Friday, 29 August 2014

MWISHO WA MATESO YA MTOTO ESTER MWENYE KISA CHA KUSISIMUA BAADA YA KUUGUA KANSA NA KUPELEKEA KUPOTEZA MGUU WAKE. HAYA NDIO ALIYOPITIA KATIKA KIPINDI KIGUMU CHA MAISHA YAKE HADI KUKUTANA NA VICTORIA FOUNDATION.

 Makala na Steven Mruma "Trust"
    Ilikua nikatika ziara ya mh. Mbunge Viti maalum Geita Vicky Kamata na mwenyekiti wa VICTORIA FOUNDATION, wakati ziara inaendea tulikutana na mama mmoja akiwa na picha za mtoto na picha zikionyesha hali mbaya ya mguu wa kushoto wa binti ambaye kwa wakati huo hatukua tunamfahamu.
     Baada ya kukutana na Mh. Vicky kamata mama yule aliomba msaada wa kusaidiwa angalau hela ya kununua dawa za maumivu ama pain killer kwa ajili ya mtoto ambaye tulimuona pichani nilistushwa na kauli ya Mh. vicky ya kukataa kumpa chochote Mama yule ambaye alijitambulisha kama mama mlezi wa mtoto kwakua mtoto yule alikua ni Yatima na aliongea akiwa serious kabisa "siwezi kukupa chochote kwakweli ila cha kukusaidia labda nikupe namba ya simu jioni unielekeze nyumbani kwako nije nimuone huyo mtoto mwenyewe na kama ni msaada nitampa baada ya kumuona" Alisema Mh. Vicky, angalau sasa nilielewa mantiki yake skuizi matapeli ni wengi sana na udhibitisho wa picha pekee hauwezi kutosheleza kujua kama kweli yule binti alikua mgonjwa kweli au la!
      Yule Mama  baada ya kusikia aliyoambiwa na Mh. Vicky hakua mbishi alikubali na kuondoka huku nyuma tukiwa na maswali mengi kama.kweli tulichokiona kwenye picha ilikua ni uhalisia kweli ama ilikua ni utapeli.
Hapa Ester alikua Tayari Bugando amelazwa
      Baada ya kumaliza mihangaiko kweli jioni yule mama alipiga simu na kutuelekeza nyumbani kwake ambapo wote tuliofika pale tulipigwa na butwaa tulimkuta binti mmoja akiwa na hali mbaya sana mguu ulivimba sana ulikua umeharibika sehemu kubwa sana  nilimuangalia mara mbilimbili Mh. vicky kwa jinsi alivyotahayari baada ya kumuona binti yule kuna wakati ambapo nilidhani labda hata alijutia kitendo chale cha kuja kumuona  binti yule ambaye tulifahamishwa kua anaitwa Ester.
    Niliangalia ambao walimuona Ester kwa mara ya  kwanza wakitokwa na machozi akiwemo Mh, Vicky pia hali ya mguu wa Ester ilikua ni ya kutisha yalikua ni maisha ya majonzi na mateso makubwa sana.
    Wote tuliokuwepo tulikua na hali ya mfadhaiko mkubwa sana. Baada ya kushuhudia hali ile na kuelezwa mambo machache kwa haraka sana VICTORIA FOUNDATION kupitia kwa mwenyekiti wake aliamua suluhisho sahihi kwa  Ester ilikua ni kumpeleka hospitali kutibiwa na sio msaada wa dawa na mambo mengine. Kwakua bado ziara ya Mh. Vicky ilikua ikiendela aliomba msaada Halmashauri ya wilaya Geita na kwa msaada mkubwa sana wa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Geita aliweza kutoa gari ambalo lilimchukua Ester hadi hospitali ya Bugando ambapo baada ya uchunguzi wa madaktari kwa haraka walisema njia sahihi ilikua ni kukata mguu.
     Taarifa hizo ziliongeza kilio cha Ester alilia kutwa nzima na kisa cha kilio chake hicho hakua tayari kabisa mguu wake ukatwe, alilia sana, Ester hakua tayari kabisa kukatwa mguu lakini pia pamoja na kilio chake aliamini kabisa kama akiletwa Muhimbili au Dar mguu wake hauwezi kukatwa.
      Baada ya ziara yake Geita Mh. Vicky alipita Bugando kwenda kujua kinachoendelea, alikuta bado kilio cha Ester cha kukataa katakata kukatwa mguu wake na alilia sana huku akisisitiza kwamba kama akifika Dar[Muhimbili] mguu wake hautakatwa. Basi baada ya kusikia hayo Mh. Vicky aliafiki bora Ester aletwe dar na mipango ilifanywa na hatimaye Ester mama mlezi na Mh. Vicky waliondoka Mwanza kwa ndege kuja Dar na wengine kuongoza msafara wa magari kurudi Dodoma na Dar.
     Baada ya kufika Muhimbili madactari pia waliakua na uamuzi mmoja tu wa kuukata mguu wa Ester na safari hii japo ni kwa huzuni lakini Ester aliafiki kukatwa mguu kwakua kulikua hakuna njia mbadala. na kwa haraka sana madactari waliukata mguu wa Ester kwa haraka na kuutua mzigo mzito ulioelemea maisha yake karibu yote ya utotoni.
      Kwasasa Ester anafuraha sana tofauti na mwanzo na baada ya kuuguza jeraha la kukatatwa mguu wake  hakuna maumizu zaidi. Baada ya tukio hili la kusisimua ambalo kwangu kama muandishi lilikua kubwa na la aina yake lilinivuta kuandika makala hii fupi kuelezea kisa hiki.
      Kwasasa Mtoto Ester analelewa na VICTORIA FOUNDATION ambayo pia ndio iligharamia mambo yote ya matibabu kwa gharama za matibabu pamoja na mahitaji yote ya msingi ktk kipindi chote cha kushughulikia matibabu yake hadi kukatwa mguu na huduma zingine..
Mtoto Ernest aliwahi kutibiwa na sasa analelewa na Kusomeshwa na VICTORIA FOUNDATION
     Baada yakisa hiki kifupi sasa nilikaa kwa uhuru na Mh. Vicky kamata na kuongea nae machache na katika mahojiano hayo alielezea namna ambayo VICTORIA FOUNDATION kama taasisi maalum ya kusaidia wenye shida hasa watoto yatima, walemavu, watoto wa mitaani pamoja na wajane inayo kila sababu ya kusaidia na kumsaidia mtoto Ester kwa ujumla kwakua ndio kazi kubwa ya VICTORIA FOUNDATION na pia nilimuuliza kwanini mara nyingi misaada yake ama ya viongozi wengi hasa wanasiasa inahusishwa na mambo ya kisiasa alinijibu kwa maneno machache na ninanukuu maneno yake " VICTORIA FOUNDATION sio taasisi ya kisiasa haifanyi kazi kwa matakwa ya kisiasa na kuanza kusaidia watu nilianza tangu nipo Benki kuu wakati ambapo sikujua kama nitakuja kugombea na kushinda kua mbunge viti maalum  Geita, kwaiyo nikiwa Mbunge ama nisipokua mbunge VICTORIA FOUNDATION itaendelea kusaidia wenye shida na hao watakaokuja na imani kwamba nafanya kwasababu za kisiasa ni watu waliokosa Uzalendo na wasiopenda kuona wenye shida wakisaidiwa na suala la kuweka katika vyomba vya habari ni kama kutoa hamasa ili watu wengne watambue kua yapo makundi yanahitaji msaada na mtu yeyote mwenye uwezo anayo nafasi kuwasaidia wenye shida na watu wasikariri kua kila anayesaidia basi ni kwasababu za kisiasa".. mwisho wa kunukuu..
 
   Ikumbukwe kua VICTORIA FOUNDATION haijanza na Ester wapo watoto waliowahi kutibiwa tatizo kama la Ester na wanaosomeshwa na kupewa kila kitu ikiwemo chakula malazi na mavazi na VICTORIA FOUNDATION na baadhi yao hawatokei jimbo analohusishwa Mh. Vicky kua anataka kugombea. na katika makala hii pia zipo picha mbalimbali za watoto wanaolelewa na VICTORIA FOUNDATION na pia picha za Ester amabye ndio msingi wa makala hii.
M/kiti wa VICTORIA FOUNDATION MH. VICKY AKIWA NA ESTER BUGANDO HAPA ALIKUA AKIPOKEA TAARIFA YA MATIBABU YA ESTER

HAPA AKIANGALIA MAENDELEO YA MGUU
ESTER AKIANDALIWA ILI ASAFIRISHWE KWA NDEGE KUELEKEA MUHIMBILI DAR ES SALAM KUTOKEA BUGANDO

ESTER AKIWA KWENYE NDEGE KUELEKEA DAR ES SALAM
HAPA NI BAADA YA ESTER KUKATWA MGUU NA ALISHIKA BAISKELI NI MAMA MLEZI WA ESTER IKUMBUKWE KUA ESTER NI YATIMA

ESTER AKIWA MWENYE FURAHA PAMOJA NA MH VICKY KAMATA NA M/KITI WA VICTORIA FOUNDATION
JEREMIA NA ERNEST PIA WANALELEWA NA VICTORIA FOUNDATION

GEITA DOCUMENTARY

Contributors