Friday, 15 February 2013
Goldie wa BBA afariki
Aliyekuwa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa na mwanamuziki maarufu nchini Nigeria, Goldie Harvey amefariki ghafla jana kiwa hospitali baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Goldie ambaye pia alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki nguli nchini Kenya, Prezzo amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Reddington, iliyoko katika visiwa vya Victoria, jijini Lagos, Nigeria.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Times, mwanamuziki huyo aliugua ghafla muda mfupi baada ya kutua Nigeria akitokea Marekani alipoenda kushuhudia tuzo za Grammy.
Taarifa za kifo chake pia zimethibitishwa na Lebo yake ya muziki ya Kennies Music kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter.
Goldie alikuwa mshiriki wa BBA mwaka 2012 ambapo alikutana na Prezzo na kuwa na mahusiano. Hivi karibuni katika kipindi cha televisheni cha ‘Churchill Live’, Prezzo alisema uhusiano wao ulikuwa katika hatua nzuri na alikuwa akijiandaa kulipa mahari.
Thursday, 14 February 2013
Tuesday, 12 February 2013
Dr.Seif Rashid azindua huduma ya mawasiliano bure kwa wahudumu wa Afya na madaktari nchini
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Seif Rashid(katikati),Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule (kulia) Mkurugenzi wa Shirika la Switchboard Ali Block wakionesha mabango ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kuwawezesha wahudumu wa Afya na madaktari kuwasiliana kwa simu za mkononi bure,huduma hiyo inatolewa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Switchboard ili kurahisisha huduma za kiafya mahosipitalini.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Subscribe to:
Posts (Atom)