Thursday, 31 March 2011

RAIS ATEMBELEA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na utalii wakati alipofanya ziara yake ya kikazi wizarani hapo.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi pamoja wafanyakazi wa Wizara ya maliasili na utalii wakati wa ziara yake ya kikazi Wizarani hapo. (picha na Freddy Maro)

RAIS KIKWETE AKUTANA NA KAMISHNA MKUU WA UMOJA WA MATAIFA WA HAKI ZA BINADAMU

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Bibi.Navanethem Pillay wakati alipomtembelea na kufanya mazungumzo naye. (Picha na FreddyMaro)

TUTALA MAKOMA KUTOKA UK AMTEMBELEA MHE.KAMATA

Tutala Makoma alipomtembelea Mhe.Vicky Kamata nyumbani kwake na kulia ni Mr Gorge kutoka Praise Power na katikati ni Groly binti wa Mhe.

Tutala na Groly
Mhe. Kamata, Tutala na mrembo Groly katika Pozi

Wednesday, 30 March 2011

BACK TO AFRICA WITH PENNY

ZANZIBAR KUSAMBAZIWA UMEME WA BILIONI 54 NA JAPAN

Balozi wa Japan hapa nchini Hiroshi Nakagawa akikabidhi mkataba wa mradi wa umeme kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo Khamis Mussa


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Japan zimetiliana saini kutekeleza mradi mkubwa wa usambazaji umeme katika Kisiwa cha Unguja utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 54 

Akitia saini mkataba wa msaada wa mradi huo leo Mjini Zanzibar, Balozi wa Japan hapa nchini, Hiroshi Nakagawa alisema pamoja na matatizo yaliyoikumba nchi yake, lakini bado kuna umuhimu wa kuisadia Zanzibar.

“Watu wengi hapa Zanzibar wanasumbuka kwa ukosefu wa umeme wa uhakika, bila shaka mradi huu utasaidia kupunguza mzigo kwa Shirika la umeme” Alisema Balozi Nakagawa.

WAZIRI MKUU APOKEA ZAWADI YA PICHA TOKA WIZARA YA MAJI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi ya picha yake iliyochorwa kutoka kwa Naibu Waziri wa maji, Gerryson Lwange (wapili kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Lwange Ofisni kwake jijini Dar es salaam Machi 30.2011. Zawadi hiyo imetolewa na watumishi wa Wizara ya Maji


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maji baada ya kukabidhiwa zawadi ya picha yake iliyochorwa, ofisini kwake jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Jerryson Lwange akifuatiwa na katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Sayi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Wizara ya Maji baada ya kukabidhiwa zawadi ya picha yake iliyochorwa iliyotolewa na wafanyakazi wa Wizara hiyo, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Machi 30, 2011. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Jerryson Lwenge na Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Sayi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Enhanced by Zemanta

WAZIRI AZINDUA AFYA YA UZAZI NA JINSI KWA VIJANA

 Naibu Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Mh. fenela Mukangara akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa haki na afya ya uzazi na jinsia kwa vijana wa miaka 10-24 uzinduzi huo ulifanyika jana makao makuu ya vijana yaliyopo Mwananyamala jijini Dar es salaam. (Picha zote na Philemon Solomon)

Naibu Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Mh.fenela Mukangara akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa mradi wa haki na afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana wa miaka 10-24

Wadau kutoka sehemu mbalimbali wakifuatilia burudani iliyokuwa ikitolewa na masii wa muziki wa kizazi kipya Diamond katika uzinduzi huo.(hayupo pichani)

Tuesday, 29 March 2011

CAG AWASILISHA RIPOTI YA UKAGUZI KWA RAIS


Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali Ludovick Utouh akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete taarifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali na mashirika yake ikulu jijini Dar es Salaam(picha na Freddy Maro).

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI MONDULI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Engutoto (hawapo pichani) katika Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, wakati alipotembelea Shule hiyo kwa ajili ya kufunguwa Jengo la Bwalo wa Wanafunzi, Makamu Rais yupo Mkoani Arusha kukaguwa na kizinduwa miradi ya maendeleo. katikati Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Isidore Shirima.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, akitembelea mashamba ya kilimo cha mpunga katika mabonde ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli, wakati alipokuwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani Arusha leo. kulia Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Isidore Shirima

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Maabara katika Shule ya Sekondari Nanja Wilayani Monduli, alipokuwa katika mfululizo wa ziara yake ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Wilayani Monduli Mkoani Arusha. kulia Mbunge wa Monduli Mhe.Edward Lowassa na Mkuu wa Mkoa Arusha Mhe. Isidore Shirima.

TAMWA WAFANYA MKUTANO MKUU

 Betty Mkwasa (kulia) ambaye ni Mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) na Mkuu wa wilaya ya Bahi akipokea zawadi ya kumpongeza kwa kupata tuzo ya mwanamke aliyefanikiwa katika mambo ya mawasiliano kwa mwaka 2008 kutoka kwa Maryam Hamdani ambaye ni mwanachama wa chama hicho wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam
 
 Gladness Munuo na Nasima Haji Chumu ambao ni wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) wakikata keki kwa niaba ya wenzao huku wanachama wengine wakishuhudia mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) Ananilea Nkya akiwaeleza wanachama wa chama hicho (hawapo pichani) kuhusu mafanikio waliyoyapata kwa mwaka wa 2010 wakati wa mkutano mkuu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mzuri Issa ambaye ni mratibu wa TAMWA Zanzibar na kushoto ni Gladness Munuo.

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam. 

(Picha na Anna Nkinda -Maelezo)

Monday, 28 March 2011

MKASA WA LEO

MKE WA RAIS KUWA RAIS BILA MUME
 

Mke wa rais wa Guatemala ameamua kutengana na mumewe, kwa sababu mke huyo anataka kugombea urais.

Katiba ya Guatemala inapiga marufuku watu wa karibu wa rais kugombea urais. Msemaji wa mahakama ambapo talaka hiyo itashughulikiwa amesema, Edwin Escobar amesema mchakato wa talaka umeanza, kati ya Sandra Torres de Colom na rais Alvaro Colom, ambaye hawezi tena kuwania urais.

HASARA YA MAANDAMANO YA SYRIA

Serikali ya Syria inasema watu 12 waliuwawa katika maandamano ya Jumamosi, wakati fujo zilipozuka katika maandamano ya kupinga serikali katika mji wa pwani wa Latakia.

Watu kama 200 piya walijeruhiwa, pale watu wasiojulikana na waliokuwa na silaha, waliosimama mapaani, walipofyatua risasi dhidi ya raia.

Wakuu wanasema, waliouwawa wengi ni raia na askari wa usalama. Rais Bashar al-Assad wa Syria anatarajiwa kuhutubia taifa, baada ya maandamano dhidi ya serikali ya zaidi ya juma moja.

MASHAMBULIO GAZA KUENDELEA

Madaktari katika eneo la Gaza wanasema Wapalestina wawili wameuwawa katika shambulio lilofanywa na Israel.

Hayo yametokea siku moja baada ya wapiganaji wa Gaza kupendekeza kusitisha mashambulio, iwapo Israel piya itakubali.Israel inasema inawalenga wapiganaji.

Mashambulio yamezidi katika siku kumi zilizopita, katika eneo la Gaza. Hili ni pigo kwa wale waliotoa wito kuwa fujo za sasa zinafaa kusitishwa. 

WASANII WA FILAMU TZ WAKUTANA KUCHANGIA FEDHA ZA CLUB YAO YA MICHEZO





Kikao hicho cha watu 50 kilichoambatana na chakula cha mchana, kilifanyika jana Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam.
Lengo ni kukuza mfuko wa Club pamoja na kusaidiana wao kwa wao linapotokea jambo kama kuugua, kuuguliwa, kufiwa au kufariki, Kuoa au Kuolewa kwa kati ya wanachama wa Club hiyo.

Walifanikiwa kwa masaa machache waliokutana kukusanya kiasi cha fedha za kutosha kuanzia

UONGOZI WA VODACOM WAKUTANA NA RAIS KIKWETE

 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi, Vodacom Group Pieter Uys, wakati wa ujumbe wa kampuni hiyo ulipofika Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kuongeza uwekezaji nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare.

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi, Vodacom Group Pieter Uys, (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare (kushoto) na Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba, wakati wa ujumbe wa kampuni hiyo ulipofika Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kuongeza uwekezaji nchini.

Rais Jakaya Kikwete, akimkaribisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi, Vodacom Group  Pieter Uys, wakati wa ujumbe wa kampuni hiyo ulipofika Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kuongeza uwekezaji nchini, (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare. Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba. Picha na Mpigapicha Wetu

TUZO ZA KILI MUSIC AWARD

 Mbunge wa viti maalum CCM Mhe.Vicky Kamata akiwa na Mr Nkinga toka COSOTA wakitoa tuzo kwa mwanamuziki bora wa RnB ambaye ni Ben Po.
Mhe.Vicky Kamata akiwa tayari kukabidhi tuzo kwa mwanamuziki bora wa RnB
 
Ben Po akiwa na tabasamu zito mara baada ya kupokea tuzo ya mwanamuziki bora wa RnB.

Waigizaji maarufu nchini Raymond Kigosi (kushoto)na Steven Kanumba nao ndani ya nyumba.
Stara Thomas akiwa sambamba na mwanamuziki mkongwe wa Taarabu kutoka Zanzibar Bi.Kidude
 
Tuzo hizo zimehudhuriwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Emmanuel Nchimbi katikati akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa BASATA Gonche Materego kulia na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Angetile Osiah.
 
Jay Mo akiwa ametinga suti nzuri katika red carpet
Lina kutoka THT akitoa burudani
Enhanced by Zemanta

GEITA DOCUMENTARY

Contributors