Ni tukio nadra sana kutokea na mara linapotokea lazima ukubali ukweli na hali halisi, zilibaki saa 36 tu kabla ya kufungwa kwa ndoa ya Mh. Vicky Kamata mbunge wa viti maalum Geita na msanii wa muziki ambaye pia amejizolea umaarufu kwa kutetea haki za wanawake.
Ilikua ni jioni ya alhamisi Mh. Vicky alianza kujiskia vibaya na kila muda uliposonga hali yake ilizidi kuwa tete na hatimaye alikimbizwa katika hospitali ya General Hospital iliyopo Tabata Segerea..
Kuugua huko kulifanya ndoa yake kuahirishwa baada ya vipimo vya daktari kudhibitisha kuwa hataweza kufunga ndoa na sababu kubwa ikiwa ni hali ya maumivu makali ya tumbo, Presha kuwa chini sana na Kutapika sana, Hayo yanatokana na ujauzito alio kuwa nao ambapo isingekua rahisi kwake kuhumili suala zima la ndoa na sherehe yake kwa ujumla kwakua ingehatarisha maisha ya mtoto aliye tumboni, kwani ujauzito huo ungeweza kuharibika na kutoka.
Daktari aliongeza pia presha yake ilikuwa chini sana na alikuwa anatapika sana jambo lililomfanya Mh. Vicky kuishiwa nguvu.
Leo asubuhi nilifika hospitali kwa mara nyingine kujua hali yake na aliweza kuongea na mimi machache na kunieleza kua hali yake imeanza kuimarika na maumivu pia yameanza kupungua na aliweza kuongea vizuri tofauti na hali ya jana ambapo alikuwa hawezi kuongea na kila alipojaribu alionekana kushindwa kuongea sababu ya maumivu makali aliyokuwa anayapata.
"
Hali yangu ni nzuri kwakweli namshukuru sana Mungu najiskia vizuri asanteni kwa maombi yenu na natumai hali yangu itaimarika na nitarejea katika hali ya kawaida muda sio mrefu" alisema Mh. Vicky huku akioneka bado anauchovu kidogo.
|
Na hii ndio Hospitali aliyolazwa Mh. Vicky Kamata |
|
Mh. Vicky Kmata akiwa amelala hii ilikuwa mara tu nilipoingia wodini alipolazwa na nilisubiri dakika kadhaa na aliweza kuamka na nikazungumza nae. |
|
Mh. Vicky Kamata akiwa amepunzika wakati nilipofika kumuangalia na kuzungumza nae juu ya hali yake. |
|
Steven Mruma [mwandishi wa habari hii] kushoto, hapa nikiongea na Mh. Vicky Kamata, ilikua ni baada ya kumuamsha na kujua hali yake ambapo aliamka na tukaanza kuzungumza machache juu ya afya yake. |
|
Hapa akinielezea hali yake kwa ujumla |
|
Baada ya Muda baadhi ya ndugu jamaa na marafiki zake nao walifika kutaka kujua hali yake na alionekana mchangamfu sana ikiashiria hali ya afya yake kuimarika . |
|
Ndugu na Marafiki waliofika kumuona hospitalini leo
|