Monday 28 March 2011

MASHAMBULIO GAZA KUENDELEA

Madaktari katika eneo la Gaza wanasema Wapalestina wawili wameuwawa katika shambulio lilofanywa na Israel.

Hayo yametokea siku moja baada ya wapiganaji wa Gaza kupendekeza kusitisha mashambulio, iwapo Israel piya itakubali.Israel inasema inawalenga wapiganaji.

Mashambulio yamezidi katika siku kumi zilizopita, katika eneo la Gaza. Hili ni pigo kwa wale waliotoa wito kuwa fujo za sasa zinafaa kusitishwa. 
Wizara ya Afya ya Gaza inasema watu wawili waliuwawa katika shambulio la ndege ya Israel isiyokuwa na rubani. Inasema mtu mwengine alijeruhiwa.

Hayo yametokea siku moja baada ya chama cha Hamas, ambacho kinaongoza Gaza, kufanya mkutano na makundi ya wapiganaji ili kujaribu kurejesha usalama. 

Baada ya mkutano huo Hamas ilitoa taarifa, kupendekeza mashambulio yasitishwe, ikiwa na Israel itasimamisha mashambulio.

Hamas inasema inataka kuzuwia mashambulio ya makombora dhidi ya Israel, lakini Israel inasema, shambulio iliyofanya ni dhidi ya kikundi cha wapiganaji ambao walikuwa karibu kufyatua makombora .
Wapalestina kama 10, wakiwemo raia, wameuwawa katika mashambulio ya Israel katika siku kumi zilizopita.Wapiganaji wamerusha makombora zaidi ya 80 kuilenga Israel

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors