Tuesday, 29 March 2011

TAMWA WAFANYA MKUTANO MKUU

 Betty Mkwasa (kulia) ambaye ni Mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) na Mkuu wa wilaya ya Bahi akipokea zawadi ya kumpongeza kwa kupata tuzo ya mwanamke aliyefanikiwa katika mambo ya mawasiliano kwa mwaka 2008 kutoka kwa Maryam Hamdani ambaye ni mwanachama wa chama hicho wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam
 
 Gladness Munuo na Nasima Haji Chumu ambao ni wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) wakikata keki kwa niaba ya wenzao huku wanachama wengine wakishuhudia mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) Ananilea Nkya akiwaeleza wanachama wa chama hicho (hawapo pichani) kuhusu mafanikio waliyoyapata kwa mwaka wa 2010 wakati wa mkutano mkuu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mzuri Issa ambaye ni mratibu wa TAMWA Zanzibar na kushoto ni Gladness Munuo.

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam. 

(Picha na Anna Nkinda -Maelezo)

No comments:

GEITA DOCUMENTARY