Thursday, 29 August 2013

PICHA: HARUSI YA MDOGO WETU FELISTER [LIKU] ILIYOFANYIKA MWISHONI MWA MWEZI HUU,

         Mwishoni mwa mwezi huu mdogo wetu Felister a.k.a LIKU alifunda pingu za maisha na Mume wake Daudi, harusi hiyo ilihudhuliwa na watu mbambali akiwemo mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo na pia Mh, Vicky Kamata ambae ni mbunge viti maalum Geita. na Baadhi ya Maofisa mbalimbali wa Serikali na wageni kutoka ndani na nje ya nchi.
          Harusi hiyo ilianza kwa Send off iliyofanyika kijijini kwa Bibi Harusi Geita na baadae kufuatiwa na Harusi iloyofana iliofanyikia Bunda mkoani mara nyumbani kwa Bwana harusi.

                               HIZI BAADHI YA PICHA KATIKA SEND OFF

Bibi Harusi Felister [Liku]


 Bibi Harusi Mtarajiwa akiingia ukumbini kwa ajili ya Send off.


Akijiandaa kukata keki na msindikizaji wake

Mh. Vicky Kamata Dada wa Bibi Harusi akiwa mwenye furaha alijumuika katika burudani ya muziki

Mjomba wa Bibi harusi ambaye pia ni Mkuu  wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akitoa nasaha kwa binti yake.

Wazazi wa Bibi harusi[ Mama wa Bibi harusi Helena Selemani wa kwanza kulia,, mjomba wa bibi harusi na mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo, Mama Mkubwa wa bibi harusi Paulina Selemani na Mama mdogo wa Bibi harusi Veronica Selemani.
Sehemu ya wahudhuriaji wakifuatilia kwa karibu

Bibi wa Bibi harusi akimpongeza mjukuu wake.

Mh. Vicky Kamata akitoa Nasaha kwa mdogo wake Liku.


kutoka kulia ni jaji mstaafu Anthon  Bahati, Mrs. Antony Bahati ambao ni babu na bibi wa Bibi Harusi, Mr&Mrs Evarist Ndikilo ,anaeyefuata ni Naibu mkurugenzi mkuu usalama wataifa bwana Zoka ambaye ni Baba wa Bwana harusi na Mkuu usalama taifa,mkoa wa Mwanza.na. kaka wa Bwana harusi,wa kwanza kushoto mstari wa mbele.


                           HIZI NI BAADHI YA PICHA  HARUSI HIYO HUKO BUNDA MARA

Bibi harusi akielekea kanisani

Wasindikizaji wakiwa tayari kumuongoza Bibi harusi kanisani
Bwana na Bibi Harusi wakisubiri mda wa kufunga ndoa

Hapa MUNGU ANAWAUNGANISHA NA KUWA MWILI MMOJA

Taratibu nyingine za harusi zikiendelea..
Mjomba wa Bibi harusi na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo na Dada yake ambaye ni Mama Mzazi wa Bibi Harusi Helena Selemani.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo wakipongzana na naibu mkurugensi mkuu usalama wa taifa Bwana Zoka ambaye ni Baba wa Bwana Harusi na nyuma ni Mama wa bwana harusi Mrs Zoka.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo [mwenye Mic] ambae pia ni mjomba wa Bibi Harusi akitoa nasaha zake, Mama wa Bibi harusi Helena wa pili kutoka kushoto na mwisho ni Mr. and Mrs. Zoka ambao ni wazazi wa Bwana harusi.

Watoto wazuri wakiwa tayari kumsindikiza Bibi Harusi, wakiwa katika picha ya pamoja [kutoka kushoto] Glory Washington wa pili ni Anthoni Ndikilo wa tatu ni Irene Ndikilo, wa nne Jackline.

Anthoni Ndikilo na Glory Washington wakiwasindikiza Maharusi

Baadhi ya wahuduriaji akiwemo Vicky Kamata wakati wa kufunga ndoa kanisani



Kanisa ambapo ndoa hiyo ilifungwa
Hawa ni baadhi ya Ndugu wa Bibi Harusi, Wajomba, Mashemeji Na watoto wa Bibi harusi
kutoka kushoto ni Jacob kaka mkubwa wa bibi harusi, Mtoto wa Bibi Harusi Revocatus Washington, Erick Ndikilo Binamu wa Bibi harusi na Methew Masalu ambaye pia ni binamu wa Bibi harusi
kutoka kushoto ni Justa Dada wa Bibi harusi, Jacob Manyaga kaka wa Bibi harusi, Happyness Dada wa Bibi harusi na Teddy Dada wa Bibi harusi..

Monday, 26 August 2013

PICHA: HALI YA AMANI YAZIDI KUWA TETE NCHINI SYRIA,,"HALI INATISHA"

      Katik hali isiyo ya kawaida maelfu ya watu wanaendelea kupoteza maisha, huku wengine wakiambulia vilema vya maisha na wengine kuwa wakimbizi baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya,, baadhi ya picha ilionyesha maiti nyingi zikiwa zimetapakaa mtaani.
       Lakini baya zaidi ni pale vijana wadogo sana wa makadrio kati ya miaka 12 hadi 17 wakiingia nao vitani na wengine wakionekana mitaani wakiw na silaha nzito kwa ajili ya mapambano..
   HII HALI NI TETE NA MBAYA SANA NA HILI NI SWALI LA KUJIULIZA SIASA ZA KWETU NAZO ZINAKWENDA WAPI?,

     HIZI NI BAADHI YA PICHA ZIKIONESHA HALI TETE  ILIYOPO NCHINI SYRIA KWASASA.

Watoto wadogo wakiwa Vitani
Umejenga nyumba kubwa kwa gharama na miaka mingi lakini dakika moja tu inakuwa sio nyumba tena ni kifusi..

Thamani ya nymba yoote lakini vita vimeileta hapa ilipo sasa
wanajeshi watoto wakishangilia mauaji kwao ni furaha akili na damu imebadilika na kua ya wanyama

hali ikiwa tete kila kona ya syria

watoto wakiwa na bunduki ya matoy zimekua kama manati tu kwao wakijianda kuingia vitani

Watoto wasiokuwa na hatia wanaendelea kuangamia kila kukicha kisa mtu mmoja amekataa kuondoka madarakani,, inauma sana

wanajeshi wakiendelea na uharibifu na mauaji hku wakifurahia wanachokifanya

Pata picha umentuma mwano dukani njiani anakutana na rocket ronger anafariki na hasa akiwa ni mwanao wa pekee, haya yamemkuta mtu huyu ambae hakufahamika mara moja

Mahali unapoishi panapokuwa kama Jehanam hapakaliki tena unakuwa mtumwa katika nchi yako mwenyewe
wanajeshi wakishangilia ushindi wa pili kulia akionekana bado ni kijana mdogo sana

Maiti kila kona ya mji mkuu wa syria kwa mbali nchi inaonekana kuwa saafi lakini hali ya mambo sasa imekua chungu na haikaliki tena

Kila mahali ni vita tu
Milipuko ya mabomu kila kukicha, na nchi inaendelea kuharibika vibaya..

GEITA DOCUMENTARY

Contributors