Thursday 25 October 2012

NSSF YAZITAKA Manchester United, Chelsea,Real Madrid



SHIRIKA la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeanzisha mchakato wa kujenga kituo cha kuibua vipaji vya soka nchini kwa kutumia jina la klabu mojawapo kubwa ya barani Ulaya.

Mkurungenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau, aliiambia Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), jana kwamba, kwa sasa wapo katika mazungumzo na timu kubwa za Real Madrid ya Hispania, Manchester United, Liverpool na Chelsea za England.

Wednesday 24 October 2012

NDEGE YA JESHI YAANGUKA, MMOJA APOTEZA MAISHA


MWANAJESHI mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya ndege ya mafunzo waliyokuwa wamepanda maofisa wa Jeshi la Wananchi nchini (JWTZ) kupoteza mwelekeo na kuanguka katika eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa Jeshi hilo, Kanali Kapambala Mgawe, alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa haijaruka, lakini maelezo yake yameonekana kujichanganya.

Alisema wakati ndege hiyo ikijiandaa kuruka ikiwa na maofisa wa mafunzo wawili, ilipoteza mwelekeo na kuserereka na kuelekea ndani kwenye hanga kitendo kilichowafanya waamue kujinusuru maisha yao.

“Ndani ya hanga hilo kulikuwa na ndege nyingine mbili, lakini hata hivyo tunashukuru hakuna madhara yaliyotokea, kila kitu kiko salama,” alisema Kanali Mgawe.

Alisema wanajeshi hao, kila mmoja aliamua kuchumpa kwa mwamvuli ambapo Kapteni Magushi alianguka juu ya paa la jengo lililokuwa karibu na eneo hilo ndipo alipopoteza maisha.

Alimtaja mwanajeshi aliyenusurika katika tukio hilo, kuwa ni Kapteni Kwidika, ambaye amekimbizwa katika hospitali ya kijeshi Lugalo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Wanajeshi hao walikuwa katika shughuli zao za mafunzo ya kawaida.

Tuesday 23 October 2012

WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE WALIPOKAGUA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI



Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge maendeleo ya jamii wakiwa katika ziara ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es salaam,wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi msimamizi kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Karim Mattaka. Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge Mh.Jenista Mhagama,na kulia kwake ni Mkurugenzi mkuu wa NSSF Dkt. Ramadhani Dau. Wakati kamati hiyo ilipo tembelea na kukagua mradi huo tarehe 18 - Oktoba - 2012

CHANZO CHA WATOTO WA MITAANI NI...


ASASI ya Woman and Children Group wilayani Kilombero imebaini ongezeko la watoto mitaani wanaoishi katika mazingira magumu wilayani humo ambalo limechochewa na matatizo mbalimbali ikiwemo uporaji wa mali za marehemu.
Akizungumza katika mafunzo ya siku 10 yaliyotolewa kwa wazazi, walezi, wajumbe wa kamati za shule na viongozi wa serikali kuanzia vitongoji hadi kata yaliyoandaliwa na asasi hiyo kwa ushirikiano na ‘Foundation for Civil Society’ katika kata ya Kibaoni na Mikelo wilayani humo.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors