Friday 28 December 2012

UJIO WA TEKNOLOJIA YA DIJITALI UTAWAKOMBOA WASANII?


KUMEKUWA na hofu miongoni mwa wasanii na Watanzania wengine kuhusu ujio wa mpango wa dijitali kwamba ni nani atasalimika.
Wasanii ninyi mtakuwa wa kwanza kusalimika kwani hivi sasa mtaweza kuuza kazi zenu bila masharti kuwa lazima sura za fulani na fulani ziwepo.
Bila shaka mfumo huu wa dijitali sasa utakuwa mkombozi na mwarobaini kwa wacheza filamu nchini.
Ni kweli utakuwa mkombozi kwa sababu kuu moja tu, kwani hivi sasa msanii/ kikundi cha wasanii kinaweza kujikusanya na kuamua kucheza filamu ya hadithi watakayotunga na kukubaliana bila kujali ndani ya filamu hiyo msanii gani mwenye jina kubwa amecheza na wataweza kuiuza katika luninga na kujipatia mkate wao wa kila siku.
Kwakuwa Tanzania inatarajiwa kuingia katika idadi ya nchi ambazo zitakuwa zimetekeleza kwa vitendo maazimio ya Tume ya Kimataifa ya Mawasiliano ( ITU), kwa kuchukua uamuzi wa kutoka katika mfumo wa utangazaji wa analojia na kuingia katika mfumo wa dijitali, ukoloni wa filamu kuuzika ama kuchezwa na wasanii /msanii nyota sasa utakufa kwa kufuatia mfumo huu wa dijitali.

Friday 21 December 2012

SERIKALI IGUSWE NA HALI YA SAJUKI



MSANII maarufu wa filamu nchini, Sadick Kilowoko ‘Sajuki’, kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya hadi kupelekwa nchini India kwa matibabu.
Baada ya matibabu ya muda mrefu, msanii huyo alirejea nchini akiwa amepata nafuu kubwa tofauti na wakati anakwenda hivyo akawashukuru wote waliofanikisha gharama za safari yake.
Lakini pamoja na kurejea nchini akiwa amepata nafuu kubwa, bado akatakiwa kurejea India kwa uchunguzi na matibabu zaidi, kitu ambacho pia kinahitaji gharama kubwa ya fedha.
Kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu (Dennis Sweya), Sajuki anahitaji kiasi cha shilingi mil. 28, ikiwa ni gharama za kwenda na matibabu nchini India.
Zimebaki shilingi mil. 21 kupata kiasi cha fedha kinachohitajika kwa ajili ya msanii huyo kwenda India kwa matibabu zaidi katika kupigania uhai wake.

Wednesday 19 December 2012

ANASWA NA NDUMBA MAHAKAMANI


Mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la RAJAB ZUBERI (30), mkazi wa Kerege, Muheza, Tanga, akiwa chini ya ulinzi wa Wanausalama  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam, baada kifaa cha upekuzi kumnasa mganga huyo akiwa na vifaa vyake vya uganga ambavyo alikuwa amekuja navyo mahakamani hapo kwa ajili ya kufanyia mambo ya kishirikina katika kesi moja inayomkabili  mmoja wa washtakiwa mahakamani hapo. 

KUKAMATWA KWA MWIZI MKUU WA MAGARI NA VIFAA VYA MAGARI

 Rama Jangiri ambaye ndiye kiongozi wa genge la waiba vifaa vya magari jijini Dar.


Hili ndiyo tukio halisi la kukamatwa kwa Rama Jangiri akiwa kwenye hotel ya Farway baada ya kufuatiliwa kupitia mtandao kufuatia tukio la wizi wa vifaa vya gari na pia Compyuta na simu kutoka kwenye gari la mmoja wa wakazi wa jiji la Dar ambalo sasa wamiliki wa magari wamekuwa na wasiwasi mkubwa kila wanapokuwa wamepaki magari yao kufuatia kushamirikwa wizi wa vifaa mbalimbali uliokuwa ukifadhiliwa na bwana Rama na kundi lake.
Rama Jangiri akifikishwa kwenye kituo cha Polisi Mbezi Juu mara baada ya kukamatwa.
 
 
 
 
Picha na teentz 

 


Sunday 16 December 2012

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU AMINA SINGO MAHALA PEMA PEPONI

Aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha utangazaji cha TIMES FM  Amina Singo afariki dunia. Amina alikuwa akitangaza kipindi cha Afro Vibes kinachorushwa na kituo hicho.
 
 
                    "Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,Amen"

Tuesday 11 December 2012

MR DENNIS KINABO NA MR MASOUD KOVA WALIPOTEMBELEA OFISI ZA VICTORIA FOUNDATION LEO

C.E.O wa Victoria Foundation Mh. Vicky Kamata 

C.E.O wa Victoria Foundation akiwa katika picha ya pamoja na Mr Masoud Kova na Dennis Kinabo

USIKU WA UHURU IKULU 9th DECEMBER



Mh Vicky Kamata akiwa na balozi wa Marekani nchini Mr. Alfonso E. Lenhardt




RAY C AMSHUKURU RAIS KIKWETE KWA MSAADA WA MATIBABU

 Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.Rehema aliyefuatana na Ma
ma yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.Kwa apande wake ,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwaajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.


Sunday 9 December 2012

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dk.Jakaya Kikwete akiwasili katika gari maalum la Kijeshi na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara 2012 yanayofanyika kila mwaka Desemba 9, Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho hayo huku akisindikizwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadik.


 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho hayo

Kikosi cha ardhini Jeshi la wananchi la Tanzania JWTZ kipita kwa gwaride la heshima mbele ya Rais Dk. Jakaya Kikwete

Kikosi cha wanaanga Jeshi la wananchi JWTZ kikitoa heshima kwa gwaride kali mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete




Friday 7 December 2012

BREAKING NEWS:Japan earthquake tsunami warning issued


A tsunami warning has been issued after a 7.3 magnitude earthquake struck off Japan's eastern coast.
The epicentre of the quake was about 245km (150 miles) south-east of Kamiashi at a depth of about 36km, the US Geological Survey said.

The quake was felt in the capital Tokyo, media report.
The tsunami warning was issued for the coast of Miyagi Prefecture, which was hit by a devastating earthquake and tsunami in March 2011.

MFUMUKO WA BEI MSIMU WA KRISMAS


WAKATI watu mbalimbali wakielekea mwisho wa mwaka katika msimu wa Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya, imegundulika kuwapo kwa uwezekano wa bei za bidhaa mbalimbali kupanda.
Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa habari hii katika baadhi ya maeneo ya jijini, umebaini kuwa baadhi yao wameanza kupandisha bei kwa bidhaa mbalimbali.
Katika Soko Kuu la Karikoo, bei za vyakula kama mchele na unga imepanda sanjari na maeneo mengine ya jiji.
Mchele kwa sasa umeanza kupanda kutoka Sh2,000 hadi Sh2,800 wakati katika baadhi ya maduka ya Supermarket umefikia Sh3,200.Bei ya unga wa mahindi imepanda kutoka Sh25,000 hadi Sh29,000 na pia bei hiyo pamoja na mchele inaweza kupanda zaidi.

Monday 3 December 2012

AJIRA AJIRA AJIRA


RESEARCH ASSISTANT (RA).     
Qualifications: Must be a holder of Bachelor’s Degree with a bias / major in any of the following
disciplines:Economics ,Industrial Economics,Development Economics,International Trade,Regional Intergration , and industrialization management
Apply: The Secretary General, East African Community ,Box 1096, Arusha Tanzania e-mail;eac@eachq.org
Details: Daily News ,Nov  19, 2012
Deadline: December 10, 2012
SENIOR CONFERENCE OFFICER.     
Qualifications: www.eac.intlink’vaczncies’
Apply: The Secretary General, East African Community ,
Box 1096, Arusha Tanzania
Details: Daily News ,Nov  19, 2012
Deadline: December 7, 2012

Friday 30 November 2012

CATHERINE FOUNDATION YAZINDULIWA JIJINI ARUSHA LEO


Mbunge wa Viti Maalum -CCM,Mh. Catherine Magige akiwa na baadhi ya wadau wakati wakibadilishana mawazo kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa Catherine Foundation kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mapema leo Asubuhi.Pamoja na Uzinduzi huo wa Catherine Foundation pia iliweza kutoa msaada wa baskeli kwa walemavu wa wilaya ya Arusha.


Mbunge wa Viti Maalum,Umoja wa Vijana CCM,Mh. Catherine Maggige akisoma taarifa ya Foundation yake ilivyoanza kazi mbele ya Mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Mh. John Mongela na kuhudhuriwa na Wananchi mbalimbali wa jijini Arusha leo.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Mh. John Mongela (kushoto) na Mbunge wa Viti Maalum,Umoja wa Vijana CCM,Mh. Catherine Maggige wakisukuma Baiskeli za walemavu wakati wa kukabidhi Baiskeli hizo kwa walemavu watatu kwa niaba ya walemavu 20 waliopewa Msaada huo.


Picha na Ahmed Mahmoud

Sleeping with the fish: Dubai unveils hotel with rooms 10m under surface of the sea


 When it comes to outlandish new design ideas, Dubai is certainly ahead of the curve.
The glittering emirate has already got the tallest building in the world, the Burj Khalifa, and even the Earth itself - in the form of dozens of man-mad islands just off its coastline.
So it is no surprise to hear that architects are set to take on a new challenge - building a half-submerged hotel, complete with underwater rooms offering views of life below the surface of the sea.

 'Today, the advent of new technology made the heart of the ocean a setting not only for diving, but also for luxurious holidays,' said a spokesperson for BIG InvestConsult, a Swiss company behind the development.

The hotel will be made up of two main discs, one above water and one below, they will be connected by three 'legs' which contain lifts and stairways to plunge guests from the sunshine above down beneath the surface of the sea.
Room with a view: Special lighting will allow guests to enjoy the flora and fauna outside their window and macro photography will help them zoom in on even the tiniest creatures
The underwater section is located up to 10 metres deep and is composed of 21 hotel rooms adjacent to the submerged dive centre and a bar.

A special lighting system will illuminate the flora and fauna outside and the highest technology in the rooms will allow guests to zoom in and take a closer look at even the tiniest creatures using macro photography.

But nervous swimmers need not worry, they won't be left all at sea, DOT insists it has kept to the highest safety requirements.



KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI



KESHO Desemba mosi ni Siku ya Maadhimisho ya Ukimwi Duniani.
Hivyo basi kwa kuwa ni miaka kadhaa sasa tangu maadhimisho hayo yaanze kufanyika ni wajibu wa kila mmoja kuamua kwa dhati kuadhimisha siku hii.
Pia yatupasa kuwakumbuka ndugu jamaa na marafiki wetu ambao wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huu wa upungufu wa kinga mwilini.

Monday 26 November 2012

BREAKING NEWS: SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA


HABARI ZISIZOTHIBITISHWA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE: Msanii mahiri wa uchekeshaji na mwanamuziki wa Bongo Fleva Sharo Millionea amefariki katika ajali ya gari huko Muheza mkoani Tanga. Tutaendelea kuwajulisha kadiri tutakavyopata habari zaidi.

ALICHOKISEMA KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA
Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”
Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.
Kwenye gari alikua mwenyewe. 

Wednesday 21 November 2012

ASKARI WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA



HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa askari wawili wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mmoja wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kumuua kwa kusudia, Swetu Fundikira.
Askari hao MT 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa JKT, Kikosi cha Mbweni, MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ, Kikosi cha Kunduchi na MT 85067 Koplo Mohamed Rashid wa JKT Mbweni.

Monday 19 November 2012

HUAWEI YAZINDUA MPANGO WA TEKNOHAMA KATIKA SEKTA YA ELIMU NCHINI



 
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mpango kabambe wa Teknohama katika Sekta ya Elimu nchini uliofadhiliwa na Kampuni ya HUAWEI kutoka China leo.
Katika Mradi huo wa Teknohama itayowezesha Watanzania mbalimbali kutoka shule za Sekondari na Vyuoni kupata vifaa na mafunzo ya Sayansi na Teknolojia ili kusukuma mbele maendeleo katika nyanja za Uchumi na Kijamii.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUAWEI kutoka China Bw. Bruce Zhang akizungumza katika hafla hiyo kwamba Mpango huu unaoitwa "Huawei ICT Star" itasaidia katika shule za Primary na Sekondari katika kusukuma mbele maendeleo ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania.
Alisema katika Program hii itasaidia kuboresha miundo mbinu katika Sanyansi na Teknolojia ili kutoa mwamko kwa vijana wa Kitanzania kujifunza masomo ya Sayansi na Teknolojia. 
Balozi wa China nchini Tanzania Mh. LU YOUQING akitoa maelezo yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa Teknohama katika shule na vyuo nchini Tanzania.
Balozi alisema mpango huu ni mwendelezo wa uhusiano mwema kati ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa China katika nyanja mbalimbali za biashara uchumi na Kijamii.
Aliongeza kwamba Serikali ya China itaendelea na mikakati yake ya kusaidia nchi ya Tanzania ili kuweza kufikia malengo ya Milenia ya 2015. 
Mgeni rasmi Mh. Mbarawa na Balozi wa China wakizindua rasmi mpango wa "HUAWEI ICT STAR" nchini Tanzania. 
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI Bw. Bruce Zhang wakitiliana saini kitabu cha makubaliano rasmi ya Ushirikiano katika Sekta ya Sayansi na Teknolojia kupitia Elimu.
 
Meza Kuu.
 
Pichani Juu na Chini ni wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
 
Profesa Mbarawa akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI. 
 
Mgeni rasmi Waziri Mbarawa akiondoka ukumbi baada ya uzinduzi.
 
 Kwa hisani ya johnbadi.blogspot.com 

GEITA DOCUMENTARY

Contributors