Sunday, 27 October 2013

MAHAFALI YA KIHISTORIA SHULE YA WAMA NAKAYAMA,WAHITIMU NA VICKY KAMATA WAKONGA NYOYO ZA WATU, MGENI RASMI RAIS DK. JAKAYA KIKWETE ASHUKA JUKWAANI KUCHEZA.

   Imeandikwa na Steven Mruma.  

Siku ya jumamosi ilikuwa ni mahafali ya kwanza na ya kihistoria ya shule ya sekondari ya wama nakayama iliyopo Rufiji, shule hii ni moja kati ya foundation ya Mama Salma Kikwete [WAMA] ambayo inasomesha wanafunzi zaidi ya 800, katika mahafali hayo mgeni rasmi alikuwa Mh. Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya M. Kikwete.
    Katika mahafali hayo yaliambatana na burudani mbalimbali za muziki pamoja na vikundi vya sarakasi nk. moja kati ya wasanii waliotoa burudani ya aina yake ni Msanii na pia Mbunge wa Viti Maalum Geita Mh.Vicky Kamata ambaye wimbo wake ulikonga nyoyo za wageni waalikwa pamoja na Mgeni rasmi ambaye aliamua kushuka kutoka jukwaa kuu na kuanza kucheza pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo. Msanii mwingine aliyetoa burudani ni Mjomba Mrisho Mpoto.
   Katika mahafali hayo pia yalihudhuliwa na Mwenyekiti mtendaji wa mashirika ya IPP Bwana Reginald Mengi ambaye alitoa ahadi ya kuchangia shilingi Bilioni moja [1] ndani ya miaka mitano [5] akiwa na maana ya kutoa milioni 200 kila mwaka kwa miaka mitano.
Msanii na pia Mbunge wa Viti maalum Geita Mh. Vicky Kamata akiimba pamoja na wanafunzi wanaoagwa [kidato cha kwanza hadi cha tatu]

Msanii na pia Mbunge Vicky Kamata akiendelea kutoa burudani

Wanafunzi wanao waaga wenzao wa kidato cha nne wakiwa tayari kuimba wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzao wakiongozwa na Msanii na pia Mbunge Vicky Kamata
M/kiti mtendaji wa makampuni ya IPP Media Bwana Reginald Mengi akiwa na Bwana Hasheem Ghalib ambao pia ni wafadhili wa  WAMA NAKAYAMA
Mh. Mbunge wa Viti maalum na Msanii wa Muziki Vicky Kamata akiimba wimbo maalum na wahitimu 

Wahitimu wakiimba kwa huzuni wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzao pamoja na Mh Vicky Kamata, wimbo huu ndio pia uliokonga nyoyo za wengi na hata mgeni rasmi aliamua kushuka kutoka jukwaa kuu na kujumuika kucheza  
Mgeni rasmi na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akiwa ameshuka kutoka jukwaa kuu kucheza pamoja na wahitimu na wageni waalikwa.

Rais Dk. Jakaya M. Kikwete akiwa mwenye furaha wakati aliposhuka kutoka jukwaa kuu kujumuika katika muziki uliokua ukiimbwa na Msanii na pia Mbunge wa Viti maalum Geita Mh. Vicky Kamata [kulia ni Mama Salma na Mh. Vicky Kamata aliyeshika Mic]

Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Salma Kikwete pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors