Wednesday 16 October 2013

HAPA NI KATIKA MJI WA KAWASAKI MTAA HUU UNAITWA KAMATA NCHINI JAPAN, AMBAPO WAHESHIMIWA WABUNGE WA KAMATI YA UCHUMI VIWANDA NA BIASHARA WALIPOKARIBISHWA CHAKULA CHA USIKU KWA RAFIKI YAO.

   Kama ulikuwa hujui Chukua hii, nchini Japan kuna mtaa unaitwa KAMATA, ni katika mji wa kawasaki ambapo waheshimiwa wabunge wa kamati ya uchumi wa viwanda na biashara na viongozi kutoka TBS walipata fursa ya kuutembelea walipokaribishwa chakula cha usiku na rafiki yao Mr. Jans. Si hilo tuu bali pia walipata fursa ya kula chakula kwa kutumia vijiko vya DHAHABU.

     Mara baada ya kumaliza kusomewa Taarifa Kutoka Kampuni ya East Afrika Auto Mobile Co,. LTD kutoka kwa Director wa kampuni hiyo Bwana Prosper Japhet waheshimiwa wabunge wa kamati ya Uchumi Viwanda na bishara Pamoja na Viongozi kutoka TBS walikaribishwa nyumbani kwa Bwana Jans ambaye ni rafiki wa karibu wa Bwana Prosper Japhet.
     Bwana Jans Pia ni Director wa Kampuni ya Ukaguzi wa magari [ Pioneer of pre-export inspection] wa Kampuni iitwayo Jans Company LTD. ambayo inafanya kazi ya ukaguzi wa magari yanayoenda zaidi nchini Kenya.

Mh. Vicky Kamata [Kushoto] akipata chakula cha usiku kwa kutumia vijiko vya dhahabu.. kulia ni M/kiti mpya wa bodi ya wakurugenziz TBS.

Mh. Vicky Kamata akiwa mwenye furaha wakati wa chakula cha usiku walichkaribishwa na Bwana Jans.

Wakipata chakula kwa kutumia vijiko vya dhahabu Kutoka kulia ni Mr. Jans ambaye ndiye aliyewakaribisha chakula cha usiku anayefuata ni Dada Betty mkaguzi kutoka TBS na Kushoto ni Mr. Luiza ambaye pia ni mkaguzi kutoka TBS.
Mh. Hatibu Haji akipata chakula kwa kutumia vijiko vya dhahabu.. kushoto ni Bwana Jans.

Mh. Haribu  Haji akiendelea kupata chakula kwa kutumia vijiko vya dhahabu.

 Huduma ya chakula ikiendelea

PICHA BAADA YA CHAKULA CHA USIKU NYUMBANI KWA MR. JANS

Mh. Vicky Kamata akiwa na Mr. Jans na Mke wa Mr. Jans[Kulia]
Mr. Jans [kushoto] Mh. Hatibu Haji [katikati]i na Mkwe  wa Mr. Jans[kulia]

WAHESHIMIWA WABUNGE WA KAMATI YA UCHUMI VIWANDA NA BIASARA WALIPOSOMEWA TAARIFA KUTOKA KAMPUNI YA EAST AFRICA AUTO MOBILE CO., LTD. KATIKA ZIARA YAO NCHINI JAPAN

Waheshimiwa Wabunge  wa kamati ua uchumi viwanda na biashara na Viongozi kutoka TBS,  wakisomewa taarifa na Director wa Kampuni ya East Africa  Auto Mobile Services Co,. LTD na Bwana Prosper Japhet ambaye ni Mtanzania anayeyefanya kazi ya ukaguzi wa magari kabla hayajafika nchini [Pioneer of pre - export inspection]  kutoka Shirika la Viwango Tanzania TBS.

Waheshimiwa wabunge na Viongozi wa TBS wakisikiliza kwa makini taarifa kutoka kwa Director wa East Afrika Auto Mobile Co,. LTD Bwana Prosper Japhet.
Waheshiwa wabunge na viongozi kutoka TBS wakijadiliana jambo mara baada ya kusomewa taarifa kutoka Kampuni ya Ukaguzi wa magari ya East Africa Auto Mobile Co,. LTD. katika ziara yao nchini Japan,

Tuesday 15 October 2013

PICHA: RAIS JAKAYA M. KIKWETE ALIPOKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI IKULU KUJADILI MUSWADA WA KATIBA.



MKUTANO kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi Bungeni umemalizika Ikulu, Dar Es Salaam kwa pande hizo mbili kukubaliana Yafuatayo:-
      Kwanza. Vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka Serikalini ili itafutwe namna ya kuyashirikisha mapendekezo hayo katika marekebisho ya Sheria hiyo.
       Pili, kwamba vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa Katiba Mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano wa jinsi kwa pamoja vitakavyosukuma mbele mchakato huo kwa maslahi mapana ya nchi yao na mustakabali wa taifa. 
     Viongozi wa vyama vyama vya siasa waliokutana na Mheshimiwa Rais Kikwete ni Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF; Mheshimiwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA na Mheshimiwa James Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.
      Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Mheshimiwa Philip Mangula, Mheshimiwa Isaack Cheyo ambaye amemwakilisha Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mheshimiwa John Cheyo na Mheshimiwa Nancy Mrikaria ambaye amemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mheshimiwa Augustine Mrema. Waheshimiwa John Cheyo na Mrema wako nje ya nchi.

Wengine ambao wameambatana na wenyeviti wao ni Mheshimiwa H. Mnyaa na Bwana Julius Mtatiro wa CUF, Waheshimiwa Tundu Lissu na John Mnyika wa CHADEMA na Bwana Martin Mng’ongo wa NCCR-Mageuzi.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mh. Tundu Lisu

Rais Kikwete akisalimiana na Mh. John Mnyika

Rais Kikwete akijadiliana na Viongozi wa vyama vya siasa.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Vyama vya upinzani na wasaidizi wao waandamizi muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu rasimu ya katika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kutoka kushoto mbele Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba CUF, Freeman Mbowe CHADEMA, Philip Mangula CCM, na Bibi Nancy Mrikaria aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mhe.Agustine Lyatonga Mrema.Waliosimama Nyuma kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu CUF Bwana Julius Mtatiro,Mhe. Tundu Lissu CHADEMA, Bwana Martin Mng’ong’o NCCR Mageuzi ,Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge William Lukuvi, Mhe.Habib Mnyaa CUF, Mbunge wa Ubungo Kwa tiketi ya CHADEMA Mhe.John Mnyika, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Mhe.Steven Wassira na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Mathias Chikawe

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Vyama vya upinzani muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu rasimu ya katiba ikulu jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba CUF, Freeman Mbowe CHADEMA, Philip Mangula CCM, na Bibi Nancy Mrikaria aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mh. Agustine Mrema.

Rais Kikwete akisalimiana na m/kiti wa CHADEMA Freeman Mbowe. Nuyama ni M/kiti wa NCCR - Mageuzi James Mbatia kushoto na Prof. Ibrahim Lipumba ambaye ni M/kiti wa CUF [Kulia]
. (picha na Freddy Maro).

PICHA: KILELE CHA MBIO ZA MWENGE PAMOJA NA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE MKOANI IRINGA.

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwasili uwanja wa CCM Samora mjini Iringa huku akishangiliwa na umati wa watu waliohudhuria kilele cha mbio za mwenge na kumbukumbu ya Mwl. Nyerere yaliyofanyika kitaifa Mjini Iringa.
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa CCM Samora

Madereva wa Bodaboda na Bajaj hawakuwa nyma kumuenzi Mwl Nyerere.
Mabalozi wa nchi mbalimbali wakifuatilia kwa ukaribu Kilele cha mbio za mwenge na Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere
Mabalozi wa nchi mbalimbali.
Viongozi wa madhehebu ya Dini zote pia walihudhuria kuonyesha mshikamano na umoja wa Watanzania bila kujali itikadi zao za Kidini..

Watoto wa halaiki wakitoa burudani ya aina yake
Makamanda waliokuwa viongozi wa mbio za mwenge wakionyesha ukakamavu wa hali ya juu.
Rais Kikwete akipita karibu na bango lenye kauli mbiu ya Maadhimisho ya kumbukumbu ya Mwl. Nyerer na kilele cha mbio za mwenge
Rais Kikwete akihutubia wananchi

Hotuba ya Rais Kikwete ikiendelea
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Bwana Juma Ali Simai akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Rais Jakaya Kikwete

Rais Kikwete akiwa na makamanda waliokimbiza Mwenge nchi nzima.


Rais Kikwete akiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikalia na viongozi wa Dini

 Picha na viongozi wa taasisi mbalimbali waliofaniisha sherehe hizi

Rasi Kikwete akiwapongeza Watoto wa halaiki.
Picha na walimu wa Halaiki

GEITA DOCUMENTARY

Contributors