Friday 15 November 2013

HAPPY BIRTHDAY DADA YETU CARO MUSHI.

 Na Steven Mruma.
  Happy birthday Dada Caroh Mushi kwa kutimiza miaka kadhaa MUNGU AKULINDE NA AKUPE MAISHA MAREFU YENYE BARAKA TELE. MUNGU AKUONGEZE HEKIMA NA UPENDO DAIMA Ameen.

PICHA ZA BIRTHDAY PART YA DADA CARO MUSHI.







 




RATIBA YA MAZISHI YA DR. SENGONDO MVUNGI.


LEO, NOVEMBA 15, 2013 – UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JK NYERERE



Saa 12:50 jioni
Kuwasili kwa mwili wa Marehemu – Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JKN


KESHO, NOVEMBA 16, 2013 – VIWANJA VYA KARIMJEE


Saa 2:00 – 3:30 asubuhi
Kuwasili kwa Wageni, Wananchi na Waombolezaji

Saa 3:30 asubuhi
Kuwasili Mwili wa Marehemu

Saa 4:00 – 5:45 asubuhi
Ibada ya Misa Takatifu, Viwanja vya Karimjee

Saa 5:45 – 6:55 mchana
Salaam za Rambirambi na Neno la Shukurani


Saa 6:55 – 8:40 Mchana
Kuaga Mwili wa Marehemu


Saa 9:00 Alasiri
Msafara kupeleka mwili wa marehemu Kibamba Msakuzi


KESHO KUTWA, NOVEMBA 17, 2013 – NYUMBANI KWA MAREHEMU - KIBAMBA, MSAKUZI


Saa 2:30 – 4:30 asubuhi
Ibada ya Misa nyumbani kwa marehemu

Saa 5:00 asubuhi
Kuanza safari ya kwenda Chanjale, Kisangara Juu, Mwanga, Kilimanjaro.
Na huko ndipo yatakapofanyika mazishi ya Dr. Mvungi.

Thursday 14 November 2013

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI NYUMBANI KWA MAREHEMU DR. SENGONDO MVUNGI HUKO KIBAMBA.

Rais Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Dr. Mvungi

Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma wakimfariji mke wa Dr. Mvungu Anna Mvungi mwenye nguo nyeupe nyumbani kwa marehemu Kibamba.
Rais Kikwete  wa pili kutoka kushoto akiteta jambo na M/kiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Warioba kushoto, wa pili kulia ni M/kiti wa NCCR - Mageuzi James Mbatia na kulia ni Mjumbe tume ya mabadiliko ya katiba na waziri mkuu mstaafu Salm Ahmed Salum

Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilali akimpa pole mke wa Dr. Mvungu Anna Mvungi alipotembelea kuwafariji nyumbani kwa marehemu Kibamba.
Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal akisaini kitabu cha Mombolezo
M/kiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Warioba akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Kibamba
Baadhi ya wajumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba wakitoa pole kwa mke wa marehemu

Baadhi ya viongozi waliofika nyumbani kwa marehemu Dr. Mvungi

Tuesday 12 November 2013

TANZIA: DR. SENGONDO MVUNGI AFARIKI DUNIA AKIWA KWENYE MATIBABU AFRIKA KUSINI


 Hayati Dr. Sengondo Mvungi enzi za uhai wake

Dr. Mvungi akiwa hospitali baada ya kujeruhiwa na majambazi kabla ya kufariki mchana wa leo.
Habari kutoka afrika kusini alikopelekwa dr. Sengondo  Mvungi baada ya kujeruhiwa na majambazi walipovamia nyumbani kwake hivi karibuni kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hasa maeneo ya kichwani.
   Hali Dr. Mvungi alibadilika na kuwa mahututi na kupelekea kupoteza maisha, tayari viongozi mbalimbali wa tume ya katiba akiwemo M/kiti wa tume hiyo Jaji J. Warioba wameshafika nyumbani kwa marehemu.

                 BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.


GEITA DOCUMENTARY

Contributors