Friday, 30 November 2012

CATHERINE FOUNDATION YAZINDULIWA JIJINI ARUSHA LEO


Mbunge wa Viti Maalum -CCM,Mh. Catherine Magige akiwa na baadhi ya wadau wakati wakibadilishana mawazo kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa Catherine Foundation kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mapema leo Asubuhi.Pamoja na Uzinduzi huo wa Catherine Foundation pia iliweza kutoa msaada wa baskeli kwa walemavu wa wilaya ya Arusha.


Mbunge wa Viti Maalum,Umoja wa Vijana CCM,Mh. Catherine Maggige akisoma taarifa ya Foundation yake ilivyoanza kazi mbele ya Mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Mh. John Mongela na kuhudhuriwa na Wananchi mbalimbali wa jijini Arusha leo.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Mh. John Mongela (kushoto) na Mbunge wa Viti Maalum,Umoja wa Vijana CCM,Mh. Catherine Maggige wakisukuma Baiskeli za walemavu wakati wa kukabidhi Baiskeli hizo kwa walemavu watatu kwa niaba ya walemavu 20 waliopewa Msaada huo.


Picha na Ahmed Mahmoud

Sleeping with the fish: Dubai unveils hotel with rooms 10m under surface of the sea


 When it comes to outlandish new design ideas, Dubai is certainly ahead of the curve.
The glittering emirate has already got the tallest building in the world, the Burj Khalifa, and even the Earth itself - in the form of dozens of man-mad islands just off its coastline.
So it is no surprise to hear that architects are set to take on a new challenge - building a half-submerged hotel, complete with underwater rooms offering views of life below the surface of the sea.

 'Today, the advent of new technology made the heart of the ocean a setting not only for diving, but also for luxurious holidays,' said a spokesperson for BIG InvestConsult, a Swiss company behind the development.

The hotel will be made up of two main discs, one above water and one below, they will be connected by three 'legs' which contain lifts and stairways to plunge guests from the sunshine above down beneath the surface of the sea.
Room with a view: Special lighting will allow guests to enjoy the flora and fauna outside their window and macro photography will help them zoom in on even the tiniest creatures
The underwater section is located up to 10 metres deep and is composed of 21 hotel rooms adjacent to the submerged dive centre and a bar.

A special lighting system will illuminate the flora and fauna outside and the highest technology in the rooms will allow guests to zoom in and take a closer look at even the tiniest creatures using macro photography.

But nervous swimmers need not worry, they won't be left all at sea, DOT insists it has kept to the highest safety requirements.



KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI



KESHO Desemba mosi ni Siku ya Maadhimisho ya Ukimwi Duniani.
Hivyo basi kwa kuwa ni miaka kadhaa sasa tangu maadhimisho hayo yaanze kufanyika ni wajibu wa kila mmoja kuamua kwa dhati kuadhimisha siku hii.
Pia yatupasa kuwakumbuka ndugu jamaa na marafiki wetu ambao wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huu wa upungufu wa kinga mwilini.

Monday, 26 November 2012

BREAKING NEWS: SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA


HABARI ZISIZOTHIBITISHWA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE: Msanii mahiri wa uchekeshaji na mwanamuziki wa Bongo Fleva Sharo Millionea amefariki katika ajali ya gari huko Muheza mkoani Tanga. Tutaendelea kuwajulisha kadiri tutakavyopata habari zaidi.

ALICHOKISEMA KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA
Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”
Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.
Kwenye gari alikua mwenyewe. 

GEITA DOCUMENTARY

Contributors