Monday, 4 April 2011

SIMBA YANYUKWA NA TP MAZEMBE

Mabingwa watetezi wa Kombe la Klabu Bingwa barani Afrika Timu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesonga mbele baada ya kuizaba Simba ya Tanzania kwa jumla ya magoli 3 – 2 katika uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam. 

TP Mazembe imesonga mbele kwa jumla ya magoli 6-3.Katika mechi ya awali iliyochezwa katika mji wa Lubumbashi TP Mazembe iliifunga Simba jumla ya magoli 3- 1. TP Mazembe ndio iliyokuwa ya kwanza kufunga goli kunako dakika ya 19 kupitia Given Sunguluma.

Kipindi cha pili Simba ilichachamaa na kupata goli la kusawazisha kunako dakika ya 51 lakini goli hilo halikudumu kwani mshambuliaji Alain Kaluyutuka alifunga goli la pili la Mazembe katika dakika ya 64 kabla ya kufunga goli la 3 kunako dakika ya 74.

Hadi mpira unamalizika Simba 2 TP Mazembe 3. Kwa matokeo hayo Simba itakuwa imetolewa kwenye mashindano hayo.

No comments:

GEITA DOCUMENTARY