Friday 13 July 2012

filamu ya SAYLA kuzinduliwa Leo Julai 13 ndani ya Naura Springs hotel, jijini Arusha...



Tarehe 13 Mwezi wa Saba, 2012 katika jiji la Arusha, filamu ya SAYLA itazinduliwa rasmi. Filamu hiyo iliyoshirikisha wasanii na watu maarufu takribani 27 ilirekodiwa maalum kwa ajili ya kuonyesha kuwa kwa kutumia sanaa, sisi watanzania tunaweza kusaidiana wakati wa matatizo. Filamu hii maalum kwa ajili ya kuwasaidia Sajuki na Wastara waliokuwa katika wakati mgumu wa kutafuta pesa za matibabu, itazinduliwa kwenye ukumbi wa Naura Springs na kuhudhuriwa na watu wengi maarufu nchini akiwemo Mh Shyrose Bhanji na wabunge wengine wa Bunge la Afrika Mashariki, Wema Sepetu akiongoza kundi la wasanii wa Bongo Movie pamoja na wengine kama Snura, Shilole ambao watatumbuiza kwa kushirikiana na Ndege mnana Linah, kwa mara ya kwanza jijini Arusha toka adondoke.


SAYLA ni filamu ya kihistoria iliyoshirikisha idadi ya kubwa ya mastaa kuliko yeyote ile itazinduliwa pamoja na video na behind the scene za nyimbo ya Mboni yangu!

Baadhi ya watu walioshiriki kwenye hiyo project ni kama ifuatavyo: Mh Zitto Kabwe, Mh January Makamba, Mh Halima Mdee, Mh Esther Bulaya, Mh Vicky Kamata, Mh Shyrose Bhanji, Mzee Chillo, Mzee Hashim Kambi, Muhogo Mchungu, Bi Kidude, Sharo Milionea, Mboto, Kitale, Wema Sepetu, Davina, Ephrahim Kibonde, Adam Mchomvu, Arnold Kayanda, George Goyayi, Mairmatha wa Jesse, Rose Chitala, Ruben Ndege, Irene Paul, Dully Sykes, Chege, Madee, Recho, Ommy Dimples, William Mtitu, Mwana FA na wengine wengi.

BAADHI YA PICHA ZA SCENE MBALIMBALI ZILIZOKO NDANI YA MOVIE YA SAYLA...

Hizi ni baadhi ya picha za scene mbalimbali nilizokuta nazo kutoka kwenye Filamu ya SAYLA. Kutana na watu maarufu waliomo ndani ya Filamu hiyo.. wakiwemo Wanasiasa na waheshimiwa mbalimbali, wanamuziki, waigizaji na wachekeshaji. ambao wote walijitolea kushiriki kikamilifu ili kuifanikisha Filamu ya SAYLA iweze kukamilika. Na uzinduzi wa Filamu hii unaanza wiki hii kwa kuanzia Arusha siku ya kesho, kuzunguka mikoa mingine husika na kuja kumaliziwa Dar es Salaam.



WEMA NDANI YA SCENE.



PRINCE DULLY SYKES NDANI.



MH. SHYROSE BHANJI NDANI.



SHARO MILLIONAIRE NDANI YA SCENE.



WAZEE NGULI WA MAIGIZO TANZANIA NAO WAMO.



YUSUFU NA ANGELA NDANI YA SCENE.



WATANGAZAJI ANOLRD KAYANDA NA ADAM MCHOMVU.


OMMY DIMPOZ NAYE YUMO.



ANGELA NDANI YA SCENE


WASANII WA BONGO FLAVA.. MADEE, CHEGE NA BARNABA.


WACHEKESHAJI KITALE NA SHARO MILLIONAIRE.



MH.ESTER BULAYA NDANI YA SCENE.



SIMPLE AKIFANYA VITU VYAKE NDANI YA FILAMU SAYLA.


MTOTO SAHIL FELLY KANO NDANI YA SCENE.


MTANGAZAJI MAIMARTA WA JESSE NA YUSUFU NDANI YA SCENE.



YUSUFU MLELA NDANI YA SCENE.



EPHRAEM KIBONDE NDANI.


IRENE NA YUSUFU.


MH.HALIMA MDEE NDANI.



MSANII RECHO NDANI YA SCENE.




RUBEN NDEGE NDANI.



AMBULANCE KAZINI NDANI YA FILAMU YA SAYLA.



BAADHI YA WAIGIZAJI WAKIWA MAKINI NDANI MOJA YA SCENE YA FILAMU YA SAYLA.















































Tuesday 10 July 2012

Wanaoiibia Tanesco watangaziwa ‘kiama’


  1.  

Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), William Mhando
MKURUGENZI wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco),  William Mhando amefanya ukaguzi wa mita za wateja baada ya kupata taarifa za kuwapo kwa watu wanaotumia umeme bila kulipia.Zoezi hilo ambalo lilifanyika jana Kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam, Mhando alisema   walipokea taarifa  za wizi wa umeme kwa njia ya mtandao hali iliyomlazimu kufuatilia kwa makini kuanzia ngazi ya chini.

Alisema tangu zoezi hilo kuanza wamefanikiwa kuwakamata watu wawili mkoani Dodoma na watatu jijini Dar es Salaam ambao kesi zao zimefikishwa mahakamani wakituhumiwa  kutumia umeme ambao haujulikani umenunuliwa wapi.

“Utakuta mteja amenunua umeme wa Sh10,000 kwetu lakini unapokwenda kukagua utakuta ana umeme wa zaidi ya pesa hiyo na hii inamaanisha kuna sehemu zingine wananunua tofauti na Tanesco ambapo kwenye mfumo haupo,” alisema  Mhando. 

Monday 9 July 2012

Ukosefu wa nishati vijijini ni janga la taifa


 

NI miaka 50 sasa tangu Tanzania ilipojipatia uhuru wake huku ikiendelea kuogelea kwenye lindi la umaskini. Siyo kwa sababu ya kukosa rasilimali, bali kutokana na sababu mtambuka.
Moja kati ya mambo yanayodhihirisha umaskini huo ni ukosefu wa nishati ya uhakika katika maisha ya kila siku na kwa maendeleo ya taifa.
Ni kweli tuna umeme wa Gridi ya Taifa, lakini hadi sasa umeme unatumiwa na asilimia 14 pekee ya Watanzania. Maana yake, hadi sasa asilimia 86 ya Watanzania hawana umeme huo, badala yake ama wanatumia umeme unaozalishwa kwa jenereta, jua au njia nyingine zisizo za uhakika.
Asilimia 14 ya hao wanaotumia  umeme ni wanaoishi mijini huku pia kukiwa na viwanda vichache vinavyozalisha bidhaa kwa masoko ya ndani na nje.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors