Thursday, 26 December 2013

WALEMAVU NA WAJANE KUFADHILIWA VYEREHANI ZAID YA 100 NA VICTORIA FOUNDATION KUPUNGUZA UGUMU WA MAISHA

Na Steven Mruma [Geita]

     Walemavu na wajane watanufaika na ufadhili utakaotolewa na Victoria Foundation Kupitia kwa M/kiti wake Mh. Vicky Kamata ambaye ni mbunge wa viti maalum Geita, katika kuwezesha makundi hayo Victoria Foundation Itafadhili Vyerehani Zaidi ya Mia Moja (100+) vya kisasa kutoka Ujerumani na Uholanzi, na si hivyo tu pia Victoria Foundation itafadhili mafunzo ya walemavu hao na jinsi ya kutimia na kufanya matengenezo ya Vyerehani watakavyopatiwa.
    Mafunzo hayo yanataraji kuanza mapema mwakani maeneo ya Nyakato SIDO Mwanza katika Ofisi za SIDO mkoa wa Mwanza.
Baadhi ya vyerehani vitakavyotolewa kwa walemavu na wajane
    Katika ufadhili huo pia baadhi ya walemavu watapatiwa Tool Box ambazo zitakuwa na vifaa mbalimbali vya ufundi wa Baiskeli na pikipiki ili kuweza kuwasaidia walemavu katika vikundi vyao kujikwamua na ugumu wa maisha,,

    Ufadhili huo pia unalenga kuwapa mitaji wajasiriamali walemavu na wajane ili waweze kuinua bishara zao na kazi zao mbalimbali za kiuchumi ili kuhakikisha wanapunguza ugumu wa maisha.  akizungumza na Viongozi wa Vikundi vya walemavu na wajane waliofika katika hafla fupi ya kutambua na kutafakari jinsi ya kuwapunguzia wajane na walemavu ugumu wa maisha, ambapo mgeni rasmi alikua Mh. Vicky Kamata ambaye aliahidi kupitia Foundation Ya Victoria Foundation Kusaidia na kufadhili miradi hiyo ili kuwawezesha walemavu, watoto yatima, watoto wa mitaani, wajane na walemavu.
   Aidha Mh. Vicky alisema imani yake kubwa mlemavu pekee anayeweza kusimama kama mleamavu ni mlemavu wa akili tu lakini hawa wengine si walemavu na kwamba hilo ni jina tu lakini wanaweza kuyatengeneza maisha yao zaidi ya binadamu wengine waliokamilika viungo vyote.
    Aliongeza pia wanachokosa sana ni kuwezeshana tu na nafasi waliyoipata kutoka Victoria Foundation waitumie kikamilifu na pia ikawe elimu kwa wenzao sehemu mbalimbali kuwa hata walemavu pia wanaweza hasa wakiwezeshwa.


Mh. Vicky Kamata akizungumza na Viongozi wa vikundi mbalimbali vya walemavu na wajane


Picha ya pamoja na viongozi wa vikundi vya walemavu,

Picha ya pamoja na viongozi wa vikundi vya walemavu


 
Mh. Vicky akijiandaa kupiga picha na Viongozi wa vikundi vya wajane.
Picha na Viongozi wa Vikundi vya wajane Geita


Mh. Vicky Akipeana mikono na viongozi wa vikundi vya wajane.


PICHA UFUNGUZI WA LENNY HOTEL GEITA: HOTEL MPYA NA YA KISASA KABISA KANDA YA ZIWA.

Steven Mruma [Geita] 

   Ukifika Geita  bila shaka utakuwa umefika sehemu muafaka kabisa iwe ni kibiashara kikazi nk. Lenny Hotel ni hotel mpya na kisasa kabisa kwa kanda ya ziwa ikiwa na huduma nyingi na za kisasa. mawasiliano: - P. O. Box 105 Geita na Simu.+255765810684 na +255655319566.     

  


Huduma zinazopatikana Lenny Hotel

Mandhari ya Hotel Kwa nje
Mmiliki wa Hotel hiyo Leonard Bugomola akittambulisha wageni waliofika katika ibada ya kumshukuru Mungu na ufunguzi wa Hotel Hiyo Mpya

Baadhi ya Ndugu jamaa na marafiki wa Leonard Bugomola wakiwa katika sherehe za ufunguzi wa hotel hiyo

Mh. Vicky Kamata akipunga mikono baada ya kutambulishwa,
Ndugu na Marafiki wa Bugomola

Tuesday, 24 December 2013

GEITA MODERN TAARAB NA MKAKATI WA KUISHIKA KANDA YA ZIWA NA TANZANIA KWA UJUMLA.

 Na Steven Mruma [Geita]

   Ilikua ni mazoea ya kawaida sana kuona muziki wa  mwambao kuwika na kushika sana maeneo ya pwani na hasa visiwani Zanzibar, lakini siku hazigandi na muziki wa taarab sasa upo kila mahali na unapendwa na karibu kila mtu, mkoani Geita lipo kundi la muziki wa taarab linaloitwa Geita Modern Taarab, bado ni kundi changa likikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa vyombo vya muziki na pesa kwa ajili ya kuanza kurekodi nyimbo zao.
   Kiongozi wa kundi hiloHadija Kabaju alito wito kwa wana Geita na watu wa Kanda ya ziwa kuwaunga mkono na kuwasaidia mambo mbalimbali ili kundi hilo liweze kufikia malengo yake kwa mantiki ya kutoa elimu na burudani ya aina yake na kuweza kuutangaza vizuri mkoa mpya wa Geita,
    Kiongozi huyo alitoa wito huo pamoja na shukrani zake kwa Mh. Vicky Kamata mbunge wa viti maalum Geita kwa kuwapatia msaada wa kinanda ambacho kitasaidia sana kukinyanyua kikundi hicho cha  Muziki wa taarab.
Mh. mbunge viti maalu Geita Vicky Kamata akiwakabidhi kinanda alichowazawadia kikundi cha muziki wa taarab, Geita Modern Taarab
Wanamuziki wa kundi la Geita Modern Taarab wakiwa na kinanda walichozawadiwa na Mh. Vicky Kamata.
Mh. Vicky Kamata akipeana mkono na Kiongozi wa kundi hilo Hadija Kabaju mwenye nguo nyekundu

Geita Modern Taarab
Mh. Vicky Kamata akizungumza na kundi la muziki wa mwambao Geita Modern Taarab

Mh. Vicky ambaye pia ni msanii wa muziki akisisitiza jambo alipokutana na kundi la Geita Modern Taarab,

Bila shaka kila mmoja alikua na furaha.

VIJANA WENGI WAMEKIMBILIA MJINI NA KUWAACHA WAZEE VIJIJINI WAKITESEKA,


     Katika ziara ya Mh. Vicky Kamata mkoani Geita alikutana na mambo mengi sana lakini familia hii ilikua ni kivutio cha kusikitisha kidogo, Vikongwe wawili walikuwa wakiishi pamoja maisha ya kujitegemea na walikua ki mtu na mkwewe, wakiishi maisha yaliyojaa kila aina ya dhiki ikiwemo kupata chakula kwa kuombaomba na kuishi nyumba duni huku wakionekana kuchoka kiasi cha kutomudu kufanya kazi yoyote inayoweza kuwaingizia kipato.
     Mara baada ya kufika kijiji na cha Nungwe Mh. Vicky alikutana na familia hii na ilikua na maisha ya kushangaza na yanayotia simanzi sana. ishuhudie katika picha.

Mmoja wa wazee ha akitoka kwenye nyumba wanayoishi yeye na mama wa mume wake [mkwewe]

Vikongwe hao wakiwa pamoja kulia ni Mama wa Mume wa Bibi wa upande wa kulia
Mh. Vicky akiongea kwa na Vikongwe hao na baadhi ya majirani pia walifika eneo la tukio

Mh.Vicky hakupenda wabaki hivihivi aliwazawadia kaga na pesa kidogo ya kujikimu.

Zawadi ya Kanga


katika picha ya pamoja na vikongwe hao

Wamependeza na zawadi zao za sikuuu hizi za mwisho wa mwaka.

Mh. Vicky akijaribu kuwauliza maswali
Nyumba wanayoishi

wakiwa na furaha baada ya kupata zawadi kutoka kwa Mh. Vicky

Hiki ni Choo na Bafu cha vikongwe hao

 

WATOTO WANAOLELEWA NA VICTORIA FOUNDATION WALIPOPATA FURSA YA KUJUMUIKA NA FAMILIA ZAO GEITA. [PAGE 2]

Na Steven Mruma 

   Watoto wawili wanaolelewa na Victoria foundation Ernest Masuuko Sunguye na Jeremia Julius walipata fursa ya kuwa pamoja na familia zao kwa muda huu wa likizo, watoto hao wanaosomeshwa na kupatiwa matibabu pamoja na huduma zote za msingi na mfuko Victoria Foundation wanasoma shule iitwayo Salvation Army English Medium iliyopo jijini Dar es salam.
   Watoto hao mmoja ambaye ni Ernest anaishi Genge Saba na Jeremia Anaishi Nungwe mkoani Geita.

   Baada ya siku ya kwanza jioni Jeremia kuwasili kijijini kwao Nungwe siku iliyofuata Ernest Masuuko naye aliwasili kijijini kwao Genge saba na mambo yalikuwa kama picha zinavyoonyesha.

 
Njia inayoelekea nyumbani kwao Ernest

Mjumbe akienda kumpasha habari mama wa Ernest kua kuna ugeni unafika nyumbani hapo

Mama yake Ernest akisubiri kwa hamu ugeni wa mwanae na Mh. Vicky Kamata

Ernest akishuka kutoka kwenye gari
Karibu tena Nyumbani Ernest
Ernest akipokewa na Mama yake kwa furaha.

Hapa akisalimiana na mama yake
Mama Ernest akipokea wageni wengine walioambatana na Mh. Vicky

Dada Jesca ambaye ni katibu wa Mh. Vicky akiwa na Mgodo wake Ernest nayeitwa kalebo na kulia ni Mh. Vicky Kamata

Monday, 23 December 2013

WATOTO WANAOLELEWA NA VICTORIA FOUNDATION WALIPOPATA FURSA YA KUJUMUIKA NA FAMILIA ZAO GEITA. [PAGE 1]

   Na Steven Mruma 

   Watoto wawili wanaolelewa na Victoria foundation Ernest Masuuko Sunguye na Jeremia Julius walipata fursa ya kuwa pamoja na familia zao kwa muda huu wa likizo, watoto hao wanaosomeshwa na kupatiwa matibabu pamoja na huduma zote za msingi na mfuko Victoria Foundation wanasoma shule iitwayo Salvation Army English Medium iliyopo jijini Dar es salam.
   Watoto hao mmoja ambaye ni Ernest anaishi Genge Saba na Jeremia Anaishi Nungwe mkoani Geita.

   Wa kwanza kufika kijijini alikuwa ni Jeremia na hali halisi ilikuwa hiuvi mara tu baada ya kuwasili kijijini.

Jeremia Julius

Jeremia akishuka kwenye Gari alipowasili kijijini kwao, Nungwe mkoani Geita

Akishuka kwenye Gari
Mama yake Jeremia akiwa haamini kumuona tena mwanaye Jeremia

Mama Jeremia akisalimiana na mwanaye
Mama Jeremia akisalimiana na Mh. Vicky Kamata na hapa alikua akimuonyesha jeraha alilolipata mguuni.

Mara tu baada ya kuwasili ndugu jamaa na marafiki walianza kukusanyika nyumbani kwa akina Jeremia

Ndugu jamaa na marafiki wakiwa nyumbani kumsalimia Jeremia
Mh. Vicky akiwa na furaha baada ya kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa wanakijiji wa Nungwe

GEITA DOCUMENTARY

Contributors