Wednesday 12 September 2012

WANAFUNZI CHUO CHA UANDISHI WA HABARI D'SALAAM (DSJ) WALIPOUNGANA NA WAANDISHI NCHINI KATIKA MAANDAMANO YA KULAANI MAUAJI YA MWANDISHI DAUD MWANGOSI

Wanafunzi wa Dar es Salaam School of Journalism wakiwa wamebeba ujumbe wao kulaani mauaji ya Daudi Mwangosi.Maandamano hayo yalifanyika jana mjini Dar es Salaam na katika baadhi ya mikoa nchini kote.

Tuesday 11 September 2012

WAZIRI MKUU AZINDUA MRADI WA MATREKTA KWA WAJASIRIAMALI MKOANI GEITA

 Waziri mkuu Mizengo Pinda akizindua mradi wa matrekta kwa wajasiriamali wa kata ya Katoro jimbo la Busanda katika mkoa mpya wa Geita


ZIARA YA WAZIRI MKUU MKOANI GEITA

 Waziri mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizindua Zahanati katika kata ya Senga mkoani Geita.Hafla hiyo ilifanyika jana ambapo waziri mkuu yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi
                     Pia hapakukosa kuwa na burudani ya Ngoma kwa Mhe. waziri mkuu      

Monday 10 September 2012

Nyakua Nyakitita: Mhadhiri DIT anayeokota makopo barabarani


WASWAHILI siku zote husema hujafa hujaumbika! Ukweli wa usemi huu unatimia unapomwona mtu huyu.
Ungemwona miaka 13 iliyopita ungeshangaa, lakini leo mtu aliyeitwa mstaarabu, bondia wa kutegemewa na mcheza twist wa ukweli, Nyakua Nyakitita amebadilika kweli.

Mtu ambaye alikuwa mhadhiri wa kutegemewa katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), msomi aliyebobea katika uhandisi, kazi aliyoianza katika miaka ya 1990, sasa anaishi kwa kuombaomba, kuchora ramani na mambo yasiyojulikana!

Leo hii, msomi huyo yuko katika hali ya kusikitisha ya uchafu uliokithiri, anashinda karibu na maeneo ya chuo hicho makutano ya Barabara za Morogoro na Bibi Titi Mohammed  huku akiokota makopo na takataka nyingine na mara nyingine akikusanya mawe na kuyapanga kwa kutengeneza michoro ya vitu mbalimbali ikiwamo ramani ya Tanzania na  kuandika majina ya marafiki zake.

Nini kilichomsibu hadi kufikia hapo? 
Kabla ya kupata matatizo ya akili mwalimu  na mhandisi Nyakua aliishi maisha mazuri tu ambayo kwa vijana wa sasa wanasema, ‘yalimtoa’ kwani alitembelea nchi kadhaa kwa ajili ya ziara za mafunzo au kozi ndefu na ambazo zilimpa fursa nzuri ya ‘kujirusha’.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors