Na Steven Mruma [Dar es salaam]
Jana yalifanyika mahafali ya 20 ya chuo cha waandishi wa habari cha DSJ na mgeni rasmi alikua ni Mh. Vicky Kamata.Wakati akihutubia Mh. Vicky aliwaasa waandishi hao waliohitimu wazitumie kalamu zao vizuri kuijeNga na kuilinda amani ya nchi ambayo kwa kiasi kikubwa inaweza kuvurugika iwapo hawatatumia vizuri kalamu zao kwa maslahi mapana ya taifa.Katika mahafali hiyo iliyofana na ya aina yake pia iliisha kwa Mgeni Rasmi kuimba wimbo wake uliomtambulisha katka tasnia ya muziki wa wanawake na maendeleo.
Ikumbukwe kua Mh. Vicky Kamata ni pamoja kua ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Geita lakini ni mwanamuziki aliyewahi kutamba na wimbo wa wanawake na maendeleo, Mapenzi na Shule, Fitina, Nimeolewa..nk. na sasa ameingiza sokoni albamu yake mpya inayotwa MOYO WA MTU KICHAKA.
ZIFUATAZO NI BAADHI YA PICHA ZA MAHAFALI HAYO YA DSJ
SAFARI ILIANZIA NJE YA OFISI ZA VICTORIA FOUNDATION KUELEKEA CHUO CHA DSJ |
MGENI RASMI MH. VICKY KAMATA AKIWASILI CHUO CHA DSJ |
HAPA AKIMSIKILIZA MKUU WA CHUO J. RUPEPO HAYUPO PICHANI NA KULIA NI MRATIBU WA MAFUNZO DADA JOYCE MBOGO |
MGENI RASMI AKISAINI KITABU CHA WAGENI |
AKISAIDIWA KUVISHWA JOHO MAALUM NA MRATIBU WA MAFUNZO JOYCE MBOGO |
MGENI RASMI AKITOKA CHUONI KUELEKEA UKUMBI ULIOANDALIWA KWA AJILI YA MAHAFALI |
BAADA YA KUWAASILI NJE YA UKUMBI ULIOFANYIKA MAHAFALI KUTOKA KUSTOTO NI MKUU WA CHUO NDUGU JOACHIM RUPEPO, MRATIBU WA MAFUNZO DADA JOYCE MBOGO NA MGENI RASMI MH. VICKY KAMATA |
KUELEKEA UKUMBINI |
BAADA YA KUWASILI WALIPOKEWA KWA NDELEMO NA VIFIJO NA WAGENI PAMOJA NA WAHITIMU NA WANACHUO WANAOBAKI. |
WIMBO WA TAIFA UKIIMBWA |
RISALA YA WAHITIMU |
SEHEMU YA WAHITIMU WALIOHITIMU MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI |
MKUU WA CHUO NDUGU JOACHIM RUPEPO AKISOMA MUHTASARI NA HISTORIA FUPI YA CHUO CHA DSJ |
MGENI RASMI MH. VICKY KAMATA AKIHUTUBIA WAHITIMU WAGENI WAALIKWA PAMOJA NA WANACHUO WANAOBAKI. |
HOTUBA IKIENDELEA |
SEHEMU YA WAHITIMU |
WAHITIMU |
WAHITIMU WAKIWA TAYARI KUTUNUKIWA VYETI KATIKA NGAZI MBALIMBALI NA KOZI MBALIMBALI |
WAHITIMU WAKIWAPA MIKONO MEZA KUU |
WAHITIMU WALIOFANYA VIZURI KATIKA KOZI MBALIMBALI WAKIPEWA VYETI MAALUM VYA HESHIMA |
UTOAJI WA VYETI MAALUM UKIENDELEA |
MIONGONI MWA WALITUNUKIWA VYETI VYA HESHIMA NI MWANAHARAKATI KIJANA JAMES MWAKIBINGA |
MGENI RASMI MH. VICKY KAMATA AKISHUKURU BAADA YA KUPATIWA CHETI MAALUM CHA HESHIMA NA SHUKRANI. |
PICHA YA PAMOJA MEZA KUU NA WAHITIMU |
PICHA YA PAMOJA MEZA KUU NA WAKUFUNZI NA WAFANYAKAZI WA CHUO CHA DSJ |
BAADA YA KUMALIZA PICHA ZA PAMOJA HAPA MGENI RASMI MH. VICKY KAMATA AKIAGANA NA UONGOZI WA CHUO |
NA HAPA MGENI RASMI MH. VICKY KAMATA ALIKUA AKIIMBA LIVE WIMBO WA WANAWAKE NA MAENDELEO. IKUMBUKWE KUA MH. VICKY PAMOJA KUA NI MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA GEITA ILA NI MUIMBAJI MAHIRI. |
PICHA ZA PAMOJA NA MASHABIKI WAKE KABLA YA KUONDOKA ENEO LA MAHAFALI |