Friday, 8 April 2011

HOW GOOD WOMAN BE.....


A good woman is proud. She respects herself and others.

She is aware of who she is.

She neither seeks definition from the person she is with, nor does she expect them to read her mind.

She is quite capable of articulating her needs.

A good woman is hopeful. She is strong enough to make all her dreams come true.

She recognizes that her love has great value and must be reciprocated.

If her love is taken for granted, it soon disappears.

A good woman has a dash of inspiration and a dabble of endurance.

She knows that she will at times have to inspire others to reach the potential God gave them.

A good woman knows her past, understands her present and forces toward the future.

A good woman knows God. She knows that with God the world is her playground, but without God she will just be played with.

A good woman does not live in fear of the future because of her past.

Instead, she understands that her life experiences are merely lessons meant

To bring her closer to self-knowledge and unconditional self-love…

Wednesday, 6 April 2011

U TRACK YAFUNGA VIFAA VYA KUDHIBITI MWENDO KASI KWENYE MABASI KWA MAKAMPUNI 11 NCHINI

Albert Kikala Meneja wa mradi wa kampuni ya Utrack akiwaelezea waandishi wa habari leo wakati alipozungumzia mpango wa kampuni hiyo, katika kupunguza ajali za barabarani kwa mabasi ya abiria kwa kufunga vifaa maalum ambavyo vinatuma taarifa za mwenendo wa dereva anayeendesha gari hilo. 
Akizungumzia kuhusu mradi huo amesema wanatumia gharama zao kwa ajili ya kunusuru maisha ya watanzania, ili kupunguza ajali za mabasi barabarani, ameongeza kuwa yeye ameshatembelea kampuni zaidi ya 130 na kuelezea mfumo huo na faida zake kwa wamiliki wa mabasi hayo, ambapo kwa sasa ni kampuni 11 zimeshafunga kifaa hicho. 

AFRICAN TOUCH IN....KITENGE






RAIS PAUL KAGAME WA RWANDA ATUMA UJUMBE KWA RAIS JAKAYA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mjumbe maalum wa Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni Waziri wa sheria na Mwanasheria mkuu wa Rwanda Bwana Tharcisse Karugama muda mfupi baada ya mjumbe huyo kuwasilisha ujumbe kwa Rais ikulu jijini Dar es Salaam kulia ni Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Bi Fatma Ndagize (picha na Freddy Maro)

WAANDISHI WA HABARI ZA UKIMWI WAPEWA TUZO NA AJAAT

 Mwenyekiti Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za UKIMWI(AJAAT) Simon Kivamo(kulia) akifafanua jambo wakati wa sherehe za kuwapa tuzo washindi wa shindano la waandishi wa habari kuhusu kuhamasisha wanandoa na wapenzi kupima Virusi vya UKIMWI (VVU) . wengine ni Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Gooffrey Majengo(katikati) na Simon Keraryo(kushoto) 
 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Guardian Gerald Kitabu akipeana mkono Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Gooffrey Majengo baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa uandishi wa makala zinazolenga kuhamasisha wanandoa na wapenzi kupima VVU ili kupambana na UKIMWI. 

Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima Helen Ngolemera akipokea cheti cha ushiriki  kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Gooffrey Majengo ikiwa ni kutambua mchango wake wa ushiriki wa uandishi wa makala zinazolenga kuhamasisha wanandoa na wapenzi kupima VVU ili kupambana na UKIMWI. Wengine katika picha na Mwenyekiti Mtendaji wa AJAAT Simon Kivamo (wa pili kutoka kulia) na Afisa Habari wa AJAAT Perege Gumbo (wa kwanza kulia)(Picha na Vicent Tiganya wa Maelezo- Dar es Salaam)

YALIYOJIRI BUNGENI DODOMA

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiingia ndani ya ukumbi wa Bunge kuongoza kikao cha kwanza cha mkutano wa tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa ufafanuzi kwa wabunge kuhusu kanuni za uendeshaji wa shughuli za bunge mjini Dodoma 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda (kulia) akijadili jambo na Waziri Ofisi ya Rais ,Utawala Bora Mathias Chikawe ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
(PICHA NA ARON MSIGWA WA MAELEZO).

Tuesday, 5 April 2011

UZINDUZI WA NEMBO MPYA YA VODACOM TANZANIA

 Katikati ni Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Bw. Dietlof Mare kushoto ni Mwamvita Mkamba Ofisa Mtendaji Mkuu wa Masoko na Mawasiliano Vodacom Tanzania, na Kulia ni Mkurugenzi wa Radio One na ITV Joyce Mhavile wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo.

 Baadhi ya wafanyakzi mbalimbali wa Vodacom Tanzania pamoja na wadau wa kampuni hiyo, wakiwa katika uzinduzi huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania  Dietlof Mare, wakati alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni ya Vodacom ambayo ina rangi nyekundu na nyeupe, uzinduzi huo ulifanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jumapili Dar es salaam.

DR. ASHA ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS JAKAYA KIKWETE IKULU

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete,Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt.Asha Rose Migiro(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia ukimwi (UNAIDS) Michel Sidibe wakiwa katika picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amkikaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt.Asha Rose Migiro. Baadaye viongozi hao wawili walifanya mazungumzo.( Picha na Freddy Maro)

WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO MKAKATI WA TAIFA WA KINGA YA UKIMWI

 Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda kuzindua rasmi jarida lenye Mkakati wa Taifa wa Kinga ya UKIMWI (2009-2012), pamoja na Mpango Kazi kuhusu Jinsia na UKIMWI (2010-2012), katika uzinduzi uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam, Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro, na kulia ni Mkurugenzi katika Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na mapambano dhidi ya Ukimwi UNAIDS Michel Sidibe.

 Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro, zawadi ya picha ya kuchora yenye picha ya Pundamilia.

 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Dr. Asha Rose Migiro, akimtambulisha Mkurugenzi wa Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya Ukimwi (UNAIDS) Michel Sidibe, wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa taifa wa kinga ya Ukimwi.

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda pia alimkabidhi mkakati huo Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Dr. Fenela Mkuangara Waziri.

 Wakuu wa Taasisi mbalimbali na Idara za Serikali pia walihudhuria katika uzinduzi huo, wa pili kutoka kulia ni Mkurugezni wa (NIMRI) Dr. Mwelle Malecela.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro akisalimiana na akina mama viongozi mbalimbali, waliohudhuria katika uzinduzi huo.

Monday, 4 April 2011

SIMBA YANYUKWA NA TP MAZEMBE

Mabingwa watetezi wa Kombe la Klabu Bingwa barani Afrika Timu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesonga mbele baada ya kuizaba Simba ya Tanzania kwa jumla ya magoli 3 – 2 katika uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam. 

TP Mazembe imesonga mbele kwa jumla ya magoli 6-3.Katika mechi ya awali iliyochezwa katika mji wa Lubumbashi TP Mazembe iliifunga Simba jumla ya magoli 3- 1. TP Mazembe ndio iliyokuwa ya kwanza kufunga goli kunako dakika ya 19 kupitia Given Sunguluma.

Kipindi cha pili Simba ilichachamaa na kupata goli la kusawazisha kunako dakika ya 51 lakini goli hilo halikudumu kwani mshambuliaji Alain Kaluyutuka alifunga goli la pili la Mazembe katika dakika ya 64 kabla ya kufunga goli la 3 kunako dakika ya 74.

Hadi mpira unamalizika Simba 2 TP Mazembe 3. Kwa matokeo hayo Simba itakuwa imetolewa kwenye mashindano hayo.

UN- MAUAJI YA IVORY COST YANAMSHTUKO

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea mshtuko wake kufuatia taarifa za mauaji ya mamia ya watu mjini Duekoue magahribi mwa Ivory Coast.

Ban Ki Moon amemtaka Alassane Ouattarra anayetambuliwa na jamii ya kimataifa kama mshindi wa kura za Urais nchini humo, afanye uchunguzi kufuatia tetesi kuwa wafuasi wake wanahusika na mauaji hayo.
 

GEITA DOCUMENTARY

Contributors