WAKATI Kampuni ya uratibu ya uagizaji wa mafuta kwa pamoja (PIC) ikipigiana chenga na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) kuhusu uhaba wa mafuta nchini, serikali imeagiza kusitisha kusafirisha mafuta nje ya nchi.
Agizo hilo la serikali lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliackim Maswi, alipokutana na Bodi ya PIC pamoja na Ewura mbele ya waandishi wa habari na kuwataka waeleze sababu za kuadimika kwa nishati hiyo nchini.