Saturday 8 March 2014

NDANI YA BUNGE LA KATIBA; MENGI YAMETOKEA LAKINI KUBWA NI KUPATA KATIBA MPYA YENYE MASLAHI KWA WATANZANIA NA VIZAZI VIJAVYO.


Posted By Steven Mruma [Dodoma]
   Bunge la katiba linaendelea mjini Dodoma yapo mengi yanatokea lakini lengo kubwa ni kuhakikisha katiba ya WATANZANIA yenye maslahi kwa Mtanzania inapatikana. Wakati bunge hili maalum la katiba likiwa limekumbwa na migongano ya hapa na pale lakini wananchi wanahitaji kitu kimoja tu kifanywe na Bunge hili maalum la katiba nalo ni kutengeneza katiba itakayo jali maslahi ya Watanzania wote....
Baadhi ya wajumbe wa Bunge maalum la katiba wakiwa katika moja ya vikao vya Bunge hilo maalum l;a katiba


Mh. Vicky Kmata na Mh. Anna Mkinda wakijadili Jambo katika moja ya vikao vya bunge la katiba
Mh. Anna Makinda akisisitiza jambo kwa Mh. Vicky Kamata 

ILI KUHAKIKISHA KATIBA MPYA INAKUMBUKA HAKI ZA WASANII WAAMUA KUTINGA BUNGENI KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA.

Na Steven Mruma [Dodoma]
    BAADHI YA WASANII MBALIMBALI HAPA NCHINI WALIAMUA KUTEMBELEA BUNGE MAALUM LA KATIBA LINALOENDELEA MJINI DODOMA ILI KUHAKIKISHA BUNGE HILO LA KATIBA LINAZINGATIA NA LINAJALI HAKI ZA WASANII. WASANBII HAO PIA WALIWASISITIZA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA WASISAHAU  HAKI ZA WASANII ILI KUWEZA KUINUA MAISHA YA WASANII NA SANAA YA TAIFA LETU LA TANZANIA KWA UJUMLA.
Baadhi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa bunge maalum la katiba

Mh. Vicky Kamata Mbunge wa Viti maalum Geita ambaye pia ni msanii wa Muziki na pia mjumbe wa Bunge maalum la katiba akiwa pamoja na wasanii wenzake walipotembvelea Bunge hilo kuwasisitiza wajumbe waliopo Bunge maalum la katiba wasiwasahau wasanii na sanaa kwa ujumla.
Mh. Mshama mbunge wa jimbo la Nkenge akitafakari jambo katika bunge  maalum la katiba, Mh. Mshama pia ni mdau mkubwa sana wa sanaa hapa nchini. 

GEITA DOCUMENTARY

Contributors