Wednesday, 30 March 2011

ZANZIBAR KUSAMBAZIWA UMEME WA BILIONI 54 NA JAPAN

Balozi wa Japan hapa nchini Hiroshi Nakagawa akikabidhi mkataba wa mradi wa umeme kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo Khamis Mussa


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Japan zimetiliana saini kutekeleza mradi mkubwa wa usambazaji umeme katika Kisiwa cha Unguja utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 54 

Akitia saini mkataba wa msaada wa mradi huo leo Mjini Zanzibar, Balozi wa Japan hapa nchini, Hiroshi Nakagawa alisema pamoja na matatizo yaliyoikumba nchi yake, lakini bado kuna umuhimu wa kuisadia Zanzibar.

“Watu wengi hapa Zanzibar wanasumbuka kwa ukosefu wa umeme wa uhakika, bila shaka mradi huu utasaidia kupunguza mzigo kwa Shirika la umeme” Alisema Balozi Nakagawa.

Mradi huo ambao una lengo la kuboresha kituo cha kupokelea umeme Mtoni Unguja, ujenzi wa vituo vidogo vya umememe kwa njia tatu za Kv 33 yenye urefu wa Km 80.Alisema mradi huo unaosimamiwa kwa pamoja na Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani Kampuni ya VISCAS ya Japan ndio iliyopewa kazi ya ukandarasi kuweka waya kuanzia Fumba.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha uchumi na mipango ya maendeleo, Khamis Mussa alisema Serikali itachangia shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi mradi utakapopita.

Alisema mradi huo utasaidia mradi mkubwa wa umeme chini ya bahari kutoka Ras Kiromoni hadi Fumba unaofadhiliwa na Shirika la Changamoto za Milenia, hivyo mradi huo utasambaza umeme katika maeneo mengine ya Unguja.

Awali, Mwakilishi wa Shirika la misaada la Japan(JICA), Yukihide Katsuta alisema anaamini mradi huo unasubiriwa kwa hamu na wananchi wa Zanzibar hasa wakati huu ambao kuna matatizo ya upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Yukihide alisema Japan imekuwa ikilisaidia Shirika la Umeme Zanzibar(ZECO) katika mambo mbalimbali hivyo, anaamini mradi huo utakuwa chachu ya kukuza uchumi. Na Fatuma Mzee wa Maelezo Zanzibar.

No comments:

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI