Mh. Vicky Kamata aliwasili Bungeni Dodoma na kama ilivyo ada
alipokewa vizuri na kila mbunge aliyekutana nae. Wabunge wengi walimpa
pole baada ya kuugua siku chache kabla ya ndoa yake na kumtakia kila la
kheri, huku wengi wakiamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kua Ndoa
yake ipo na itakuwepo siku yoyote Mungu akiamua kulitimiza kusudi lake
juu ya Mh. Vicky Kamata.. Wakati wabunge wengi
wakimuhurumia na kudhani kua kutofungwa kwa ndoa yake kungemgharimu siku
nyingi kurudi katika hali ya kawaida, ilikua ni tofauti kabisa kwa
upande wa Mh. Vicky Kamata kwani muda wote alikua na amani na kwamba
hakujiskia vibaya kama wengi walivyodhani na ndio maana ilichukua muda
mfupi sana na aliweza fika Bungeni na kazi ya kuwatumikia wananchi wake
wa Geita na Tanzania kwa ujumla ilianza mara moja na kwamba bado
anaamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kwamba Mungu hakosei na
anamini Muda si mrefu atafunga ndoa na kila mtu atashuhudia na mkono wa
Mungu utasiamama juu ya ndoa yake.
|
Mh. H. Kigwangala akiwa amemkumbatia Mh. Vicky Kamata baada ya kuingia ukumbi wa Bunge mjini Dododma |
|
Mh. Vicky Kamata akiteta jambo na baadhi ya wabunge wenzake ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma |
|
Mh Vicky Kamata akiwa amekumbatiwa na mbunge mwenzake |