Friday, 22 August 2014

TANZIA: MKURUGENZI WA TISS MSTAFU [USALAMA WA TAIFA] AFIWA NA DADA YAKE ANGALIA BAADHI YA PICHA ZA MAZISHI

Na Steven Mruma [ Bunda-Mara]
      Hivi majuzi aliyewahi kua Naibu mkurugenzi Usalama wa Taifa [TISS] Ndugu Jack Zoka alipata msiba mkubwa kwa kufiwa na dada yake mkubwa aitwaye Wakuru Mugendi kilichotokea huko mkoani mara.
      Mazishi yalifanyika huko kijijini kwao Changuge Bunda mkoani Mara huku Baadhi ya Viongozi akiwemo Mh. Vicky kamataMbunge Viti maalum Geita RSO wa Mwanza Meja Jason M. na Mzee Selemani Kikwete. 

   ZIFUATAZO NI BAADHI YA PICHA ZA SIKU YA MAZISHI 

kutoka kushoto ni Ndugu Jack Zoka, Mzee Suleiman Kikwete, Mh. Vicky Kamata na Mama mdogo wa Vicky kamata aitwaye Helena Suleiman

 Jacky Zoka ambaye ni Kaka wa Marehemu akiwa na waombolezaji wakati wa Mazishi.

Baadhi ya waombolezaji wakiwa na simanzi wakifatilia ka ukaribu mazishi


RSO wa mkoa wa Mwanza Meja Jason akiteta jambo na Mh. Vicky Kamata

Mzee Suleiman Kikwete akiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu Wakuru Mugendi

Mama mdogo wa Mh. Vicky Kamata Helena Suleiman akiweka shada la maua katika nyumba ya milele ya Dada yetu kipenzi Wakuru Mugendi. 
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.. "Ameen"

TANZIA: AJALI YAUA MTOTO WA MH. CHARLES KITWANGA, HIZI NI PICHA ZA BAADHI YA WABUNGE WAKIWA UWANJA WA NDEGE DODOMA KUELEKEA KWENYE MSIBA MWANZA.

Na Steven Mruma 'Trust' [Dodoma]
    Mbunge wa Misungwi Mh.Charles Kitwanga amepata msiba mkubwa kwa kufiwa na mwanaye wa kwanza aitwaye Vedastus Kitwanga uliotoke siku ya Jumamosi Baada ya Gari Kuacha njia na kwenda kumgonga na kupoteza maisha.
     Baadhi ya vingozi wa serikali na wajumbe wa bunge la katiba wakiongozwa na mwenyekiti wao Mh. S.Sitta walikua miongoni mwa viongozi waliokwenda kumfariji Mh. Kitwanga.

   Hizi ni baadhi ya picha wakati wakiwa uwanja wa ndege wa Dodoma kulelekea msibani Mwanza

Jopo la Viongozi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba wakiwa uwanja wa ndege wa Dodoma kulelekea Mwanza kwenye msiba wa Mh. Kitwanga
Mh. Vicky kamata pia alikua miongoni mwa viongozi walioelekea msibani Mwanza hasa ikizingatia pia yeye ni miongoni mwa wabunge wanaotokea kanda ya ziwa [Geita]
Hapa wakielekea Kupanda Ndege.

Mh Vicky Kamata akimsalimia Mh Sawel Sitta Kwa heshima zote za Kisukuma.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE "Ameen" 
R.I.P Vedastus Kitwanga GONE TOO SOON

Monday, 18 August 2014

PICHA: MAMA TUNU PINDA ALAKIWA BAADA YA KUREJEA KATIKA MTANO WA WAKE WA MAWAZIRI WA KUU AMBAPO ALITUNUKIWA TUZO YA HESHIMA KAMA BALOZI WA AMANI DUNIANI

Picha Habari na Steven Mruma "Trust"  
       Ilikua ni mapokezi ya aina yake ya kumpokea moja kati ya wanawake mashujaa ambaye ni mke wa waziri mkuu wa Tanzania mama Tunu Pinda alipokua kwenye mkutano wa dunia kuhusu mambo ya ya amani na kutunukiwa cheti cha kumtambua kama Balozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama uliomalizika hivi karibuni (Agosti 12, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini.
 
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwa na Rais wa Universal Peace Federation (UPF), Dk. Thomas Walsh (kushoto) na Mwenyekiti wa UPF, Dk. Charles Yang mara baada ya kutunukiwa cheti cha kumtambua kama Balozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama  uliofanyika Seoul Korea Kusini.
      Baada ya kutunukiwa tuzo hiyo kama balozi wa amani na usalama duniani Mama Tunu pinda aliwasili nchini na kufanyiwa mapokezi makubwa na baadhi ya viongozi wanawake pamoja na mumewe waziri mkuu wa Tanzania Mizengo K.P. Pinda.
     Miongoni mwa waliompokea alikuwepo mbunge wa Viti maalum na mpambanaji wa haki za wanawake duniani Mh. Vicky Kamata pamoja  na wanaharakati na viongozi mbalimbali wanawake.

ANGALIA PICHA ZA MAPOKEZI YAKE J.K.NYERERE INTERNATIONA AIRPORT ALIPOWASILI












GEITA DOCUMENTARY

Contributors