Hosni Mubarak ameamua kung'ang'ania tawi, ameongea kama vile yuko Mtwara. Hosni Mubarak anaonekana kutoelewa kinachoendelea Tahrir na kwingineko Egypt. WaMisri sasa wanaonekana kuwa hawana jinsi. Wataingia mitaani kukata mti. Kama ilivyo kawaida, ukubwa wa moto utakaowaka utaanza kupimwa baada ya swala ya Ijumaa hii leo.(Nam Mdau Maggid Mjengwa)