Friday, 21 December 2012

SERIKALI IGUSWE NA HALI YA SAJUKIMSANII maarufu wa filamu nchini, Sadick Kilowoko ‘Sajuki’, kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya hadi kupelekwa nchini India kwa matibabu.
Baada ya matibabu ya muda mrefu, msanii huyo alirejea nchini akiwa amepata nafuu kubwa tofauti na wakati anakwenda hivyo akawashukuru wote waliofanikisha gharama za safari yake.
Lakini pamoja na kurejea nchini akiwa amepata nafuu kubwa, bado akatakiwa kurejea India kwa uchunguzi na matibabu zaidi, kitu ambacho pia kinahitaji gharama kubwa ya fedha.
Kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu (Dennis Sweya), Sajuki anahitaji kiasi cha shilingi mil. 28, ikiwa ni gharama za kwenda na matibabu nchini India.
Zimebaki shilingi mil. 21 kupata kiasi cha fedha kinachohitajika kwa ajili ya msanii huyo kwenda India kwa matibabu zaidi katika kupigania uhai wake.

Kwa mujibu wa Sweya, katika kutafuta fedha zaidi za kujazia pengo la kiasi kinachohitajika, Sajuki amekuwa akipanda kwenye majukwaa.
Sajuki anaamini kupitia matamasha yake huko mikoani, walau atapata fedha za kuongezea kwani kiu yake ni kupata fedha zitakazomwezesha kwenda India kwa matibabu.
Kutokana na kuguswa na hali inayomkabili Sajuki, Sweya ametoa wito kwa wapenzi, mashabiki wa burudani na Watanzania wenye mapenzi mema kwa ujumla, kujitokeza kumsaidia fedha.
Sweya amedokeza kuwa hivi karibuni Sajuki alipanga kufanya onesho kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijiji Arusha, lakini alishindwa kutokana na hali ya kiafya.
Sisi Tanzania Daima tukiwa sehemu ya wadau wa michezo, sanaa, burudani na maendeleo kwa ujumla, tunadhani sasa ni wakati muafaka kwa msanii huyu kusaidiwa na mamlaka za juu serikalini.
Tunasema haya kwa kuzingatia kuwa katika hali ya kawaida, kiasi cha shilingi mil. 28 ni kikubwa ambacho kwa staili hii ya kuchangiwa, itachukua muda mrefu kuzipata.
Kibaya zaidi ni kwamba Sajuki anapoteza muda mwingi kutafuta fedha hizo za kumpeleka India, bila kujali athari ya kuchelewa huko, pia athari za kiafya zinazoweza kumpata kwa kupanda kwake jukwaani.
Wakati tukijielekeza kwenye mazingira magumu yanayomkabili Sajuki kwa sasa, tunakumbuka moyo wa huruma wa Rais Jakaya Kikwete kwa watu kadhaa akiwemo msanii Rehema Charamila ‘Ray C.’
Baada ya msanii huyo kulemewa na athari za matumizi ya dawa za kulevya, Kikwete akatoa msaada wa matibabu na msanii huyo ameweza kurejea kwenye hali ya kawaida.
Kwa dhamira njema kabisa, tunamuomba Rais Kikwete amtazame Sajuki kwa jicho la huruma, ikiwezekana amsaidie fedha ili aweze kwenda India kwa matibabu zaidi.
Kama Rais atafanya hivyo, atakuwa ameepusha athari zaidi zinazoweza kumpata Sajuki kwani kitendo cha kupanda jukwaani kusaka fedha za matibabu, ni kuongeza matatizo ya kiafya.
Ingawa ni vigumu kwa serikali kumsaidia kila mgonjwa, kwa gharama kubwa za matibabu zinazohitajika kwa Sajuki, ni busara kwa serikali kumsaidia.Habari na freemedia

7 comments:

Anonymous said...

[url=http://www.freewebs.com/effexorpills]will lose weight venlafaxine
[/url]effexor jaw pain
venlafaxina y embarazo
effexor usage
venlafaxine hcl back pain
venlafaxine winthrop lp 75 mg

Anonymous said...

Their large ears, and small mouths are a reminder to listen more than we speak.
Pets as presents seem like a great idea, but the logistics of owning a
pet came be very tricky. The oranges aren't really suited to eating - it's more like you are drinking fruit
than eating it, way too juicy.
Also visit my homepage - white elephant gift exchange ideas

Anonymous said...

[URL=http://pharmacypills.atspace.co.uk/buy-amitriptyline-canada/sitemap18.html]Map18[/URL]

Anonymous said...

Hi there, I enjoy reading all of your article. I like to write a little comment
to support you.
my page > Sex Show

Anonymous said...

[url=http://asacol-mesalamine.webs.com/]Salofalk buy
[/url] mesalamine online
pentasa 800 mg
order Apriso

Anonymous said...

[url=http://casodex-bicalutamide.webs.com/]buying Casodex
[/url] Pencial
generic Casodex
order Casodex online

Anonymous said...

[url=http://www.microgiving.com/profile/ribavirin]buy virazole online
[/url] copegus 100 mg
copegus
order rebetol online

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI