Wednesday, 25 July 2012

PICHA ZA MATUKIO YA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA MNAZI MMOJA LEO !!!



Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam kuhudhuria sherehe za Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa.

Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwasili katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo kuhudhuria maadhimisho ya Kumbukumbu ya siku ya Mashujaa. Hapo akisalimiana na wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana Vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyikia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Raisi Dkt. .Jakaya Mrisho Kikwete akiweka Ngao na Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya siku ya Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Wa kwanza kutoka kushoto ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, Makanu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Raisi wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa pili wa Raisi wa Zanzibar Balozi Seif Idd, Raisi Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai, Nahodha na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq, wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo kuhudhuria sherehe za Maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa Tanzania.




Monday, 23 July 2012

BREAKING NEWS:WAZIRI HAMAD MASOUD AJIUZULU KUFUATIA AJALI YA MELI YA MV SKAGIT


Waziri wa mawasiliano na miundombinu Zanzibar Mheshimiwa Hamad Masoud – CUF amejiuzulu rasmi wadhifa huo  ili kuwajibika kisiasa baada ya tukio la ajali ya MV Skagit.
Kufuatia hatua hiyo Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein amemteua mwakilishi wa jimbo la Ziwani – CUF kushika nafasi hiyo

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI MJINI BEIJING-CHINA

 Mh. Vicky Kamata akiwa na Dr.Behnam Tai ambaye ni Director wa AUS-HS Australia,ambaye pia alikuwa ni mfanyakazi wa United Nations(UN-Habitat).Mbali na wadhifa huo Dr Behnam Tai ni Professor katika chuo cha NEW SOUTH WALES,Sydney.Na ndiye alikuwa coordinator wa ziara hii mjini Beijing

 Kutoka kushoto ni Mr. Jacob Mayalla,Mh. Vicky Kamata, Dr Behnam Tai na Mh. Suma ambaye ni mbunge wa Tabora mjini

 Mh. Vicky Kamata akiwa katika picha ya pamoja na Dr. Behnam Tai na Ms. Shirley ambaye ni mmoja wa Coordinators wa AUS-HS Beijing,China
 Mh Mfutakamba(kushoto) akiwa na kijana wake Hamisi Mfutakamba anayesomea Engineering mjini Beijing katika picha ya pamoja na Mh Vicky Kamata

GEITA DOCUMENTARY

Contributors