Friday 27 September 2013

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR MHE. BALOZI SEIF ALI IDDI AZINDUACHAPISHO LA MGAWANYO WA IDADI YA WATU KWA UMRI NA JINSI.

    Makamu wa pili wa rais Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi (Mb na MBW) Amezindua chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu kwa umri na jinsi katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es salaam siku ya tarehe 25 september 2013.
   Akizindua chapisho hilo Mh. Balozi Seif Iddi Alisema""
Serikali  zote Nchini zitaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo ndani na nje ya nchi kupitia mipango ya maendeleo ziliyo jiwekea ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na  Mpango wa kupunguza umaskini { Mkuza } katika kuimarisha Sekta ya Elimu, Afya na soko la ajira ili kuweza kukabiliana na kasi ya ongezeko la idadi ya watu hapa Nchini.  Mwenyekiti huyo Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati  akizindua chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu kwa umri na jinsi kwenye sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, akiwakabidhi baadhi ya viongozi na wananchi vitabu vya machapisho ya mgawanyo wa watu kwa umri na jinsi mara baada ya kuzindua rasmi chapisho hilo kwenye ukumbi wa kimataifa wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Anaye kabidhiwa ni M/kiti wa uchumi viwanda na Biashara Mh. Mahmudu mgimwa akishuhudiwa na Hajatt Amina M, Said wa pili kutoka kushoto na kulia ni Naibu waziri wa Fedha Saada Mkuya.
Viongozi mbalimbali wa serikali na wadau wa mashirika mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu kwa umri na jinsi uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es saalam.

Naibu waziri wa Fedha Saada Mkuya akitoa hotuba katika uzinduzi huo.
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia kwa umakini uzinduzi huo. kutoka kulia ni Mh.Vicky Kamata, Mh. Paul Kimiti, Mh, Mustafa Mkulo na Mh. Sophia Simba.
Mgeni Rasmi wa uzinduzi wa chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu kwa umri na jinsi Mh. Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi mwenyekiti wa uchumi viwanda na biashara Mh. Mahamudu Mgimwa chapisho hilona nyuma kulia ni Naibu waziri wa fedha Mh, Saada Mkuya.
Mgeni Rasmi wa uzinduzi wa chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu kwa umri na jinsi Mh. Balozi Seif Ali Iddi akimgawa chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu kwa umri na jinsi.
Mgeni Rasmi wa uzinduzi wa chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu kwa umri na jinsi Mh. Balozi Seif Ali Iddi akimgawa chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu kwa umri na jinsi kwa viongozi, wawakilishi wa mashirika mbalimbali na wananchi.

MAJANGA CHADEMA: MWENYEKITI, KATIBU NA WANACHAMA 380 WAHAMIA CCM HANDENI


    Uongozi wa juu wa Chama Cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Handeni Mkoani Tanga umekihama Chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wilaya na Katibu wake pamoja na wanachama 380 ambao wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)..
   Tukio hilo linalotoa taswira mbaya kwa CHADEMA  na ishara njema kwa CCM limetokea juzi katika kata ya Kwamatuku, ambapo Mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdallah Bulembo alifanya mkutano wake wa hadhara na kupokea wanachama hao wapya wa CCM kutoka CHADEMA.   
Viongozi hao wa Chadema ni pamoja na Mwenyekiti wa wilaya ya handeni, Luka Selemani, mwenyekiti wa kitongoji cha maguruwe, mjumbe wa Baraza Kuu Taifa (Chadema) na Mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya wilaya.

   
  Wengine ni Katibu wa wilaya hiyo, Athumani Ngido ambaye pia ni mjumbe wa baraza kuu Taifa na mwenyekiti wa kamati ya utendaji wa Mkoa wa Tanga., Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya wilaya hiyo, Jack son Fransis ambaye pia ni mwenyekiti wa kata ya Kabuku na mgombea udiwani wa Kata hiyo...
  
      Mbali na hao, wamo Mwenyekiti wa Tawi la umoja wa Vijana wa Tawi la Kwamatuku, Abrahaman Mtengwa na mjumbe wa kushughulikia migomo ya chama hicho, Juma Mkomba.. 
 
Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara, Bulembo alisema kukimbia kwa viongozi na wanachama hao ni ishara kuu ya chama hicho kusambaratika vipande vipande katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu...
 
Alisema kadiri siku zinavyokwenda Chadema kitazidi kusambaratika kutokana na baadhi ya viongozi wake kukumbatia madaraka huku wengine wakiachwa wapiga debe.


 

Wednesday 25 September 2013

WANANCHI WA JIMBO LA GEITA, WANUFAIKA NA MRADI WA SOLAR [UMEME WA JUA] WENYE THAMANI YA TSH. MILIONI 293 ULIOFADHILIWA NA MBUNGE WAO VICKY KAMATA.

      Wanachi wa jimbo la Geita mkoa mpya wa Geita Wanufaika na Mradi wa Solar Uliofadhiliwa na Mbunge wa viti maalum Geita Mh. Vicky Kamata wenye Thamani ya Shilingi Milioni 293.   Mradi huo umewafikia wananchi wote wa kata zote za jimbo la Geita.
      Akizungumzia ufadili huo Vicky Kamata amesema Solar zitasaidia kuboresha huduma za afya na Elimu Jimboni hapo, kwani changamoto ya kukosa umeme ilikua inarudisha nyuma maendeleo ya Jimbo hilo. "Angalau sasa wanachi wa Geita watanufaika na ufadhili huo katika secta ya afya na Elimu ambao ndio nguzo kuu za maendeleo", alisema Mh. Vicky katika Hafla ya Kufunga Solar hizo iliyo hudhuliwa pia na mkuu wa wilaya ya Geita Mh. Manzie Mangochie ambaye alikuwa mgeni rasmi.
     Maeneo yaliyofungwa Solar ni Zahanati zote za jimbo la Geita na Nyumba za watumishi wa Afya pamoja na nyumba za baadhi ya Walimu na Shule za sekondari na chache za Msingi. 

Maeneo yaliyonufaika na ufadhili huu ni kama ifuatavyo:-

  •     Kwa upande wa AFYA kata zilizo nufaika na na ufadhili huo ni 

  1. Kata ya Nzela,- Kituo cha afya Nzela majengo nane [8] ya zahanati yalipata solar na nyumba nne [4] za waatumishi wa afya pia zilipata Solar
  2. kata ya Bugulula - Kituo cha afya Kasota Jengo moja [1] lilipata solar na nyumba mbili [2] za watumishi wa afya.
  3. Kata ya Bulela - Kituo cha afya  Bulela Jengo Moja [1]  lilipata solar  na nyumba mbili [2] za watumishi wa afya.
  4. Kata ya Lubanga - kituo cha afya Lubanga jengo moja [1] lilipata solar   na nyumba moja [1] ya mtumishi wa afya.
  5. Kata ya Nkome - kituo cha afya Nkome jengo moja [1] lilipata solar .
  6. Kata ya Senga - kituo cha afya Senga jengo moja [1] lilipata solar na nyumba mbili [2] za watumishi wa afya.
  7. Kata ya Lwenzela - Kituo cha afya Lwenzela jengo moja [1] lilipata solar na nyumba mbili [2] za watumishi wa afya.
  8. Kata ya Bugulula - Kituo cha afya Bugulula jengo moja [1] lilipata solar na nyumba moja [1] ya mtumishi wa afya.
  9. Kata ya Isulwa Butumbwe - kituo cha afya Kifufu jengo moja [1] lilipata solar na nyumba moja [1] ya mtumishi wa afya.
  10. Kata ya Bung`wangoko - kituo cha afya Nyakaduha jengo moja [1] lilipata solar na kituo cha afya cha Kishinda jengo moja [1]
  •   Kwa Upande wa Elimu maeneo yaliyonufaika ni kama ifuatavyo:-

  1. Kata ya Kakubilo - Shule ya Sekondari Kikubilo Solar Moja [1] na nyumba moja [1] ya mwalimu ilipata solar.
  2. Kata ya Bugalama - shule ya Shule ya Sekondari Bugalama solar Moja [1] na solar katika nyumba mbili [2] za walimu pia zilipata solar
  3. Kata ya Bung`wangoko- Bung`wangoko Sekondari Solar moja [1]. 
  4. Kata ya Katoma - Shule ya sekondari Katoma solar moja [1] na Shule ya sekondari Nyamboge solar moja [1].
  5. Kata ya Nyanguku - Shule ya sekondari Nyanguku Solar moja [1].
  6. Kata ya Kagu  - Shule ya sekondari Kagu Solar moja [1] na Nyumba mbili [2] za walimu zilipata solar pia Shule ya msingi Nyawilimilwa walipata Solar moja [1] na nyumba mbili [2] za walimu pia zilipata solar.
    Katika Kata za Kasamwa, Mtakuja na Karangalala Zipo katika Gridi ya taifa ya ememe na hivyo kuwa na uhakika wa kupata umeme kutoka katika Gridi ya Taifa.

Baadhi ya picha katika tukio la uzinduzi na ufungwaji wa solar jimboni Geita.

Mkuu wa wilaya ya Geita Mh. Manzie Mangochie akizindua mradi kwa kuweka jiwe la msingi la mradi huo [jiwe la msingi halionekani pichani] pamoja na Mbunge wa viti maalum Geita Mh. Vicky Kamata.
Viongozi mbalimbali wa chama na serikali pamoja na wananchi wakiambatana na mfadhili wa Solar ambae pia ni Mbunge wa viti maalum Geita Mh. Vicky Kamata walihudhuria ufungwaji huo wa solar
 
Mitambo ya kisasa ikiwa imefungwa kataka kituo cha afya Nzela.
Mh. Vicky Kamata Mbungewa viti maalum Geita akifatilia kwa ukaribu ufungwaji wa solar na nyuma ni Katibu msaidizi wa CCM wilaya ya Geita Bwana Kusaga.

Mitambo Solar system ya kisasa iliyofadhiliwa na Mh. Vicky Kamata ambaye ni Mbunge wa viti maalum Geita.

Baadhi ya Solar zilizofadhiliwa  na Mbunge wa viti maalum Geita Mh. Vicky Kamata.

Mafundi wa Solar wakifunga solar katika Moja ya Zahanati.

Baadhi ya wananchi hawakuwa nyuma walifuatilia kwa ukaribu ufungwaji wa Solar hizo popote pale walipokuwa na uwezo wa kufika.

Tuesday 24 September 2013

PICHA: TUKIO LA UGAIDI KENYA [WESTGATE MALL] JESHI LAKARIBIA KUDHIBITI MAGAIDI.. VICKY KAMATA BLOG NA VICTORIA FOUNDATION WATOA POLE.


Polisi wakipambana na Magaidi na Mwili wa mmoja wa raia wasio na hatia waliouwawa ukionekana sehemu ya kuingilia
    Mnamo siku ya Jumamosi Kenya ilikumbwa na Balaa la kuvamiwa na akuuwawa watu zaidi ya 50 kwa kupigwa risasi na magaidi wa kikundi cha al shabab katika Super market maarufu kama WESTGATE MALL Jiji Nairobi.
    Msemaji wa jeshi la Kenya kanali Cyrus Oguna alisema jumapili usiku kwamba jeshi hivi sasa linadhibiti kabisa soko la maduka ya kifahari mjini Nairobi  la Westgate Mall ambako watu 68 waliuwawa na wanamgambo wa kisomali wa kundi la Al-shabab.
mmoja wa majeruhi akpatiwa huduma
Anasema wengi wa mateka waliokuwa wamezuiwa ndani ya soko hilo kubwa wameokolewa lakini inavyoonekana washambuliaji wangali wanawashikiliwa mateka katika sehemu ya maduka na Jeshi la ulinzi la Kenya KDF linadhibiti jengo zima.  Anasema idadi ya watu wanaoshikiliwa mateka haijazidi 10.

Uvamizi wa jengo hilo unaingia katika siku ya tatu jumatatu na jeshi linakadiria kuna kati ya washambuliaji 10 hadi 15.

Wanamgambo wa kundi la Kisomali la Al-Shabab wamedai kuhusika na shambulio hilo na kutishia jumatatu asubuhi kwamba watawauwa mateka wote ikiwa jeshi litaendelea kuwashambulia.

Shambulio hilo lilianza takriban saa sita mchana kwa saa za Kenya  siku ya jumamosi katika soko la maduka ya kifahari la Westgate Mall na kusababisha vifo vya watu 68 na takriban 175 kujeruhiwa kufuatana na maafisa wa serikali.
      Akilihutubia taifa Rais Uhuru Kenyatta katika hotuba yake kwa hamasa aliapa  kusimama imara kupambana na kitisho cha ugaidi  akiongeza kusema kwamba vikosi vya usalama vya Kenya vina nafasi nzuri ya kuwashinda waliohusika na shambulio hilo.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyata.
 Akizungumza na Sauti ya Amerika-VOA mchambuzi wa masuala ya kiusalama na kijeshi Godwin Chilewa anasema huwenda kulikuwa na kasoro katika mfumo kamili wa usalama wa Kenya lakini ni vigumu kwa wakati huu kuvilaumu vikosi vya usalama hadi uchunguzi kufanyika.
  Anasema tatizo kuu linaweza kuwa ni ukosefu wa mawasiliano kati ya idara mbali mbali za usalama na namna ya kukusanya habari za kijasusi na jukumu la raia vile vile.

Rais Barack Obama amezungumza na kiongozi mwenzake Uhuru Kenyatta na kutoa rambi rambi zake na kuahidi uungaji mkono wa Marekani katika juhudi za Kenya kupambana na ugaidi.

    "VICKY KAMATA BLOG NA VICTORIA FOUNDATION WANAWAPA POLE WALE WOTE WALIOPOTEZA NDUGU ZAO NA PIA INAWAPA POLE NA KUWAOMBEA WAHANGA WA TUKIO HILO KWA UJUMLA,LAKINI PIA INAWAOMBEA WALIOJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO LA UGAIDI WAPONE HARAKA.

     VICTORIA FOUNDATION NA VICKY KAMATA BLOG KWA UJUMLA INALAANI KITENDO HICHO CHA KINYAMA KWA RAIA WASIO NA HATIA. 

   PIA TUZIDI KUIOMBEA NCHI YETU MUNGU AKAIEPUSHE NA MAJANGA KAMA HAYA AMBAYO YANACHUKUA ROHO ZA WATU WASIO NA HATIA NA KUONDOA NGUVU KAZI YA TAIFA KWA UJUMLA".


PICHA ZA TUKIO HILO, NA JINSI WANAJESHI POLISI KENYA WAKISHIRIKIANA NA MAKOMANDOO WA MAREKANI NA ISRAELI KUWADHIBITI MAGAIDI WALIOPO NDANI


Majeruhi akiwahishwa hospitali
Majeruhi akioka katika jengo akiwa amejeruhiwa vibaya
Maofisa uslama wakipambana na magaidi ndani ya WESTGATE MALL
Mauaji ya kinyama yaliyofanywa na Magaidi wa kikundi cha Al-shabab
Majeruhi akpatiwa huduma [akipandishwa kwenye ambulance]
mwili wa mmoja wa raia wasio na hatia waliouwawa na magaidi
Magaidi wa kikundi cha al-shabab wakionekana ndani ya jengo hilo wakiendelea kushikilia mateka na kuua watu wasio na hatia


Wahanga wa tukio hilo wakikimbia kunusuru maisha yao na pembeni ukionekana mwili wa mtu aliyeuwawa na magaidi hao
Majeruhi akiwahishwa hospitali
Wanajeshi wakiwa tayari kwa mapambano ndani ya jengo waliopo magaidi wa al-shabab
Hali inatisha ndani ya Jengo la WESTGATE MALL ni machozi na damu
Mwili wa mtu aliyeuwawa ukionekana ndani ya jengo la westgate mall.
Ulinzi usiku na mchana kuhakikisha magaidi hao wanatiwa mbaroni.
Jengo la westgate mall lifuka moshi wakati wa mapambano kati ya maofisa wa usalama na magaidi
Majeruhi akisaidiwa
majeruhi
Mama akiwa na watoto wake waliamua kujificha kwa style hii kuokoa maisha yao
Sehemu ya mgahawa ambao pia ulishambuliwa vikali na magaidi
Rai waliokuwa mateka wakitoka nje ya jengo baada ya kuokolewa na vikosi vya usalama
Wanausalama wakiwa kazini kupambana na magaidi  na mwili wa raia aliyeuwawa na magaidi hao wa al-shabab
Majeruhi akipandishwa kwenye ambulance
Baadhi ya raia waliokuwa wameshikiliwa mateka wakitoka baada ya kuokolewa.



Eneo la maegesho ya magari ikionekana miili ya watu waliouwawa na wengine wakiomba msada kwa ishara ya kujisalimisha.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyata akioa salamu za rambirambi kwa wahanga na pia kuzungumzia tukio hilo kwa ujumla.
Raia wakikimbia kutoka nadni ya jengo baada ya kuokolewa na vikosi vya usalama.
Wanajeshi wakiwa tayari kwa mapambno nje ya jengo
Wanajeshi wa kenya wakizidi kujipenyeza ndani ya jengo hilo kupambana na magaidi hao wa al-shabab.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors