Saturday 28 April 2012

TRA yapunguza kodi ya bodaboda


MAMLAKA ya Mapato (TRA) mkoani Morogoro, imewapunguzia kodi wafanyabishara ya pikipiki maarufu kama bodaboda kutoka Sh95,000 hadi Sh35,000 kwa mwaka kwa pikipiki moja. 

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na kaimu Meneja wa mamlaka hiyo mkoani hapa, Kilomba Kanse na kuthibitishwa na Meneja wa Mkoa, Hakim Kimungu, hatua hiyo imefikiwa na mamlaka kufutia ombi la wafanyabishara hao kutaka kupunguziwa kodi hiyo. 

Uelimishaji kupunguza vifo vya malaria nchini

TANZANIA inaweza kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria kwa kiwango kikubwa, iwapo Serikali itaweka mfumo maalumu wa uelimishaji jamii kwenye ngazi ya vijiji.

Kulingana na takwimu zilizotolewa na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) nchini, watu 80,000 wanakadiriwa kufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huo na asilimia 36, ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Wednesday 25 April 2012

Study tour ya kamati ya Nishati na madini nchini Norway


Hapa tukiwa tumemaliza kikao na wabunge wa bunge la Norway

LEO NI SIKU YA MALARIA DUNIANI


Shirika la Afya Duniani, WHO, inaripoti kwamba mwaka 2009 takriban watu bilioni 3.3, ikiwa ni nusu ya wakazi wote duniani, walikabiliwa na hatari ya kuambukizwa na malaria. Kila mwaka hiyo inapelekea watu milioni 250 kuugua homa ya malaria na kusababisha karibu vifo elfu 850.

Mkutano mkuu wa wa 60 wa Shirika la Afya  Duniani ulizindua rasmi siku ya malaria duniani mwaka 2007 kuadhimisha  juhudi duniani za kudhibiti ugonjwa wa Malaria.


Siku hii ni ya kutathmini maendeleo yaliyopatikana katika kudhibiti na kutokomeza kabisa malaria, pamoja na kuhamasisha upya juhudi kuelekea lengo la kutokuwepo tena kifo hata moja kutokana na malaria ifikapo 2015.
Kundi la madaktari wasio na mipaka linasema Malaria ni muuaji mkubwa wa watoto chini ya umri wa miaka mitano katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara. Kundi hilo la wataalamu wa afya linasema nchi zilizoendelea zinatakiwa kuwa na nia thabiti ya dhati  kuzisaidia nchi zinazoendelea katika kupambana dhidi ya Malaria.


Lengo la kauli mbiyo ya mwaka huu "kupata maendeleo na mafanikio" ni kutokomeza vifo kutokana na malaria ifikapo 2015

Tuesday 24 April 2012

Maelfu wamzika Mutharika


MAELFU ya wananchi wa Malawi jana walifurika katika Shamba la Ndata, Thyolo kusini mwa Blantyre ambako aliyekuwa Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika alizikwa.

Rais wa Malawi, Joyce Banda aliwaongoza maelfu ya wananchi hao wakiwamo marais watano wa Afrika, wawakilishi wa nchi, mashirika ya kimataifa na jumuiya za kikanda katika mazishi hayo yaliyofanyika kutwa nzima ya jana.

Mh. Vicky Kamata akiwa ziarani nchini Norway






GEITA DOCUMENTARY

Contributors