwa tete na hatimaye alikimbizwa katika hospitali ya General Hospital iliyopo Tabata Segerea..
       Kuugua huko kulifanya ndoa yake kuahirishwa baada ya vipimo vya daktari kudhibitisha kuwa hataweza kufunga ndoa  na sababu kubwa ikiwa ni hali ya maumivu makali ya tumbo, Presha kuwa chini sana na Kutapika sana, Hayo yanatokana na ujauzito alio kuwa nao ambapo isingekua rahisi kwake kuhumili suala zima la ndoa na sherehe yake kwa ujumla kwakua ingehatarisha maisha ya mtoto aliye tumboni, kwani ujauzito huo ungeweza kuharibika na kutoka.
       Daktari aliongeza pia presha yake ilikuwa chini sana na alikuwa anatapika sana jambo lililomfanya Mh. Vicky kuishiwa nguvu.
   Leo asubuhi nilifika hospitali kwa mara nyingine kujua hali yake na aliweza kuongea na mimi machache na kunieleza kua hali yake imeanza kuimarika na maumivu pia yameanza kupungua na aliweza kuongea vizuri tofauti na hali ya jana ambapo alikuwa hawezi kuongea na kila alipojaribu alionekana kushindwa kuongea sababu ya maumivu makali aliyokuwa anayapata.
    " Hali yangu ni nzuri kwakweli namshukuru sana Mungu najiskia vizuri asanteni kwa maombi yenu na natumai hali yangu itaimarika na nitarejea katika hali ya kawaida muda sio mrefu" alisema Mh. Vicky huku akioneka bado anauchovu kidogo.

Na hii ndio Hospitali aliyolazwa Mh. Vicky Kamata
Mh. Vicky Kmata akiwa amelala hii ilikuwa mara tu nilipoingia wodini alipolazwa na nilisubiri dakika kadhaa na aliweza kuamka na nikazungumza nae.
Mh. Vicky Kamata akiwa amepunzika wakati nilipofika kumuangalia na kuzungumza nae juu ya hali yake.
Steven Mruma [mwandishi wa habari hii] kushoto, hapa nikiongea  na Mh. Vicky Kamata, ilikua ni baada ya kumuamsha na kujua hali yake ambapo aliamka na tukaanza kuzungumza machache juu ya afya yake.
Hapa akinielezea hali yake kwa ujumla
Baada ya Muda baadhi ya ndugu jamaa na marafiki zake nao walifika kutaka kujua hali yake na alionekana mchangamfu sana ikiashiria hali ya afya yake kuimarika .
Ndugu na Marafiki waliofika kumuona hospitalini leo

4 comments:

Unknown said...

Getwell soon sis

Anonymous said...

Pole sana Dada Vicky hayo no majaribu ya shetani inshalah utapona

Anonymous said...

mungu akuponye haraka vicky,ushauri wangu tu rudi magotini kwa mungu sema" asante wewe ni mungu mkuu,unayetuazia mema " !

Anonymous said...

Its like you read my mind! You seem to know a lot about this, like you wrote
the book in it or something. I think that you could do with a few pics
to drive the message home a bit, but instead of that, this is excellent
blog. A fantastic read. I'll definitely be back.


my web-site - diy improvements ()

GEITA DOCUMENTARY

Contributors