Akikabidhi baiskeli hizo katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Abdullahaman Kinana alisema ni wakati sasa akina mama na viongozi wa UWT waliopata baiskeli hizo wazitumie katika shughuli mbalimbali za kuwafikia wananchi na kuwasaidia kutatua matatizo yao pamoja na kazi ya kujenga chama.
Nae Vicky Kamata alipokua akizungumza alishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta kumwagia sifa kemkem katibu mkuu huyo wa CCM kwa kujitoa kwa dhati kabisa kukipigania chama,, "Natoa Baiskeli hizi kwa viongozi wote wa UWT mkoa wa Geita kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na katibu mkuu, ninatoa pongezi za dhati kabisa kwani kulingana na nafasi yake angeweza kwenda nchi mbalimbali kula bata lakini aliacha yote ameacha familia yake anazunguka Tanzania nzima jua lake, joto lake, mvua yake, baridi yake lakini hajali" alisisitiza Mh Vicky alipokua akiongea kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika viwanja vya Nyankumbu Geita.