Tuesday, 11 December 2012

MR DENNIS KINABO NA MR MASOUD KOVA WALIPOTEMBELEA OFISI ZA VICTORIA FOUNDATION LEO

C.E.O wa Victoria Foundation Mh. Vicky Kamata 

C.E.O wa Victoria Foundation akiwa katika picha ya pamoja na Mr Masoud Kova na Dennis Kinabo

USIKU WA UHURU IKULU 9th DECEMBER



Mh Vicky Kamata akiwa na balozi wa Marekani nchini Mr. Alfonso E. Lenhardt




RAY C AMSHUKURU RAIS KIKWETE KWA MSAADA WA MATIBABU

 Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.Rehema aliyefuatana na Ma
ma yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.Kwa apande wake ,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwaajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.


Sunday, 9 December 2012

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dk.Jakaya Kikwete akiwasili katika gari maalum la Kijeshi na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara 2012 yanayofanyika kila mwaka Desemba 9, Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho hayo huku akisindikizwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadik.


 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho hayo

Kikosi cha ardhini Jeshi la wananchi la Tanzania JWTZ kipita kwa gwaride la heshima mbele ya Rais Dk. Jakaya Kikwete

Kikosi cha wanaanga Jeshi la wananchi JWTZ kikitoa heshima kwa gwaride kali mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete




GEITA DOCUMENTARY

Contributors