Wednesday 24 September 2014

KUTOKA MAISHA MAPYA YALIYODHANIWA KUA YANGEKUA YA FURAHA DUNIANI LAKINI MUNGU ALIMPENDA ZAIDI AKAWE NA FURAHA MBINGUNI.. R.I.P. ESTER.

Na Steven Mruma "Trust"
    Mwishoni mwa mwezi wa August 28/29, niliandika makala ikizungumzia mtoto aitwaye Ester aliyekua anaugua kansa na kupelekea kukatwa mguu wake..
    Pamoja na kufanikiwa kupunguza makali ya kansa lakini tulishachelewa kansa ilimuathiri sana na kusababisha hitilafu katika mapafu yake hali iliyopelekea kufariki dunia mnamo tarehe 18/09/2014 na kuzikwa tar 20/09/2014 jijini Dar es salam.
  
Pamoja na kupitia maisha ya maumivu kwa takribani miaka miwili baada ya kukutana na Victoria foundation Ester na familia ikiwemo watendaji wa Victoria foundation tuliamini kama Ester angepona na kuishi tena maisha ya furaha, japo haikua hivyo tunaamini ilikuwa ni mpango wa MUNGU hadi hapo hitimisho la Ester lilipotimia, yaani mauti yake.
    sipendi kulizungumzia sana hasa kutokana na makala niliyowahi kuandika katika Blog hii mwishoni mwa mwezi wa August.

 Tumia muda mchache kuangalia picha za tukio la mazishi yake yaliyofanyika jijini Dar es salam wikend iliyopita.   

MWILI WA MAREHEMU UKITOLEWA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI HOSPITALI YA AMANA

MWILI UKIPANDISHWA KWENYE GARI KUELEKEA NYUMBANI KWA AJILI YA MAZISHI

MWILI WA ESTER UKIWA NYUMBANI TAYARI KWA KUAGWA

MTUMISHI WA MUNGU AKIONGOZA MISA YA KUMUAGA MAREHEMU ESTER

MWILI WA ESTER UKIAGWA NA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI

ILIKUA NI VILIO NA SIMANZI NA WENGINE WALIDHIRAI MARA BAADA YA KUONA MWILI WA MAREHEMU ESTER
DEOGRATIAUS MOJA KATI YA VIONGOZI WA VICTORIA FOUNDATION AKIAGA MWILI WA MAREHEMU

STEVEN MRUMA MWANDISHI WA MAKALA HII NA MAKALA  MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA VICTORIA FOUNDATION AKIAGA MWILI WA MAREHEMU.

ALPHA MOJA KATI YA VIONGOZI WA JUU WA VICTORIA FOUNDATION AKIAGA MWILI WA MAREHEMU ESTER
NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WAKIAGA MWILI WA MAREHEMU

MWILI WA MAREHEMU ESTER UKIPANDISHWA KWENYE GARI KUELEKEA MAKABURINI KWA AJILI YA MAZISHI

MWILI WA ESTER UKIWA MAENEO YA MAKABURINI NA HAPA NDIPO ALIPOLALA KATIKA NYUMBA YA MILELE.

MWILI WA ESTER UKIWEKWA KABURINI

MWILI WA ESTER UKIFUKIWA[UKIZIKWA] KABURINI



WAWAKILISHI WA VICTORIA FOUNDATION STEVEN MRUMA NA ALPHA WAKIONGOZWA NA MAMA MDOGO WA MAREHEMU KUWEKA SHADA LA MAUA KATKA KABURI ALILOLALA ESTER   


MWAKILISHI WA VICTORIA FOUNDATION STEVEN MRUMA BAADA YA KUTOA SHUKRANI ZAKE MARA BAADA YA MAZISHI

BAADHI YA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WALIOKUJA KUMSINDIKIZA ESTER KATIKA SAFARI YAKE YA MWISHO.

NA HAPA NDIPO SAFARI YA MWISHO YA DUNUANI YA ESTER ILIPOISHIA BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.. "Ameen"

GEITA DOCUMENTARY

Contributors