Friday 28 May 2010

ROSE JOHN atwaa taji Miss Dar Inter College


Mshindi wa Shindano la Miss Dar inter College lililofanyika jana katika ukumbi wa Billcanas, Rose John (katikati) wa Chuo cha Ustawi wa Jamii akiwa mwenye tabasamu baada ya kutangazwa mshindi katika mashindano ya Miss Miss Dar inter College yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Billicanas, Dar es Salaam jana. Kulia ni mshindi wa pili, Cassian Millinga wa Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE) na Marrylidya Boniface wa Ustawi wa Jamii.

Meli


Meli ya Jeshi la Maji la Uholanzi, Johan de Witt inayofanya msako wa maharamia katika Bahari ya Hindi, ikiwa kwenye bandari ya Dar es Salaam baada ya kukabidhi vifaa mbali mbali kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) jana.

Mayaula afariki



MWANAMUZIKI mkongwe wa Jumahuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Fredy Mayaula Mayoni, amefariki dunia jana jijini
Brussels, Ubeligiji, kwa ugonjwa wa kansa ya ubongo.

Marehemu Mayaula Mayoni (64) ni mwanamuziki aliyekulia na kusomea jijini Dar wakati wa utoto wake miaka ya 60.

Mayoni, baba yake alikuwa ni mmoja
wana diplomasia katika ubalozi wa Congo (Zaire) nchini Tanzania.

Pia, marehemu aliwahi kuicheza timu Yanga ya Dar es Salaam miaka ya nyuma.

Marehemu Mayaula, atakumbukwa zaidi alipojiunga na bendi ya TP OK Jazz, iliyokuwa ikiongozwa na gwiji la muziki, Franco Luambo Makiadi nchini DRC.

Mayaula alijiunga TP OK Jazz baada ya kurudi kwao na kujihusisha zaidi na muziki na kufanikiwa kurekodi wimbo wa Cherie Bondowe au Sherry bondowe, wimbo ambao ulimpa umaarufu sana.

Mbali na TP Ok, aliwahi kufanya kazi na mwanamuziki Mpongo Love ambate pia ni marehemu.
Mungu amlaze pema peponi Mayaula Mayoni.

Thursday 27 May 2010

Egypt claims on Nile rejected


Ethiopia's prime minister has rejected a threat by Egypt to prevent the building of dams and other water projects upstream on the Nile river.

Meles Zenawi said on Wednesday that Egypt will not be able to stop his country from building dams on the river.

His comments came nearly a week after Ethiopia joined Uganda, Rwanda, Tanzania and Kenya in signing a new treaty on the equitable sharing of the Nile, despite strong opposition from Egypt and Sudan who have the major share of the river waters.

The Nile flows through 10 African nations, but the distribution of its waters among each Nile basin country has long been a source of tension in the region.

Historic agreements have given Egypt and Sudan veto power over upstream projects that could affect the flow of water.

But the agreement signed last week by four of the Nile Basin countries marked the creation of a new commission to manage the water.

Kenya, Burundi and the Democratic Republic of Congo are expected to sign within a year.

'Old-fashioned ideas'

Egypt has warned that the agreement lacks legitimacy.

But Zenawi told Al Jazeera's Andrew Simmons that Egypt's approach is out of date.
The Nile River Basin

The source of the Nile, the longest river in the world, is Lake Victoria.

Hivi hii biashara bado inaendelea???


Wafanyabiashara wa vyuma chakavu wakiendelea na biashara yao kama wanavyoonekana pichani huku wa wakiwa na lundo la nyaya ambazo haikujulikana mara moja walikozipata. Biashara imechangia uharibifu wa miundombinu mbalimbali kama kung’olewa kwa vyuma vya kingo za madaraja, mifuniko ya chemba za barabara na nyaya za umeme.

Wednesday 26 May 2010

Ray C: Mwanamuziki anayeikumbuka kazi yake ya zamani


UVUMILIVU ni kitu cha msingi sana katika maisha ya mwanadamu kila siku hasa inapotokea unataka kufanya kitu fulani ambacho baadae kinaweza kikakuletea manufaa ambayo ulikuwa umeyasubiri kwa muda mrefu.

"Kwa mfano wakati naanza fani hii ya kuimba, watu wengi sana waliongea, wengine waliniambia hujui kuimba, wengine watakuambia hili na lile ilimradi tu kunikatisha tamaa katika fani ambayo ndio kwanza nilikuwa naingia," anasema Ray C.

Uvumiliivu pia unakwenda sambamba na muenekano na usikivu, kama msanii ni lazima uwe na 'good personality' kwa watu wote ili uweze kuuza kazi zako na uweze kukubalika kwenye jamii, pia wasikilize mashabiki wako, wakubwa zako, DJs na wadau mbalimbali wa fani ya muziki," anasema Ray C.

Ushauri huo umetolewa na msanii nguli katika miondoko ya Bongo fleva nchini ambaye inasemekana ndiye msanii wa kike mwenye mvuto kushinda wote Afrika Mashariki, Rehema Chalamila, wapenzi wa muziki wake wanamtambua zaidi kwa jina Ray C.

Ray C mwenye umri wa mika 28 hivi sasa, jina lake lilianza kuvuma alipokuwa mtangazaji redioni kabla hajaamua kuingia rasmi kwenye ulimwengu wa muziki, sio tena kama DJ bali muimbaji na mwanamuziki.

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni Ray C anasema safari yake ya muziki ilianzia toka alipokuwa mdogo kwa kupenda kuwasikiliza wanamuziki mbalimbali wa enzi hizo kama Bi. Shakira (mwimbaji wa taarabu) na Remmy Ongala.

"Lakini pia nilikuwa napenda sana kusikiliza nyimbo za kihindi na pia kuangalia sinema za kihindi, nilikuwa sio msikilizaji mzuri sana wa redio kipindi hicho, nakumbuka nilichokuwa nakifanya wakati nikiangalia sinema za kihindi ni kwamba wanapofikia tu sehemu ya kucheza unajua tena movie za kihindi, kila baada ya action fulani, muziki unafuata nachukua kalamu na karatasi naandika wanachoimba kwa kiswahili," anasema.

"Ilifikia mahali ikawa mtu akiniambia niimbe wimbo fulani wa kihindi nakuimba wote lakini bila hata kuelewa maana yake, ingawa sikujua wakati huo kumbe ndio taratibu nikawa najifunza uimbaji, nadhani ndio maana hata hivi leo ukisikiliza vizuri baadhi ya nyimbo zangu utasikia zina baadhi ya vionjo au mahadhi ya kihindi hivi," anasema.

Anasema katika kila kitu ambacho mwanadamu atakihitaji kukifanya kwa ajili ya maisha yake ya baadae lazima kitakuwa na mwanzao na hata kwa upande wangu kama sio watu fulani leo hii asingekuwa msanii na ingewezekana angeishia katika fani ya utangazaji tu kama ilivyo kwa wengine ambao alianza nao kazi ya kutangaza.

"Kuna watu wawili watatu ambao walinishawishi kuingia katika muziki lakini sana ni Ruge Mutahaba ambaye wakati huo ndiye aliyekuwa meneja wangu pale Clouds FM, nakumbuka mara nyingi kila baada ya kumaliza kufanya kipindi changu redioni alikuwa akinisikia nikiimbaimba kwenye 'corridors' za pale ofisini", anasema.

"Nakumbuka akanishauri kama ninapenda kuimba na ningependa kurekodi basi nifanye mazoezi zaidi ya uimbaji, nitafute mtu aniandikie wimbo au niandike mwenyewe niingie studio kurekodi japo single moja kwanza na kisha kama itakuwa nzuri basi yeye angenisaidia kurekodi albamu nzima," anasema.

Miss Inter College kufanyika leo

Baadhi ya washiriki wa shindano la kumsaka mrembo wa Vyuo, Miss Dar Inter College wakiwa katika mazoezi jana ambapo shindano hilo linatarajiwa kufanyika leo katika Ukumbi wa Billcanas Dar es Salaam leo.

Free time night club

Mmiliki wa Free Time Grace Kamata ,akifurahi na marafiki


FREE TIME ni kiota cha raha kinachopatikana maeneo ya kona ya Segerea, mbali na burudani kama vile muziki nyama choma bia na vyote vinavyopatikana hapa,kuna ukumbi mzuri kwa ajili ya sherehe mbalimbali, pia kuna club ya usiku kwa wale wasiojali sana usinginzi siku za week end.MNAKARIBISHWA.


Monday 24 May 2010

Monetary Affairs Committee (MAC)

Magavana wa Benki kuu za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa mikutano wa Naura Spring Hotel Arusha-Tanzania tarehe 10/05/2010.Magavana hawa walikubaliana kuingia katika mchakato wa kuwa na sera moja ya fedha ambayo itaziwezesha nchi za Afrika Mashariki kuwa na sarafu moja na hatimaye kuwa na benki kuu moja.
Magavana wa Benki kuu za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakzi wa benki kuu ya Tanzania na wafanyakazi wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ilikuwa ni burudani baada ya mkutano..

GEITA DOCUMENTARY

Contributors