Tuesday, 5 April 2011

WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO MKAKATI WA TAIFA WA KINGA YA UKIMWI

 Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda kuzindua rasmi jarida lenye Mkakati wa Taifa wa Kinga ya UKIMWI (2009-2012), pamoja na Mpango Kazi kuhusu Jinsia na UKIMWI (2010-2012), katika uzinduzi uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam, Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro, na kulia ni Mkurugenzi katika Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na mapambano dhidi ya Ukimwi UNAIDS Michel Sidibe.

 Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro, zawadi ya picha ya kuchora yenye picha ya Pundamilia.

 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Dr. Asha Rose Migiro, akimtambulisha Mkurugenzi wa Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya Ukimwi (UNAIDS) Michel Sidibe, wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa taifa wa kinga ya Ukimwi.

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda pia alimkabidhi mkakati huo Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Dr. Fenela Mkuangara Waziri.

 Wakuu wa Taasisi mbalimbali na Idara za Serikali pia walihudhuria katika uzinduzi huo, wa pili kutoka kulia ni Mkurugezni wa (NIMRI) Dr. Mwelle Malecela.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro akisalimiana na akina mama viongozi mbalimbali, waliohudhuria katika uzinduzi huo.

No comments:

GEITA DOCUMENTARY