Friday 25 March 2011

JESHI LA NATO SASA KUDHIBITI ANGA LIBYA

Majadiliano yanaendelea kuhusu nani aongoze harakati za kijeshi

Shirika la kujihami la NATO sasa limekbali kuchukua jukumu la kuthibiti anga ya Libya ili kuhakikisha marufuku ya ndege kutopaa inatekelezwa.Hatua hii imeafikiwa kwenye kikao cha waakilishi wa nchi wanachama wa shirika hilo mjini Brussels Ubeljiji.

Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema wanachama wote wa shirika hilo wameunga mkono uamuzi huo. Marekani ndio imekuwa ikisimamia utekelezaji huo lakini inataka kukabidhi wadhifa huo haraka iwezekanavyo.



Nchi wanachama wa NATO walikubaliana alhamisi usiku kuwa wachukue jukumu hilo na huenda wakakabidhiwa rasmi na Marekani katika siku mbili zijazo.

Kwa sasa shirika hilo linaongoza juhudi za kuzuia silaha kuingia Libya. Lakini bado haijaamuliwa ni nani atakae ongoza harakati za mashambulizi zinazoendelea katika lengo la kulinda raia wa Libya.

Katibu mkuu Rasmussen amesema kuwa wanajadiliana kuhusu uwezekano wa wao kuchukua wadhifa huo.Kuna baadhi ya wahusika ambao hawapendezwi na kuwa wanajeshi kutoka nchi za magharibi wanaendesha operesheni za kijeshi katika nchi ya Kiislamu.

Kufuatia tashwishi hizo, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Uturuki inasemekani wamekubaliana kimsingi kuwa usimamizi wa harakati zote za kijeshi nchini Libya zinakabidhwa shirika la Nato.

Ikiwa hivyo, baraza la mawaziri kutoka nchi wanachama wa NATO wakiwemo viongozi wa nchi za kiarabu zinazounga mkono hatua zinazochukuliwa dhidi ya Libya, watahusika kikamilifu katika maamuzi ya operesheni hiyo.

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors