Friday 7 December 2012

MFUMUKO WA BEI MSIMU WA KRISMAS


WAKATI watu mbalimbali wakielekea mwisho wa mwaka katika msimu wa Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya, imegundulika kuwapo kwa uwezekano wa bei za bidhaa mbalimbali kupanda.
Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa habari hii katika baadhi ya maeneo ya jijini, umebaini kuwa baadhi yao wameanza kupandisha bei kwa bidhaa mbalimbali.
Katika Soko Kuu la Karikoo, bei za vyakula kama mchele na unga imepanda sanjari na maeneo mengine ya jiji.
Mchele kwa sasa umeanza kupanda kutoka Sh2,000 hadi Sh2,800 wakati katika baadhi ya maduka ya Supermarket umefikia Sh3,200.Bei ya unga wa mahindi imepanda kutoka Sh25,000 hadi Sh29,000 na pia bei hiyo pamoja na mchele inaweza kupanda zaidi.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo lililopo jijini Dar es salaam, walitoa ushauri kwa wateja wa bidhaa mbalimbali za vyakula kununua mapema mahitaji yao kabla bei hazijaanza kupanda kwa kasi na hasa ifikapo katikati ya mwezi huu.
Wakizungumza na gazeti hili walisema hali ya bei katika soko bado si shwari na kwamba upo uwezekano wa bei za vyakula kupanda baadaye ingawa kwa sasa bado siyo mbaya.
Juma Selemani ambaye ni mfanyabiashara wa sokoni hapo alishauri ni vyema kufanya ununuzi mapema ili kuepuka gharama kwa kupanda kwa bei katika msimu huu wa sikukuu ni lazima na haukwepeki.
“Misimu yote ya sikukuu hasa za mwishoni mwa mwaka, bei za bidhaa mbalimbali hupanda si tu bei za vyakula bali hata nguo na bidhaa nyingine,” alisema Selemani.
Baadhi ya wateja waliokuwa sokoni hapo walipozungumza na gazeti hili walisema kwa sasa ni mapema sana kuanza kununua mahitaji ya sikukuu kwa watu wengi wanategemea mishahara kwa hiyo ifikapo mwisho wa mwezi ndiyo wataweza kuanza kununua mahitaji yao.
Habari na mwananchi comm. 

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors