Wednesday, 6 April 2011

WAANDISHI WA HABARI ZA UKIMWI WAPEWA TUZO NA AJAAT

 Mwenyekiti Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za UKIMWI(AJAAT) Simon Kivamo(kulia) akifafanua jambo wakati wa sherehe za kuwapa tuzo washindi wa shindano la waandishi wa habari kuhusu kuhamasisha wanandoa na wapenzi kupima Virusi vya UKIMWI (VVU) . wengine ni Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Gooffrey Majengo(katikati) na Simon Keraryo(kushoto) 
 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Guardian Gerald Kitabu akipeana mkono Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Gooffrey Majengo baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa uandishi wa makala zinazolenga kuhamasisha wanandoa na wapenzi kupima VVU ili kupambana na UKIMWI. 

Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima Helen Ngolemera akipokea cheti cha ushiriki  kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Gooffrey Majengo ikiwa ni kutambua mchango wake wa ushiriki wa uandishi wa makala zinazolenga kuhamasisha wanandoa na wapenzi kupima VVU ili kupambana na UKIMWI. Wengine katika picha na Mwenyekiti Mtendaji wa AJAAT Simon Kivamo (wa pili kutoka kulia) na Afisa Habari wa AJAAT Perege Gumbo (wa kwanza kulia)(Picha na Vicent Tiganya wa Maelezo- Dar es Salaam)

No comments:

GEITA DOCUMENTARY