Thursday 4 August 2011

VITUO VYA MAFUTA MBEYA VYANGOMA KUUZA MAFUTA

 Vituo vya mafuta jijini Mbeya vimegoma kuuza mafuta aina zote sababu ya kupinga hatua ya EWURA kupunguza bei ya mafuta.

 Moja ya kituo cha mafuta kilichongoma kutoa huduma

Baadhi ya madereva wakigombea kununua mafuta katika moja ya kituo

Wednesday 3 August 2011

MUBARAK KUJIBU MASHTAKA YA MAUAJI MISRI

Ulinzi mkali umedumishwa katika mji mkuu wa Misri, Cairo ambako aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak anatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Inaarifiwa kuwa maafisa wa usalama walifyatua risasi hewani katika bustani ya Tahrir Square ili kuwatawanya waandamanaji.

Mubarak ambaye aliondoka madarakani mwezi wa Februari anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi pamoja na mauaji ya mamia ya waandamanaji.
Mawakili wake wanasisitiza kuwa mteja wao ni mgonjwa sana na kuna idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo hawaamini ikiwa atafika mahakamani kujibu mashtaka dhidi yake.

VODACOM MISS TANZANIA KUINGIA KAMBINI AGOSTI 8

Lino Internation Agency chini ya Mkurugenzi wao Hashim Lundenga ambao ni waandaji wa shindano lenye hadhi ya kimataifa la urembo la Vodacom Miss Tanzania wametangaza rasmi jumla ya warembo thelathini (30) waliofanikiwa kupata nafasi ya kushiriki katika shindano la Urembo la Vodacom Miss Tanzania 2011.
 
Warembo hawa wamepatikana baada ya kupitia ngazi mbali mbali za Mashindano ya Vodacom Miss Tanzania katika ngazi za chini, ikiwa ni pamoja na Vitongoji, Wilaya na Mikoa, na hatimaye ngazi ya Kanda, Jumla ya Kanda kumi na moja (11) zilishirikishwa katika Mashindano haya, Lundenga alisema kambi ya shindano hili la "Vodacom Miss Tanzania 2011" inategemea kuanza siku ya Jumatatu ya tarehe 8 / 8 / 2011 jijini Dares Salaam.

MAONYESHO YA NANENANE DODOMA

 Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha Eva Varelian (kushoto) na Alice Kihiyo (kulia) wakimhudumia mteja  wakati wa maonyesho ya nane nane yanayoendelea mjini Dodoma
  Afisa Mfuko wa Hiari wa Kujiwekea akiba uzeeni (GEPF) Aziza Selemani akitoa ufafanuzi kwa mwananchi aliyetembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nane nane leo mjini Dodoma.
 Afisa Uhisiano wa Mfuko wa Penseni wa PPF Edward Kyungu akitoa maelezo
kwa mwananchi katika banda la Wizara ya Fedha juu ya muhimu wa mfuko huo katika maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayoendelea mjini Dodoma .
 Onni Sigara(katikati) na Adamu Msumule(kushoto) wakati wa maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayoendelea mjini Dodoma.
 Afisa katika kitengo cha bajeti cha Wizara ya Fedha Adamu Msumule akitoa maelezo juu ya vipaumbele vya bajeti ya mwaka huu katika maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayoendelea mjini Dodoma

ANNA LUKINDO ATINGISHA JIJINI LONDON

 Model akiwa mzingoni
 Mojawapo ya design tofauti
 Model ndani ya kivazi
 Jestina kionyesha mitindo ya mavazi
 Mavazi ya Anna yalikuwa kivutio kikubwa
 Maonyesho ya mavazi yakiendelea
 Model ndani ya vazi la Anna
 Model ndani ya kivazi cha Anna
 MC akitoa matangazo
 Kutoka Kushoto ni Mariam Kilumanga, Jestina George, Anna Shelukindo na mdau wakiwa katika pozi
 Ma model wa Anna katika pozi
Mama Balozi na staff wa Ubalozi nao walikuwepo kumsupport Mtanzania mwenzao
 Model Tina,Anna,Tammy, Zulfa na rafiki wa Anna

Mtanzania mbunifu wa  mitindo ya nguo Anna Lukindo ametikisa ulimwengu wa fashion jijini london wikiendi  iliopita. Anna alionyesha mavazi aliyobuni kwenye maonyesho ya  La Geneve North Event,  yaliyofanyika London. Ubunifu wa Anna ulipokelewa kwa vifijo na nderemo kwani ulikuwa ndio uliotia fora. 

Kulikuwa na wabunifu wengine kumi lakini Anna ndio alikuwa mwafrika na Mtanzania pekee ambaye Mavazi yake yalikubalika na kupendwa na watu wengi zaidi.

 Mojawapo ya wageni na wadau mbalimbali walijjitokeza kumpa sapoti Anna ni  Mh Balozi wetu  Peter Kallaghe na Mama Balozi, Naibu Balozi Chabaka Kilumanga pamoja na watanzania wengine.

Kwa niaba ya URBAN PULSE Tunapenda Kumpongeza Dada yetu Anna Na Kumtakia  kila la kheri pamoja na Mafaniko Mema.


GEITA DOCUMENTARY

Contributors