Friday, 29 June 2012

 Mh. Vicky Kamata(wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mr. Phil Harris(kulia) ambaye ni Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Family Friend Community Connection-FFCC ya California Marekani inayosaidia watoto na maendeleo ya Afrika, Johan (wa pili kutoka kushoto) ambaye ni Assistant wa FFCC, Ms.Happy kutoka Singida na Mr.Steve wa Arusha(aliyesimama)
                               

Thursday, 28 June 2012

DOCTOR ULIMBOKA ATEKWA , NA KUJERUHIWA



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka ametekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, kisha kutupwa katika Msitu wa Pande, nje kidogo ya jiji Dar es Salaam.Daktari huyo ambaye amekuwa akiratibu mgomo wa madaktari unaoendelea, aliokotwa na msamaria mwema akiwa amefungwa mikono na miguu akiwa katika hali mbaya.

Baada ya kuokotwa na wasamaria wema na kufikishwa katika Kituo cha Polisi, Dk Ulimboka aliwahishwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) kwa matibabu, na ilielezwa kuwa hali yake haikuwa nzuri.

Taarifa za kujeruhiwa kwa Dk Ulimboka zilisambaa kwa kasi katika vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na ujumbe mfupi wa simu.

Wednesday, 27 June 2012

MABALOZI WAMUAGA DKT. ASHA ROSE MIGIRO




Mabalozi wa Afrika katika Umoja wa Mataifa wakimuaga Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayemaliza muda wake, Dkt Asha-Rose Migiro (mwenye kilemba katikati) , kwenye hafla iliyofanyika Washington Marekani, jana.



GEITA DOCUMENTARY

Contributors